UHURU KENYATTA AKANUSHA KUWEPO MVUTANO WA KIUCHUMI KATI YA TANZANIA NA KENYA
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Jumamosi alikanusha ripoti za vyombo vya habari kwamba kuna mvutano baina ya Kenya na Tanzania. Akizungumza mjini Mombasa wakati wa ufunguzi gati la makontena katika bandari ya Mombasa, Kenyatta alipuuzia maneno kwamba kuna mvutano wowote na badala yake akasema kuwa nchi hizo zinasaidiana. Alisema anaona kwenye vyombo vya habari kwamba kuna “mgogoro baina yetu, lakini nataka kusema wazi wazi kwamba Kenya na Tanzania hazina mgogoro wowote baina yao,” alisema.Kenyatta alisema uchumi wa nchi hizo mbili umefungana kwa miaka mingi na ni kwa ajili ya faida ya watu wa nchi hizo mbili. Alitaja kufunguliwa kwa njia inayojulikana kama “northern frontier” ambayo itaunganisha bandari ya Mombasa kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania, hadi Bujumbura, Burundi – njia ambayo itafupisha urefu wa kutoka Bujumbura hadi Mombasa kwa kilomita 300 nzima. “Afrika Mashariki haiko katika mashindano ya wenyewe kwa wenyewe,” alisema Kenyatta. “Afrika M...