Posts

Showing posts from June 21, 2013

KAULI YA MWIGULU KUHUSU BOMU LILILORUSHWA ARUSHA

Image
MWIGULU NAYE ADAI KUWA BOMU LILIRUSHWA NA CHADEMA...."KAMA SIO WAO, MCHUKUA VIDEO ALITAARIFIWA NA NANI KWAMBA BOMU LITARUSHWA???" Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba  amesema bungeni leo kwamba Chadema ilipanga kufanya shambulio la bomu kwenye mkutano wa Soweto jijini Arusha. Amesema hakuna jambo ambalo Chadema wamewahi kupanga wakashindwa. “Itakuaje mtu amechukua mkanda wa tukio la umwagaji wa damu bila kutikisika au mchukuaji kukimbia, haiwezekani- hiyo walipanga. “Inakuaje amechukua mkanda wa video kama mkanda wa harusi, yaani kama mkanda wa sendoff.? Amehoji Mwigulu huku wabunge wa CCM wakimuunga mkono kwa kupiga meza bungeni. Mapema wiki hii katika mkutano wa Chadema, mtu mmoja asiyefahamika alirusha bomu kwenye mkutano wa Chadema na kusababisha watu wanne  kufariki dunia na wengine 68 kujeruhiwa na kupelekwa katika Hospitali ya Mt Meru, Arusha.

"EDWARD LOWASSA ANAHUSIKA NA KUTEKWA KWANGU PAMOJA NI KIPIGO NILICHOPEWA"...NASSARI

Image
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amemtuhumu Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kwamba anahusika na kipigo alichokipata kutokana na chuki aliyonayo kwake. Aidha amemtuhumu Spika wa Bunge, Anne Makinda kwamba naye ni miongoni mwa watu wanaomchukia pamoja na viongozi wengine wa Bunge, kwa kuwa hakuna kati yao aliyempigia simu au kumtumia ujumbe wa kumjulia hali kutokana na kipigo alichopata ambacho kimemsababishia maumivu makali. Akizungumza jana akiwa kwenye chumba alicholazwa katika Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa na Ufahamu Muhimbili (Moi), Nassari alidai Lowassa ambaye amewahi kuwa waziri mkuu kabla ya kujiuzulu, amemchukia tangu alipomshinda mkwewe Sioi Sumari, kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika Aprili mwaka jana. Nassari aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Selian ya jijini Arusha kabla ya kuhamishiwa MOI, alidai kupigwa na kuchaniwa nguo na Green Guard wakati alipokuwa katika jitihada zake za kuhesabu kura kwenye ...

POMBE SI MAJI WAHENGA WALISEMA.....MWANAMKE AVUA NGUO NA KUCHEZA UCHI BAADA YA KUZIDISHA POMBE HUKO MBAGALA ZAKHEIM

Image
DADA mmoja ambaye jina lake halikuweza kujulukana mara moja aliuacha hoi umati wa watu waliokuwa kwenye baa moja hivi (jina kapuni) huko mbagala Zakheim mara baada ya kuvua nguo zote na kubaki uchi wa mnyama na hivyo kusababusha hali ya taharuki katika maeneo hayo.     Chanzo cha habari  kinadai kuwa dada huyo alifika maeneo hayo akiwa vizuri kabisa... Uchafu wake  ulianza baada ya yeye kunywa bia nyingi  mithiri ya mtu mwenye kiu ya maji .Pombe  ilipopanda kichwani, mrembo huyo alianza kukata mauno ovyo na  kusaula nguo mojamoja  mpaka  alipoyaanika na makalio yake..

PICHA ZA MAZISHI YA WAHANGA WA MLIPUKO WA BOMU HUKO ARUSHA

Image
  Picha za Mazishi ya mwenyekiti wa BAWACHA kata ya Sokoni I Judith William Moshi, aliye fariki kwa mlipuko wa bomu kwenye viwanja vya Soweto jijini Arusha siku ya kufunga kampeni za chaguzi ndogo tarehe 15.06.2013..

MTOTO AFANYIWA UPASUAJI KUONDOA MIGUU MIWILI YA ZIADA

Image
Mtoto wa miezi miwili wa kiume nchini Namibia amefanyiwa upasuaji wa aina yake baada ya kuwa amezaliwa akiwa na miguu minne.   Andrew Palismwe, anayetokea Caprivi, anaendelea vizuri na matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji uliochukua masaa tisa kuondoa miguu miwili kwenye Hospitali ya watoto ya Red Cross War Memorial  iliyoko mjini Cape Town, Afrika Kusini. Mtoto huyo sasa anaendelea kupata nafuu kwenye Hospitali ya Windhoek Central nchini Namibia, imeripotiwa. Alizaliwa akiwa na miguu miwili ya ziada chini ya tumbo lake Aprili 6. Hali hiyo inadhaniwa kuwa ni matokeo ya mapacha ambao hawakukamilika.   Daktari wa Hospitali ya Windhoek Central, Clarissa Pieper alisema: "Hii ni hali ambayo mapacha wameungana pamoja na kufuatia mimba ya mapacha ambayo hawakutengana kabisa, lakini kuunda watoto wawili wanaokua ndani ya kila mmoja. Katika suala hili, mtoto mwingine hauendelea kikamilifu."   Mama wa Andrew, Ruthy Mutanimiye alisema katika hospital...