MTOTO Nice Valentino mwenye umri wa miaka mitatu na miezi tisa, ambaye ana vitu vingi vya kushangaza, ikiwemo kufundisha wanafunzi wa shule za sekondari, ameibuka ndani ya mjengo wa Global Publishers Ltd, Bamaga-Mwenge akiwa na baba yake mzazi na kuanika maajabu saba ya kushangaza, Risasi Jumamosi linakujuza. Mtoto Nice Valentino akikokotoa maswali aliyopewa na waandishi. AJABU LA KWANZA Kwa mujibu wa baba mzazi wa mtoto huyo, Valentino Swenya, aliyezaliwa katika wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Nice alianza kuandika maneno na namba za Kiingereza akiwa na umri wa miezi sita, jambo ambalo liliwashangaza sana. AJABU LA PILI Kadiri alivyokuwa akikua, ndivyo uwezo wake wa kuzungumza kiingereza ulivyozidi, lakini katika hali ya kushangaza, Nice hafahamu kabisa kuzungumza Kiswahili, lugha ya wazazi wake na anapolazimika kuongea, basi huongea kwa shida kama inavyowatokea wageni wanaojifunza lugha hiyo ya t...