Waziri Jafo atoa agizo hili
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, ameagiza kufikia mwezi Desemba mwaka huu taasisi zote za serikali katika halmashauri ya jiji la Dodoma zinatakiwa kupata hati miliki ya maeneo yao. Aidha, ametoa muda wa mwezi mmoja kukamilishwa kwa ujenzi wa kituo cha afya cha Hombolo jijini hapa ambacho kimeonekana kuwa ujenzi wake upo nyuma ikilinganishwa na vituo vingine 208 vinavyokarabatiwa nchini. Jafo alitoa maagizo hayo juzi mara baada ya kupokea taarifa ya ujenzi wa kituo cha afya Hombolo iliyotolewa na Mganga wa kituo hicho kilichopatiwa fedha kiasi cha Sh. milioni 500 na serikali kwa ajili ya ukarabati. Katika taarifa hiyo ya ujenzi moja ya changamoto iliyotolewa na Mganga wa kituo hicho, Dk.Hosea Lotto alisema kituo hicho hakina hati miliki.Dk. Lotto alisema pamoja na majengo ya kituo cha afya Hombolo kuwepo toka mwaka 1968, lakini mpaka hivi sa...