Posts

Showing posts from May 5, 2017

Watumishi wa zahanati mbili wote feki"

Image
Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali amefunguka na kusema zahanati mbili katika halimashauri yao zimefungwa kutokana na watumishi wake wote kukutwa na vyeti feki, jambo ambalo linapelekea wananchi katika kata hizo kukosa huduma.  Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali. Hamidu Bobali alisema hayo jana bungeni na kusema sakata la vyeti feki limeleta athari katika halimashauri yao "Hili suala la vyeti feki Mh. Mwenyekiti limeleta athari kubwa sana katika halimashauri yetu, hivi hapa napoongea kuna zahanati mbili zote zimefungwa kutokana na ukweli kwamba watumishi wake wote wameonekana na vyeti feki" alisema Hamidu Bobali  Mpaka sasa sakata la vyeti feki limeanza kuleta athari katika baadhi ya maeneo baada ya watumishi wengine kuamua kujiondoa wenyewe makazini kama amri ya Rais Magufuli ilivyoagiza kuwa wajiondoe wenyewe na kuachia nafasi hizo. 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA KUTANO WA ROTARY CLUB ARUSHA

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akivishwa beji ya uanachama wa Rotary Club na Dk. Manoj Desai kwenye mkutano wa 92 wa mwaka unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania (District 9211) katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 4, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Rotary Club kwenye mkutano wa 92 wa mwaka unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania (District 9211) katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 4, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa 92 wa mwaka wa Rotary unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania (District 9211) katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 4, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Washiriki wa Mkutano mkutano wa 92 wa mwaka wa Rotary unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania (District 9211) wakishangilia mara baada ya Waziri Mkuu kutangaza kuwa yeye na mke wake, Mary Majaliwa wanajiunga na Rotary Club katika ukumbi wa AIC...