MILIPUKO YA MABOMU YAUWA WATU ZAIDI YA 7A INDONESIA
Jengo la mgahawa wa Starbucks Coffee lililopo Mji Mkuu wa Indonesia, Jakarta ambapo mabomu hayo yamelipuliwa mapema leo. Milipuko ya mabomu takribani sita imetokea katika Mji Mkuu wa Indonesia, Jakarta na baadaye ufyatulianaji mkali wa risasi na watu zaidi ya saba wameripotiwa kuuawa japo polisi wanasema huenda kuna idadi kubwa zaidi ya waliouawa. Kati ya hao waliouawa ni maofisa watatu wa polisi, raia wawili akiwemo Mreno mmoja pamoja na washambuliaji watano. Polisi wa Indonesia wakijihami Milipuko imetokea maeneo kadha, ikiwa ni pamoja na mgahawani katika duka la kibiashara lililoko karibu na Ikulu ya rais wa nchio hiyo na ofisi za Umoja wa Mataifa (UN). Kuna ripoti za maafisa wa polisi kuonekana kwenye majengo na barabara za mji huo karibu na kituo hicho cha kibiashara. Eneo hilo limezingirwa na maafisa wa usalama. Rais Joko Widodo amehimiza raia wawe na utulivu na kushutumu “kitendo hicho cha ugaidi”. “Tunaomboleza watu waliofariki kwa sababu ya kisa h...