Jerry Muro Aiponda Yanga, Adai Kuna Wanafiki
Aliyekuwa msemaji wa Klabu ya Yanga, Jerry Muro amesema kuwa ilikufanikiwa katika utendaji ndani ya uongozi wa mabingwa hao wa kihistoria ni lazima kuangalia ni nani anakuletea ushauri. Muro ameyasema hayo ikiwa ni sikuchache tu zimepita tangu Yanga imtangaze msemaji mpya wa timu hiyo, Dismass Ten aliyochukua nafasi yake. “Yanga kuna majungu watu wanapenda wafanye vitu vyao, kuna wanafiki ambao watakwambia ufanye hiki ukikifanya unaingia chaka. “Wapo Yanga SC watu wenye msaada wa kweli, wazuri sana, wenye akili na wenye mapenzi ya kweli kuhakikisha Yanga inakuwa kama TP Mazembe watu wote hao wapo Yanga. “Unachotakiwa kufanya ni kufungua macho kuangalia ni nani anakuletea ushauri, maana kuna mwingine anakuletea ushauri wakati yeye kashindwa kuongoza nyumba yake kaachana na mkewe ,hajali watoto wake yeye mwenyewe kufua nguo hafui nguo maisha yake yamemshinda,” alisema Jerry Muro aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo. Mungu anasema unapojipenda nafsi yako wewe mp...