SAFARI YA KINANA, MAKAMBO-DAR KWA TRENI
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akipanda behewa na wasaidizi wake, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (juu), wakati yeye na msafara wake waliposafiri kwa treni kwa zaidi ya saa 22, kutoka Stesheni ya Makambako na kuwasili Dar es Salaam, saa 12, 30, Desemba 9, 2013, kwa teni ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA), mwishoni mwa ziara yake ya zaidi ya siku 22, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za Wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua, katika Mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe. Treni ilitoka Makambako jana saa 2.30 asubuhi. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akishuka kwenye behewa na wasaidizi wake, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiani wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (juu), kukagua stesheni ya Mlimba, mkoani Morogoro, wakati yeye...