Posts

Showing posts from July 2, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Eng. Isack Kamwelwe kuwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kangi Lugola kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Meja Jenerali Jacob Kingu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Kailima Ramadhani kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Thomas Mihayo kuwa Kamishn...

SALAMBA,KAGERE WAIPELEKA SIMBA ROBO FAINALI YA KOMBE LA KAGAME CUP 2018

Image
Washambuliaji wapya wa  klabu ya Simba wameisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya APR  ya Rwanda Mchezo wa Michuano ya Kagame inayoendelea jijini Dar Salaam kwenye viwanja vya Chamazi na Taifa. Katika mchezo huo uliokuwa na mashambulizi ya zamu kwa zamu, ulimalizika dakika 45 za kwanza bila timu yoyote kuona bao. Mara baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, timu zote zilionesha kukamiana zikiwa na lengo la kucheka na nyavu ambapo mnamo dakika ya 66, Kinzingabo aliweza kuiandikia APR bao la kwanza. Ilichukua takribani dakika 6 baadaye Simba kuweza kusawazisha ambapo katika dakika ya 72, mshambuliaji aliyesajiliwa kutoka Lipuli ya Iringa, Adam Salama alifunga na kuufanya ubao wa matokeo kusomeka 1-1. Wakati mpira ukiwa katika dakika za nyongeza, straika hatari mpya, Meddie Kagere aliifungia Simba bao la pili na la ushindi kwa njia ya penati baada ya kiungo Said Ndemla kuangushwa katika eneo la hatari. Kwa Matokeo hayo Simba na ...

WIZARA YA AFYA YATANGAZA RASMI KUPOKEA HOSPITALI ZA RUFA ZA MIKOA

Image
WIZARA ya afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imetangaza rasmi kuanzia Juali 1 2018  imepokea Hospitali 28 za Rufaa za Mikoa ambazo zilikuwa chini ya usimamizi wa OR-TAMISEMI . Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala. “Hospitali ambazo tumezipokea zina jumla ya vitanda 7,474 na jumla ya watumishi 8,671 ambao, kati yao Wauguzi ni 3,960, Madaktari 536, Madaktari Bingwa wa fani mbalimbali ni 182, na waliobakia ni watumishi wa kada zingine mbalimbali za Afya” alisema Waziri Ummy. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo juu ya matangazo yaliyo kwenye mbao mapema leo wakati alipofanya ziara ya kukagua huduma za Afya zinazotolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala. Waziri Ummy amesema kuwa Hospitali ambazo Wizara imezipokea ni Ho...

Breaking News: Gari Lateketea kwa Moto Daraja la Kigamboni

Image
MOTO umewaka na kuteketeza gari dogo aina ya Toyota Ractics, leo Jumatatu, Julai 2, 2018 katika Daraja la Nyerere (Kigamboni) jijini Dar es Salaam huku mwenye gari akifanikiwa kutoka nje ya gari na kukimbilia sehem salama. Chanzo cha ajali hiyo imedaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme wa gari hiyo pindi limefika kwenye kukata ticket hitilafu hiyo imetoka na kuanza kuungua, juhudi za kuliokua gari hilo zilifanyika na kufanikiwa kuuzima moto huo hali likiwa limeshaungua mbele. Inadaiwa ajali hiyo imetokea wakati dereva wa gari hilo akilipia fedha ili avuke ng’ambo, lakini pia huku kukiwa hakuna taarifa ya majeruhi wala vifo vilivyoripotiwa kutokana na ajali hiyo. Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu.