Posts

Showing posts from January 24, 2017

BREAKING NEWS : RAIS WA MAREKANI TRUMP AFUTA UFADHILI KWA MASHIRIKA YA UTOAJI MIMBA

Image
Donald Trump amerejesha utekelezwaji wa Sera ya Jiji la Mexico Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini agizo rasmi la rais kupiga marufuku kutolewa kwa pesa za serikali ya Marekani kufadhili mashirika ya nchi za nje ambayo yanatekeleza au kutoa habari kuhusu utoaji mimba.Afisa wake wa mawasiliano Sean Spicer amesema hatua hiyo ya rais inaonesha kwamba "anataka kuwatetea Wamarekani wote, wakiwemo wale ambao hawajazaliwa." Agizo hilo ambalo kirasmi linafahamika kama "the Mexico City Policy" (Sera ya Jiji la Mexico) huenda likayakera makundi ya kutetea uhuru wa wanawake kuamua kuhusu uzazi, ambayo tayari yametiwa wasiwasi na msimamo wake wa kupinga utoaji mimba.Bw Trump anaunga mkono utoaji mimba upigwe marufuku Marekani.Lakini hii si mara ya kwanza kwa marufuku dhidi ya ufadhili wa mashirika ya utoaji mimba nje ya Marekani kutolewa.Rais wa Republican Ronald Reagan mara ya kwanza alianzisha Sera ya Jiji la Mexico mwaka 1984 na k