Posts

Showing posts from March 23, 2016

Samatta hajakubali kuona rekodi ya Tanzania ikivunjwa na Chad mikononi mwake

Image
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars March 23 imeshuka katika dimba la Idriss Mahamat kucheza na wenyeji wao timu ya taifa ya Chad katika muendelezo wa michezo ya makundi ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika   (AFCON) itakayochezwa mwaka 2017. Huu ulikuwa ndio mchezo wa kwanza wa Mbwana Samatta akiichezea Taifa Stars kama nahodha wa timu hiyo, katika mchezo huo uliochezwa Chad , Taifa Stars imeibuka na ushindi wa goli 1-0, goli la Taifa Stars lilifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 30, baada ya kutumia vyema krosi ya Farid Musa . Samatta amefanikiwa kuitunzia Tanzania rekodi dhidi ya Chad , kwani mara ya mwisho Taifa Stars alikutana na Chad , ugenini na kufanikiwa kuibuka kwa ushindi wa goli 2-1. Magoli ya Taifa Stars wakati huo yalifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 11 na Nurdin Bakari dakika ya 88, huku goli la Chad la kufutia machozi lilifungwa na Mahamat Labbo dakika ya 12. Taifa Stars itarudiana na Chad Jumatatu ya March 28...

BREAKING NEEWWSS:RAIS MAGUFULI ATUMBUA JIPU TANESCO

Image
Rais Dk. John Pombe Magufuli. Rais wa awamu ya tano, Dk. John Pombe Magufuli anayesifika kwa utumbuaji wa majipu, safari hii ameifanya kazi hiyo kimyakimya, baada ya kuivunja Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco) iliyokuwa ikiongozwa na Dk. Mighanda Manyahi, Risasi Mchanganyiko linathibitisha. Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, bodi hiyo iliyokuwa na wajumbe wanane, ilivunjwa Machi 3, mwaka huu katika barua zilizosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Mhandishi Mussa Ibrahim Iyombe na kusababisha kuongezeka kwa idadi ya bodi za mashirika mbalimbali ya serikali zilizovunjwa. Bodi hiyo ya wakurugenzi iliyovunjwa, licha ya mwenyekiti wake Dk.  Manyahi ilikuwa na wajumbe ambao ni Dk. Haji Semboja (Makamu Mwenyekiti), Kissa Kilindu, Juma Mkobya, Shaaban Kayungilo, Dk. Mutesigwa Maingu, Boniface Muhegi, Felix Kibodya na Nyamajeje Weggoro. Mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina lake, alisema n...

Basi la Super Sami Lapata Ajali Tabora

Image
Aajali ilivyotokea. Ng’ombe wakiwa wamkufa baada ya kugongwa na basi hilo. Basi lapinduka na kujeruhi watu Igunga WATU kadhaa wajeruhiwa baada ya basi la Super Sami lenye namba za usajili T 819 DEN kutoka Mwanza kwenda jijini Dar es Salaam kupinduka katika Kijiji cha Igogo, wilayani Igunga mkoani Tabora leo wakati likijaribu kukwepa ng’ombe. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa taarifa za awali zinaonyesha dereva wa basi alikuwa anaongea na simu.

How do you block someone on Facebook?

Image
Quick Answer To block someone on Facebook, sign into Facebook, click the lock icon at the top of the page, and then select "How Do I Stop Someone From Bothering Me?" Enter the name of the person you wish to block, click Block, and then confirm the block request. Full Answer Sign on Sign into your Facebook account. Click the lock icon Click the icon that resembles a lock in the upper-right section of any Facebook page. This icon opens the Privacy Shortcuts dropdown menu. Locate the user Select "How Do I Stop Someone From Bothering Me?" In the dropdown menu, enter the name or email address of the person you wish to block, and then click Block. This action opens the Block People dialog box with a list of people you can block. Block the user Click the name of the user you wish to block in the "Are You Sure You Want To Block" dialog box. Click Block to confirm. If the person you want to block is not on the list, go ...

PICHA ZA AY NA PREZOO ZILIVUNJA NDOA YA DAYNA NYANGE

Image
Msanii wa muziki, Dayna Nyange amedai kilichosababisha wakaachana na mzazi mwenzake ni wivu wa mapenzi uliotokana na picha aliyopiga na wasanii wawili wa Kenya, Wahu na Prezzo pamoja na Mtanzania, Ambwene Yessaya ‘AY’. Muimbaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwae Rahma, ameliambia gazeti la Mtanzania, kuwa picha hizo alizipiga na wasanii hao kabla hajawa maarufu wala kujihusisha na muziki kwa kiasi kikubwa hivyo hiyo ilikuwa sehemu ya kutafuta marafiki wa kumsaidia kimuziki. “Kutokana na picha hiyo mchumba wangu huyo alihisi kwamba mmoja wa wasanii hao labda natoka naye kimapenzi hivyo akawa hataki nipige picha na wasanii na nisijihusishe tena na masuala ya kimuziki,” alisema Dayna. Aliongeza, “Muziki ni kitu ninachokipenda sana katika maisha yangu hapo nikaona wivu umezidi kwa mwezangu ambaye tumebarikiwa kupata mtoto mmoja wa kike mwenye miaka 10, tukaamua kuachana nami nikaendelea na muziki wangu hadi leo bila mchumba, mpenzi wala nini na maisha yana...

TAASISI YA MANJANO FOUNDATION KUENDESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE WA DODOMA

Image
Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi  Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers  ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation utaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Dodoma kuanzia Jumatatu, tarehe 28 March 2016 kwenye ukumbi wa  LAPF House Mkoani  Dodoma. Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake watakaochaguliwa 30 kutoka mkoani Dodoma na mikoa ya jirani.  Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Dodoma wanafikia malengo yao waliojiwekea. Wanawake wakazi wa Mkoa wa Dodoma waliotuma maombi na wanaopenda kunufaika na mradi huo  wanaombwa kujitokeza kwa ajili ya usaili siku ya Jumamosi tarehe 26 Machi 2016 kuanzia saa tatu (9:00AM) asubuhi kwenye ukumbi wa wa  LAPF House Mkoani Dodoma. Mafunzo yana lengo la  kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kum...

MWANASAYANSI ALIETENGENEZA VIRUS HATARI VYA UKIMWI

Image
Ameua maelfu na maelfu ya watu, alitengeneza ugonjwa huu mnamo miaka ya 1970, na sasa daktari huyu kwa jina   Robert Gallo   ametoka adharani na kusema amepata dawa ya kutibu ugonjwa huo.     Robert Gallo   anaelezwa kwamba alihusika na vita vya kibaiolojia kwa lengo la kuwaondosha watu weusi na mashoga duniani katika miaka ya 1970

MAGAZETI YA LEO JUMATANO TAREHE 23.03.2016

Image

MAGAZETI YA UDAKU LEO TRH 23/03/2016

Image

MKURUGENZI MTENDAJI WA EWURA AMTEMBELEA SPIKA

Image
     Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson kizungumza na Wajumbe wa  Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati Kamati hiyo ilipokutana na  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa.      Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimsikiliza Meneja Mahusiano wa EWURA Bw Titus Kaguo wakati walipomtemblea Ofisini kwake kati kati ni Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA Bw. Felix Mgamlagosi  (Picha na Ofisi ya Bunge )        Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson akifuatilia Mjadala kati ya  Wajumbe wa  Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na  Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa alipoitembelea kamati hiyo. Anayezungumza  kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Balozi Adadi Rajabu  na (kulia mwenye tai yekundu) ni Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Charles Kitwaga.  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA ...

SOKO LA FERI LATAKIWA KUTAFUTA GESI YA BEI NAFUU

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekea kwenye soko la samaki la Feri akitokea ofisini kwake Magogoni jijini Dar es salaam kukagua hali ya soko hilo Machi 22, 2016. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la kukaangia samaki kwenye soko la samaki Feri la jijini Dar es salaam Machi 22, 2016, Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mama Lishe wakati alipotembelea soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam Machi 22, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia Mama Lishe wakati alipotembelea soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam Machi 22, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Bodi ya soko la Kimataifa la Samaki la Feri, kukutana na makampuni mbalimbali yanayouza gesi ili kupata kampuni inayouza kwa bei nafuu zaidi lengo likiwa ni kuwapunguzia gharama wakaangaji wa samaki sokoni hapo. ...

SPIKA NDUGAI AFANYA MABADILIKO YA BAADHI YA WAJUMBE WA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE.

Image
Na Benedict Liwenga-Maelezo. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) amefanya mabadiliko ya baadhi ya Wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge ili kuzingatia mahitaji mapya na changamoto zilizojitokeza baada ya kuunda Kamati hizo mwezi Januari 2016. Taarifa hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Ofisi ya Bunge Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ambapo imeelezwa kuwa, mabadiliko hayo, yamefanywa chini ya Kanuni ya 116(3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge inayompa Spika Mamlaka ya kuteua Wabunge kuunda Kamati Mbalimbali za Bunge. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, kufuatia mabadiliko hayo ambayo baadhi yake yamehusu Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti au wote wawili, Kamati za Kudumu za Bunge zilizoathirika na mabadiliko haya zitawajibika kufanya Uchaguzi wa viongozi kwa mujibu wa kanuni ya 116 (10). Baadhi ya Kamati ambazo zimeathirika na mabadiliko hayo na ambazo zitawajibika kufanya uchaguzi kwa viongozi ni zikiwemo; Kamati ya Ardhi...