Posts

Showing posts from April 22, 2018

Afande adakwa kwa tuhuma za rushwa

Image
MAMLAKA ya Kuzuia Rushwa na Kuhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) inamshikilia ofisa wa jeshi la polisi kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh. 250,000. Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Uhusiano wa ZAECA, Mwanaidi Suleiman Ally, alisema ofisa huyo Rajabu Juma Simba, mkazi wa Meli Nne-uzi, kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya zaidi ya Sh. 250,000  kutoka kwa vijana wawili ambao majina  yao yamehifadhiwa. Alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 4.30 asubuhi nje ya kituo cha polisi cha Mwanakwerekwe, baada ya kuwakamata na chombo walichokuwa nacho aina ya Pasola, kwa kuwatuhumu wanaenda kununua dawa za kulevya aina ya bangi. Alidai baada ya kuwapekua hakuwakuta nazo na kuwaamuru kwenda nao kituo cha polisi Mwanakwerekwe kwa mahojiano zaidi. Alisema mara baada ya mahojiano, ofisa huyo aliwaamuru vijana hao wampatie Sh. laki mbili ili awaachie na chombo chao, vijana hao walimpatia shilingi laki moja na baadae kuwachiwa wao na...

Yafahamu matatizo ya ngozi yanayotokana na kunyoa ndevu na nywele na jinsi ya kujitibu

Image
Wakati unaponyoa ndevu na nywele, baada ya kunyoa, wakati wa kuota nywele hizo zipo baadhi ya sehemu nywele hushindwa kutoka nje ya ngozi na kuota ndani ya ngozi hali inayopelekea kusababisha uvimbe na vipele. Zipo aina mbili za mapele yanayotokana na Kunyoa nywele na ndevu. Magonjwa haya ni kama ifatavyo 1. Acne Keloidalis Nuchae Acne keloidalis nuchae (AKN) Ni tatizo linalotakana na maambukizi ya bacteria P.Acnes kwenye ngozi baada ya kunyoa,hali inayopeleka vijitundu vya vinyweleo kuziba na kufanya nywele kushindwa kutoka nje ya ngozi na kukulia ndani ya ngozi hivo kusababisha mapele makubwa na makovu. Acne keloidalis nuchae (AKN) mara nyingi hutokea sehemu ya kisogo. Mbali na kunyoa tatizo hili pia huweza kusababishwa na uvaaji wa kofia. 2.Pseudofolliculitis barbae (PFB) Tatizo hili huwapata watu wengi, hili hutokea sehemu za kidevu na mashavu. Hii pia husababishwa na kuziba kwa vinyweleo vya ngozi baada ya kunyoa hivo kupelekea ndevu kukulia ndani ya ngozi na kus...