MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE AUSHANGAA UKIMYA WA MWIGULU NCHEMBA
Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete anamshangaa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuendelea kukaa kimya juu ya matatizo ya kiusalama kwa wananchi yanayoendelea nchini wakati yeye ndio kiongozi mwenye dhamana ya kulitatua hilo. Akiongea bungeni Jumanne hii, mbunge huyo amesema, “Kumekuwa na malalamiko mengi sana, tumeshuhudia malalamiko mengine yanahitaji majawabu kama siyo majibu ya haraka ili kuondoa hizi sintofahamu walizonazo wananchi.” “Niwaombe sana hakuna sababu ya mtu kama Mhe. Waziri Mwigulu kuendelea kukaa kimya wakati wananchi wanalalamika juu ya hali yakiusalama katika maisha yao,” ameongeza. “Mimi binafsi niishauri serikali yangu kwamba unapojibu jambo lolote lile unatoa hali ya wasiwasi,” amesisitiza.