Posts

Showing posts from October 20, 2018

Jinsi ya kuruka vihunzi vya mwanume anayekutongoza mara kwa mara

Image
Miongoni mwa kero ambazo huwakumbuka wadada wengi ni pamoja na kutongozwa, jambo hili  huwa halikwepeki kwani lipo tu. Hivyo kama wewe ni msichana ambaye upo  kwenye mahusiano na bado unaendelea kukutana na ushawishi wa kutongozwa kila iitwapo leo pindi ukutapokutana na mtu ambaye anakutongoza unatakiwa kuwa hivi. 1. Usijibu mtu huyo simu wala texts zake.  Kitu cha kwanza cha kufanya ni kuhakikisha kuwa haujibu simu zake wala kumtext hata kama umeboeka. Ukiwa unajibu simu zake basi utakuwa unampa matumaini kuwa uko interested na yeye. Ukimzima baada ya muda flani bila shaka atakuja kuelewa – ama unaweza tu kumpa ile hotuba ya kuwa wewe na yeye hamulingani. 2. Mblock katika mitandao ya kijamii.  Kando na kuwa hujibu sms zake wala simu zake, unapaswa kublock contacts zake zote katika mitandao ya kijamii ambazo unazijua. Kama unahisi kumblock utakuwa umevuka mipaka yakuonekana mb...

TFF Yapangua Kikosi Cha Simba

Image
Kikosi cha timu ya Simba SC. KIKOSI cha Simba ambacho kitashuka dimbani kesho kumenyana na Stand United kitakuwa na mabadiliko makubwa kutokana na sababu mbalimbali. Simba, kesho Jumapili itakuwa Uwanja wa Taifa kusaka alama tatu muhimu mbele ya Stand United. Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems amelazimika kukifanyia mabadiliko kikosi chake hicho kutokana na baadhi ya wachezaji wake kukumbana na adhabu mbalimbali kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Mabadiliko hayo ya kikosi cha Simba yanahusika zaidi kwenye safu ya ulinzi ambapo nyota wake wawili James Kotei na Erasto Nyoni wataukosa mchezo huo kutokana na kufungiwa na TFF. Wachezaji hao walibainika walifanya vitendo vya utovu wa nidhamu. Pia Simba itamkosa nahodha wake, John Bocco ambaye naye alikumbwa na adhabu hiyo. Kiungo Jonas Mkude anaweza kukosekana kutokana na kuwa majeruhi. Aussems ameliambia Championi Jumamosi kuwa, kutokana na hali hiyo amelazimika kukifanyia mabad...

ADAKWA AKITOA MAHARI NG’OMBE WA WIZI

Image
BUNDA: Dunia ina mambo! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia tukio la bwana harusi mtarajiwa, James Marwa, mkazi wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kunaswa akitoa mahari ya ng’ombe 10 wa wizi ili amuoe Prisca Faustine, mkazi wa Kijiji cha Kihumbu wilayani Bunda katika Mkoa wa Mara. Tukio hilo la aina yake limetokea Oktoba 3 mwaka huu, majira ya saa 3:00 katika Kijiji cha Kihumbu, Kata ya Hunyari, wilayani Bunda na kusababisha bwana harusi mtarajiwa huyo kuambulia kipigo na kukosa mke, kabla ya kuangukia mikononi mwa polisi. Tukio hilo la kufedhehesha lilimkumba Marwa baada ya Chacha Nyamahi, mkazi wa Kijiji cha Makundusi, Kata ya Nata wilayani Serengeti kuuarifu uongozi wa Kijiji cha Kihumbu kuwa anatafuta mifugo yake (ng’ombe) 48 ambao waliibwa wakiwa malishoni Oktoba 2, mwaka huu. Nyamahi alisema siku hiyo, akiwa safarini majira ya alfajiri, kijana mmoja alifika nyumbani kwake na kumkuta mkewe pamoja na mchungaji wa ng’ombe zake zipatazo 300 akawaambia ...

BREAKING NEWS: Bongo Muvi Yapata Pigo, Muigizaji wa Filamu Afariki Dunia

Image
BREAKING NEWS: Aliyewahi kuwa msanii wa maigizo wa Kundi la Sanaa la Kaole, Ramadhani Mrisho Ditopile maarufu kama Mashaka amefariki dunia katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam leo Jumamosi, Oktoba 20, 2018 majira ya saa 3, asubuhi.

Ratiba ya kuagwa na kuzikwa Isack Gamba hii hapa

Image
Marehemu Isack Gamba Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa zamani wa IPP media, kupitia Radio One na ITV kabla ya kuhamia Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani, Deutche Well DW, Isack Gamba anatarajiwa kuzikwa Bunda mkoani Mara mapema wiki ijayo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo  ya habari jijini Dar es salaam, mwili wa Isack Gamba utawasili nchini jumatatu ya wiki ijayo na shughuli ya kuaga mwili huo zitaanza wiki hiyo. Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa kwa upande wa Dar es salaam, msiba upo kwa dada yake, Gongo la Mboto, kituo kipya. Na kwa anayetaka kufika anaweza kuuliza Mongolandege kwa Mandai, Mbuyuni. Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo mara baada ya zoezi la kuuaga mwili wa Isack Gamba mwili huo utasafirishwa kuelekea Bunda Mkoani Mara mahali alipozaliwa kwa ajili ya mazishi ya mwili wake. Oktoba 18 mwaka huu kulisambaa taarifa juu ya kifo cha mtangazaji nguli wa zamani alikutwa akiwa amefariki nyumbani kwake mjini Bonn Ujerumani ambapo ilisadikika k...