Maskini Millen Magese..Ugonjwa Wake Waendelea Kumsumbua Afanyiwa Operation Mara 13...Ashindwa Kufanya Show Afrika Kusini
Akiwa kitandani, Millen Magese anaongea kwa tabu baada ya kuzidiwa katikati ya onesho la Mercedes Benz Fashion Week, jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Anawatoa hofu mashabiki wake kwasababu kilichotokea kiliwashtua. Akiwa kwenye kitanda cha hospitali, mwanamitindo huyo aliyewahi kuwa Miss Tanzania, anasema kiwango cha sukari kilikuwa kimeshuka kwa kiasi kikubwa kutokana na kupata maumivu makali na kutokwa damu nyingi kwa siku nane mfululizo. Millen akipewa huduma ya kwanza baada ya kuzidiwa Kutokana na tukio hilo, Millen ameshindwa kuendelea kushiriki kwenye show hiyo kubwa ya fashion. Maumivu anayoyazungumzia Millen si maumivu ya kawaida, ni maumivu makali. Mrembo huyo yupo kwenye vita vigumu na virefu dhidi ya ugonjwa uitwao Endometriosis. Ni ugonjwa ambao huhusisha seli zinazofaa kuwa ndani ya mji wa uzazi kuwa nje ya mji huo. Millen na wanawake wengine wanaosumbuliwa na ugonjwa huo hukabiliana na maumivu makali kila nyakati za siku zao za hedhi. N...