Posts

Showing posts from August 16, 2013

WASANII MAMISS FANI IMEWASHINDA NA WAMEKIMBILIA KUJIUZA......"THEA"

Image
BAADA ya wasanii waliotoka kwenye mashindano ya u-miss kuvuma sana na kupotea ghafla, msanii mkongwe kunako gemu la filamu Bongo, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ amefunguka na kudai utabiri wake umetimia. Akizungumza na mwandishi  wetu hivi karibuni, Thea alisema miaka kadhaa iliyopita alitabiri kuwa wasanii waliokuwa wanavuma sana ambao walitokea kwenye mashindano ya u-miss, hawatadumu kwenye uigizaji hivyo utabiri wake umetimia kwani sasa hivi, hawavumi tena. “Utabiri wangu unafanya kazi kwa sababu kwa sasa wale wasanii walioibukia kwenye mashindano ya u-miss wengi hawasikiki tena, wasanii wanatakiwa kutambua kuwa sanaa hii siyo lelemama yaani mpaka kufikia hapa tulipo tulifanya kazi ya ziada, tulisota sana kwenye vikundi,” alisema Thea

RAIS KIKWETE APOKELEWA NA RAIS JOYCE BANDA WA MALAWI KWA FURAHA LEO

Image
Rais Joyce Banda wa Malawi akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amuda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lilongwe tayari kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za SADC leo

DAKTARI ALIYEMTIBU SHEIKH PONDA MOROGORO ATIWA MBARONI...... CHAMA CHA MADAKTARI CHAPINGA NA KUDAI HANA KOSA

Image
Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ambaye alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Tiba na Mifupa (Moi), jana aliondolewa na kupelekwa katika Gereza la Segerea, Dar es Salaam.  Kitendo hicho kimelaaniwa vikali na familia yake na wafuasi wake, ambao wamepanga kufanya maandamano makubwa leo  ... Sheikh Ponda, ambaye alisomewa shtaka la uchochezi akiwa kitandani na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Tumaini Kweka ilidaiwa kuwa alitenda kosa hilo katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya Juni 2 mpaka Agosti 11, mwaka huu. Alisomewa mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Hellen Liwa. Jana, Polisi waliimarisha doria kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanzia saa 1:30 asubuhi. Magari matatu ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia(FFU) yaliyobeba askari wenye silaha yalionekana yakiranda katika maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.

WANANCHI WAUA MAJAMBAZI MAWILI JIJINI MWANZA...

Image
WATU wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi wameuawa na wananchi mkoani Mwanza wakati wakijaribu kuiba katika kituo cha mafuta cha GBP. Akizungunzumza na mwandishi wetu, shuhuda mmoja ambaye alikuwa eneo la tukio hilo alisema kuwa majambazi hao walifika katika kituo hicho cha mafuta wakitaka kuiba.

PICHA 100 ZA UCHI ZA MSANII MANAIKI SANGA NA MADEMU 30 ZANASWA. ....WAPO MAMISS KIBAO

Image
xdjay  imefanikiwa kunasa picha mbalimbali za aibu za msanii   chipukizi na mwanamuziki Manaiki Sanga akifanya ufuska wa kutisha na   wanawake tofauti tofauti hali inayoonesha ameazimia kujitoa muhanga   juu ya gonjwa hatari la ukimwi linalotishia dunia nzima.  Habari za uhakika toka kwa chanzo chetu kilichotushushia shehena za  picha hizo kilisema msanii huyo ambae pia ni anaigiza pamoja na kundi  la Ze Komedi la East Afrika Tv tangu apate jina amekuwa akijihusisha  na vitendo viovu vya unyanyasaji wa kijinsia kwa kuwarubuni mabinti  kupiga nao picha za aibu kwa lengo la kutafuta jina na amekuwa   akitumia kiasi kikubwa cha pesa kufanikisha suala hilo.  Aidha katika hali nyingine msanii huyo aliyetamba sana kwenye filamu  ya Love Position, Tikisa na nyinginezo amekuwa akitumia gari yake  kufanyia ufusika  hadharani..   <<  BOFYA  HAPA  KUONA  PICHA>>>

MAGARI MAWILI YAGONGANA NA TREKTA WATATU WAFARIKI DUNIA

Image
Mkuu wa wilaya ya Mbozi Dk. Michael Kadeghe akiwa na Mkuu wa Polisi wilaya ya Mbozi Ally Wendo katika eneo la ajali leo asubuhi Mabaki ya lori   Mabaki ya trekta TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI -AJALI   MNAMO  TAREHE 15.08.2013  MAJIRA YA    SAA 20:30HRS  HUKO KATIKA  KIJIJI CHA   CHIMBUYA BARABARA YA    MBEYA/TUNDUMA WILAYA YA    MBOZI  MKOA WA MBEYA.  GARI T.765 BBA AINA YA    SCANIA  LILILOKUWA LIKITOKEA MBEYA MJINI KUELEKEA TUNDUMA LILIENDESHWA NA DEREVA AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE LILIGONGA    TREKTA AMBALO HALIJAFAHAMIKA NAMBA ZA USAJILI KISHA KULIGONGA  GARI ACP 8839 AINA YA   SCANIA    MALI YA    KAMPUNI YA    USAFIRISHAJI YA    DHANDHO  LILILOKUWA LIKITOKEA TUNDUMA KUELEKEA MBEYA MJINI DEREVA WA GARI HILO BADO KUFAHAMIKA. KATIKA AJALI HIYO  WATU WATATU    WAWILI KATI YAO WALIKUWA KATIKA GA

BINTI ANYIMWA KUGOMBEA UONGOZI KWA SABABU NI MZURI KUPITA KIASI

Image
  Msichana mrembo kutoka Iran amejikuta akikosa nafasi ya uongozi katika halmashauri ya jiji lake kwa kuambiwa kuwa yeye ni mzuri sana hivyo amepitiliza sifa za nafasi hiyo. Nina Siahkali Moradi (27), alikuwa miongoni mwa wagombea katika uchaguzi wa halmashauri ya jiji la Qazvin nchini Iran, ambapo baada ya kura kuhesabiwa alikamata nafasi ya 14.  Lakini hata hivyo wiki moja baadaye kura zake zilifutwa na kiongozi wa halmashauri ya jiji hilo kwa maneno ya kejeli akimwambia “We don’t want a catwalk model on the council,”   Katika uchaguzi huo Nina alipata kura 10,000 na kumfanya akamate nafasi ya 14 kati ya 163, lakini wapinzani wake katika uchaguzi huo walilalamika kuwa Moradi alipigiwa kura kwasababu ni mzuri sana anavutia, pia mdogo.   Kwa mujibu wa The Independent, baraza huchukua washindi 13 wa juu na mgombea anayeshika nafasi ya 14 huwekwa kama ‘reserve’.

HUYU NDO KIJANA ALIYEKAMATWA NA MWAKYEMBE AKISAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA JN-DAR

Image
Habari ambayo imeripotiwa na ITV inadai  kwamba baada ya siku moja ya ziara ya kushtukiza ya Waziri wa uchukuzi Dk. Harison Mwakyembe kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar-es-Salaam, kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kimekamatwa uwanjani hapo katika harakati za kusafirishwa kwenda nchi za nje. Aliekamatwa ni kijana ambae alikua anazisafirisha hizo dawa zikiwemo bangi pia akielekea nchini Italia.

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WAOMBOLEZA KIFO CHA KATIBU MKUU IKULU MSTAAFU ABEL MWAISUMO

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo huku Mama Salma Kikwete akisubiri zamu yake wakati walipokwenda kuomboleza na kufariji wafiwa  kwa msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu Abel Mwaisumo aliyefariki juzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 16, 2013. Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo  kwa msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu Abel Mwaisumo aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es salaam  leo Agosti 16, 2013.    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuomboleza na kufariji wafiwa  kwa msiba wa Katibu Mkuu wa Ikulu mstaafu Marehemu Abel Mwaisumo aliyefariki majuzi huko India alikokuwa anatibiwa. Hapa ni nyumbani kwa marehemu Oysterbay jijini Dar es salaam  leo Agosti 16, 2013.

MWANAMKE ABAKWA NA KUCHOMEKWA KISU SEHEMU ZA SIRI HUKO SHINYANGA

Image
Mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30 amekutwa amekufa katika makaburi ya Majengo soko la mjini Kahama mkoani Shinyanga huku mwili wake ukiwa ametobolewa macho na kuonesha kupigwa na kitu kizito usoni. Mwanamke huyo ambaye hajatambulika jina lake na anakotoka alikuwa amevaa Blauzi nyeusi yenye madoa meupe, viatu vyenye urembo wa silva, mnene kiasi, mweusi na mwenye nywele ndefu. Mwili wa Mwanamke huyo amegunguliwa leo majira ya saa sita Mchana baada ya watu waliokuwa wanachimba kaburi kuuona mwili huo pembeni ya eneo hilo na kutoa taarifa Polisi. Kwa mujibu wa majirani wanaoishi eneo la makaburi hayo, tukio hilo linakisiwa kutokea usiku wa kuamkia jana huku baadhi ya kina mama wakisema kuwa walisikia sauti ya mwanamke akipiga mayowe katika eneo la mnadani.   Naye mwenyekiti wa kitongoji cha Majengo   Kaskazini Noel Mseven amesema amepata taarifa kutoka kwa wananchi na baada ya kufika katika eneo hilo walibaini kuwa sehemu za siri z

MWAKTEMBE AWAFUKUZA KAZI WALIOMSAIDIA AGNESS MASOGANGE KUPITISHA MADAWA YA KULEVYA KATIKA UWANJA WA NDEGE

Image
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa agizo kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kuwafukuza kazi na kuliagiza jeshi la Polisi nchini kuwaunganisha na wengine kwenye kesi mahakamani ili kujibu mashitaka ya jinai, wale wote waliohusika katika kuuwasaidia Agness Gerald na mwenziye Mellisa Edward kupitisha dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine "TIK" au "Meth" au "USAN" kilogramu 180 kuelekea Afrika Kusini Julai 5, ambako walikamatwa katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha O. R. Tambo nchini humo. Waziri Mwakyembe ametoa agizo hilo leo, ofisini kwake, mbele ya waandishi wa habari wakati alipowaita ili kuufahamisha umma kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizaa yake kuhusu suala la dawa za kulevya. Waliofukuzwa ni   Koplo Ernest, Yusuph, Jackson, Juliana Tadei na Mohamed ambao walihusika katika kuwasaidia Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Mellisa kupitisha dawa za kulevya kuelekea Afrika Kusini ambako walikama