Posts
Showing posts from May 19, 2014
WEMA, DIAMOND WACHAFUA HALI YA HEWA
- Get link
- X
- Other Apps
JAMBO limezua jambo. Pamoja na kuanza kwa kishindo safari yake ya kuelekea Afrika Kusini ‘Sauz’ kwa ajili ya fainali za kuwania Tuzo za MTV Africa (MAMA), mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na baby wake, Wema Isaac Sepetu wamechafua hali ya hewa, Ijumaa Wikienda lilikuwa linarandaranda ndani ya nyumba. Mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz 'akijidai' ndani ya ukumbi wa Club Billicanas. Pamoja na kufanya makamuzi ya kufa mtu kwenye shoo ya kuwatambulisha wasanii wanaowania tuzo hizo kwenye Ukumbi wa Bilicanas uliopo Posta, Dar, Diamond hakumpandisha Wema stejini kama kawaida yake, jambo lililozua kizaazaa. Kuna muda mashabiki wake walipiga kelele wakimtaka Wema apande stejini lakini hakufanya hivyo. Awali Diamond alipanda stejini mishale ya saa 8:00 akipishwa na msanii kutoka Sauz, Jigger ambaye alikuwepo kwa ajili ya kutoa sapoti kwa Mbongo Fleva huyo. Wema Sepetu akihojiwa na mmoja ya watangazaji katika ukumbi wa Billicanas. Msauz huyo alifa...
Angalia Picha Kijana Afia kaburini wakati akijaribu kufukua maiti
- Get link
- X
- Other Apps
Maiti ya kijana huyo ikiwa imenasa kaburini ukio la ajabu na la kushangaza limetokea huko nchini Nigeria baada ya kijana mmoja kukutwa akiwa amekufa kaburini,kijana huyo alikumbwa na umauti wakati akifanya jaribio la kufukua kaburi ili aibe fuvu la marehemu kwa ajili ya matumizi ya mambo ya kishirikina. Kwa mujibu wa mtandao wa Saturday Tribune wa Nigeria, tukio hilo limetokea katika mji wa Ilobu eneo oa Osun ambapo mtu huyo alikutwa akiwa amekufa huku nusu ya mwili wake ukiwa umeingia kaburini.Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa na marafiki zake wengine waliokuwa wanafanya tukio hilo lakini baada ya kuona mwenzao amenaswa ndani ya kaburi walikimbia na kumuacha akihangaika kujinasua,lakini jitihada zake ziligonga mwamba mpaka pale umauti ulipo mkuta. “Mwili wake ulikutwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi huku kichwa chake kikiwa kimefunikwa na tope. Wakazi wa eneo hilo waliripoti polisi na walikuja baadae wakautoa mwili...
Huyu Ndiye Msanii Mwenye Elimu Ya Juu "Masters"
- Get link
- X
- Other Apps
ufupi Wengi huanza kuchakaza viatu vyao wakipita ofisi moja baada ya nyingine kuomba nafasi za kazi zilizotangazwa na mwishowe hujikuta wakiwa wamefanya usaili zaidi ya ofisi 10 pasipo kuitwa kazini. Kwa kawaida vijana wengi Afrika, hususan Tanzania wanapohitimu elimu ya juu, jambo ambalo hulifikiria ni kutafuta ajira. Wengi huanza kuchakaza viatu vyao wakipita ofisi moja baada ya nyingine kuomba nafasi za kazi zilizotangazwa na mwishowe hujikuta wakiwa wamefanya usaili zaidi ya ofisi 10 pasipo kuitwa kazini. Hata hivyo hii ni tofauti na msanii wa Hip Hop kutoka Kundi la Weusi, Nickson Simon maarufu kama Nikki wa II ambaye ana shahada ya Uzamili katika maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDMS). Nikki wa II ambaye pia ni mshindi wa tuzo za muziki za Kilimanjaro 2014 KTMA kupitia wimbo Bora wa Hip Hop “Nje ya Box”, aliowashirikisha G Nako na Joh Makini wote kutoka Kundi la Weusi, anasema licha ya kwamba amehitimu elimu ya juu na k...
NABII WA TANZANIA ANAYEPONYA UGONJWA WA DENGUE KWA JUICE
- Get link
- X
- Other Apps
Baada ya time ya Babu wa Loliondo kuponya kwa kutumia kikombe,sasa ni time ya kiongozi wa dini ambaye anajiita nabii na kutangaza kuwa anatibu ugonjwa wa Dengue kwa kutumia juisi. Nabii huyu anayejulikana kwa jina la Yaspi Bendera baada ya taarifa zake kusambaa kumefanya baadhi ya wagonjwa kuanza kwenda kwenye kanisa lake la Ufunuo kwa Watu Wote lililopo Yombo Buza-Kipera. Ingawa Serikali imeonya vitendo vya baadhi ya watu kuwaondoa wagonjwa hospitalini na kuwapeleka kwenye maombi na kusema mtu yeyote anayesababisha wagonjwa kuondolewa hospitalini kwenda kufanyiwa maombi atachukuliwa kuwa ni adui namba moja,katika jitihada za kupambana na ugonjwa huo na kusisitiza kuwa wagonjwa ni lazima kwanza watimize dozi wanazopewa na wataalamu hospitalini ndipo waendelee na imani zao. Taarifa ya wataalam inasema kuwa ugonjwa huo unatokana na mbu aina ya aedes egypti sasa Nabii Yaspi anadai kuwa homa ya dengue ni pigo lililoletwa na ...
TASWIRA KUTOKA NYUMBANI KWA MAREHEMU KUAMBIANA....MWILI WA KUAMBIANA KUAGWA J’TATU NA J’NNE DAR
- Get link
- X
- Other Apps
Mke wa marehemu Adam Kuambiana, Janeth Rithe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kunduchi akifarijiwa. Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani Bunju B, Dar. Msiba upo hapa Bunju B. MWILI wa Mwigizaji na Muongozaji filamu maarufu Bongo, Adam Kuambiana utaagwa kesho Jumatatu nyumbani kwake Bunju B, Dar na siku ya Jumanne asubuhi utapelekwa Viwanja vya Leaders kuagwa na mashabiki wake. Taarifa hizi zimetolewa na mke wa marehemu, Janeth Rithe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kunduchi (Chadema)! swahilitz
UKAWA WAPATA PIGO MKOANI IRINGA.....WAPOKELEWA KWA MABANGO YA KUWAPINGA, MKUTANO WAGUBIKWA NA VURUGU KUBWA
- Get link
- X
- Other Apps
UMOJA wa Katiba ya Wananchi ( UKAWA ) umepokelwa kwa mabango yanayowapinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa yaliyokuwa yamebebwa na vijana.... Mabango hayo yalikuwa yanasomeka kuwa, "Tuna mashaka na ndoa ya UKAWA watauza nchi", huku yakisisitiza umuhimu wa vijana wa Wilaya ya Mufindi kutaka Serikali mbili..... Pia mabango hayo yalikuwa yanawataka wajumbe wa UKAWA warudishe posho kwanza bungeni mjini Dodoma.... Katika mkutano wao uliofanyika juzi mjini Mafinga Viwanja vya mashujaa, mkutano huo uliendeshwa na mwenyekiti wa chama cha Wan...
MASIKINI ADAM KUAMBIANA, ALIJUA KIFO CHAKE AKAJIANDAA LAKINI ALICHELEWA! KILICHOMUUA KIKO HAPA, KUAGWA KESHO LEADERS NA KUZIKWA KINONDONI
- Get link
- X
- Other Apps
KWELI kifo hakina huruma! Msemo huu umetimia juzi kufuatia kifo cha ghafla cha mwigizaji na mwongozaji wa filamu za Kibongo, Adam Philip Kuambiana (38) kilichotokea akiwa njiani kukimbizwa kwenye Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam baada ya kuugua. Kuambiana aliugua ghafla kwenye kambi ya kurekodi filamu na wasanii wenzake iliyopo katika Nyumba ya Kulala Wageni ya Silvarado iliyopo Sinza ya Kwaremmy, Dar. Aboubakar Katwila ‘Q-Chillah’ alisema muda mchache kabla ya kufikwa na mauti, Kuambiana alimlalamikia maumivu ya tumbo ambapo Ijumaa iliyopita alisema hali yake si nzuri kwani alikuwa akiendesha damu tupu. Q-Chillah alisema: Jana (Ijumaa) jioni Kuambiana na wasanii wenzake walikuwa baa wakinywa pombe hadi usiku mnene lakini bado aliendelea kulalamikia maumivu ya tumbo. Wenzake walimuuliza ni kwa nini alikuwa akiendelea kunywa pombe kama anaumwa? Akawaambia wamuache! Baada ya kumaliza kunywa kila mmoja alikwenda k...
MENEJA EWURA AJIUA HOTELINI BAADA YA KUHOJIWA NA BUNGE
- Get link
- X
- Other Apps
Dar/Dodoma. Meneja Biashara wa Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) amekutwa amekufa hotelini katika mazingira ya kutatanisha muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam akitoka Dodoma ambako alihojiwa na Kamati ya Bunge ya Bajeti. Meneja huyo, Julius Gashaza, ambaye alikuwa na jukumu la kupanga bei za mafuta za kila mwezi, alihudhuria kikao hicho mjini Dodoma kwa siku mbili; Ijumaa na Jumamosi iliyopita kuhusu mambo mbalimbali, yakiwamo kiwango cha mafuta kinachoingizwa nchini, mgawo wa fedha unaotolewa na Ewura kwenda kuhudumia umeme vijijini (Rea) na fedha za mfuko wa barabara. Jeshi la Polisi, Mkoa wa Temeke limethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa meneja huyo alikutwa amejinyonga kwa kutumia tai kwenye hoteli ya Mwanga Lodge iliyopo Yombo Vituka wilayani Temeke. Nyumbani kwa meneja huyo wa Ewura, kulikuwa na waombolezaji waliokuwa kwenye vikundi na kikao cha maandalizi ya mazishi kilifanyika ndani ya ny...