Waziri Mkuu Akagua Shamba La JKT
Waziri Kassim Majaliwa amekagua shamba la uzalishaji wa mbegu bora za mihogo aina ya mkombozi linalomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi cha Rwamkoma wilayani Butiama. Amekagua shamba hilo linalomilikiwa na Kikosi cha JKT Rwamkoma leo (Jumamosi, Januari 20, 2018) alipowasili wilayani Butiama akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mara. Kikosi hicho kimewezeshwa na Halmashauri ya Butihama. Waziri Mkuu amewakipongeza kikosi cha JKT Rwamkoma kwa uamuzi huo wa kuzalisha mbegu bora za mihogo ambazo baadae zitasambazwa kwa wakulima wa zao hilo wilayani hapa.Pia amewataka wakazi wanaoishi karibu na shamba la kikosi hicho hilo kulitumia kama shamba darasa kwa ajili ya kujifunza namna bora ya kulima zao hilo. Kwa upande wake Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Kanali David Msakulo alisema shamba hilo linaukubwa wa ekari 60, na mbegu zitakazozalishwa zitatosha kupanda ekari 900.Mkuu huyo wa kikosi hicho aliongeza kuwa mbegu hizo zinazozalishwa katika shamba hilo zi...