EXCLUSIVE: Babu Seya, Papii Watuma Ujumbe Mzito Kwa JPM!
Papii Kocha (katikati) akiimba na baba yake Nguza Viking (kulia). DAR ES SALAAM! Kwa Wabongo walio wengi, majina ya Nguza Viking ‘Babu Seya’ na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ siyo mageni. Wao ni wafungwa wanaotumikia kifungo cha maisha ndani ya Gereza la Ukonga, Dar baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kulawiti na kunajisi watoto 10. …Wakipelekwa mahakamani kabla ya hukumu yao. Tangu kufungwa kwao, mwaka 2004, miaka 12 iliyopita, mengi yamesemwa, mengi yameandikwa, lakini wenyewe hawajawahi kufungua vinywa kusema lolote, hivyo kwa mara ya kwanza, Septemba 3, mwaka huu, Risasi Mchanganyiko, limekutana nao ndani ya gereza hilo na kufanya nao mahojiano yaliyochukua dakika 55. ILIKUWAJE? Septemba 2, mwaka huu, Risasi Mchanganyiko lilipata taarifa kwamba, wafungwa hao waliandika barua kwa Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ wakiomba msamaha kutoka kwake ili waachiwe huru. Ili kuweka sawa mzani wa habari, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu Mkuu wa Gereza la Ukonga, ACP Stephen...