LINAH: NAJUTA KUMUANIKA MPENZI WANGU

STAA wa Muziki wa Kizazi Kipya, Estelina Sanga āNdege Mnanaā amefunguka ya moyoni kuwa, kamwe hawezi kurudia kosa la kumuanika mpenzi wake kwenye mitandao ya kijamii au kwa watu na kukiri kuwa ndiyo sababu kubwa iliyochangia kuachana na mpenzi wake, William Bugeme. Akizungumza na Showbiz kwa hisia kali msanii huyo anayebamba na Ngoma ya No Stress alisema, hakuwa akijua kama kuanika uhusiano wake kwenye mitandao ya kijamii kutamletea majanga. āMimi tena kumuonesha mpenzi wangu nimekoma, najutaaa! Maana kwanza wakimjua wengine watajipendekeza na kumchukua na wengine watampelekea maneno ili tugombane hivyo bora nikae kimya labda wamjue siku ya harusi tu nimejifunza,ā alisema Linah.