Kiongozi wa waasi wa M23 ajisalimisha
Kiongozi wa waasi wa M23 Bertrand Bisiimwa ameripotiwa kusalimu amri kwa jeshi la Uganda. Kiongozi huyo wa waasi alivuka na kuingia nchini Uganda kwenye masururu wa magari mawili huku wanajeshi wa Umoja wa Mataifa na wale wa DRC walipofika kilomita tano kuelekea katika kambi yake ya kijeshi Mwandishi wa BBC Ignatius Bahizi amesema baada ya kuongea na afisaa mmoja wa usalama eneo la Bunagana alimthibitisha kujisalimisha kwa Bisiimwa akisema kuwa anahojiwa na maafisa wa usalama katika eneo la Bunagana katika mpaka wa Uganda na Congo DRC. Waasi wa M23 mnamo siku ya Jumatatu walitoroka maeneo yao ya vita ikiwemo eneo la Rumangabo baada ya kukabiliwa na mashambulizi kutoka kwa jeshi la UN na sasa inaarifiwa wametorokea msituni. Majeshi yanayopambana na waasi hao yamefanikiwa kuwashinda waasi hao katika miji waliyokuwa wameiteka na sasa kuna matumaini kuwa jeshi la DRC linaweza sasa kusitisha harakati za kundi hilo ambazo zilianza miezi 20