Posts

Showing posts from August 10, 2015

Unamuwaza kila wakati, hakuwazi kabisa, wa nini?

Image
NAMSHUKURU Mungu kwa kunikutanisha na wewe msomaji wangu katika safu hii, hakika yeye ni mwema na ametujalia uzima ili na wewe uweze kupata kusoma kile ambacho nimekuandalia siku ya leo. Mapenzi ni dawa. Mapenzi yanatupa furaha, yanatingisha dunia. Hakuna kitu kizuri kama kupendwa. Umpate mtu akupende na wewe umpende. Dunia yote mnaiona ni ya kwenu. Pamoja na kuwa matamu, wakati mwingine hugeuka shubiri. Yanakuwa machungu pale mmoja wenu anapokuwa hampendi mwenzake sawasawa na anavyopendwa. Mmoja anapokuwa anampenda mwenzake wakati anayependwa harudishi upendo, penzi haliwezi kuwa na uhai mrefu. Linaweza kulazimishwa kwa sababu fulani lakini mwisho wa siku ukweli unabaki palepale. Naam! Hapo ndipo kwenye kiini cha mada yangu ya leo. Ambaye anapendwa ataleta visa ili mradi tu muachane, atafanya hivyo kwa sababu hakupendi. Yupo ampendaye. Si wewe. Wewe anakufanya wa akiba au maslahi fulani. Unayempenda anaweza kukudanganya. Akajifanya anakupenda kumbe hakupendi....

WEMA SEPETU AELEZA ‘MAHABA’ YAKE KWA JANUARY MAKAMBA!

Image
Brighton Masalu MTOTO ‘laini’ kunako tasnia ya urembo na filamu Bongo, Wema Sepetu ameeleza kwa hisia kali jinsi anavyompenda Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba katika utendaji kazi wake. Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, mbele ya naibu waziri huyo, Wema alisema miongoni mwa viongozi ambao humyima usingizi katika kuliongoza taifa hili kwa weredi mkubwa ni pamoja na Makamba. “Yeah, kusema ukweli nampenda sana Makamba, hakika ananivutia kwa mengi, hususan utendaji kazi wake,” alisema Wema.

BREAKING NEWS : MWENYEKITI WA CCM MKOA WA DODOMA ADAM KIMBISA ABWAGA MANYANGA.

Image
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, Ndg. Adam Kimbisa, aachia ngazi. Amedai kuwa anataka kumpumzika siasa ila wadadisi wa mambo wanasema ni maandalizi ya kuja UKAWA.  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

BREAKING NEWZZ, JESHI LA POLISI LAKANUSHA TAARIFA ZA KUPIGA MARUFUKU MSAFARA WA LOWASSA, SOMA HAPA WALICHOSEMA

Image
  Kamanda Kova asubuhi ya leo akiongea na ITV amekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo whatssap kuwa watu wasiokuwa na shughuli mjini wasiingie kwa sababu mgombea wa CHADEMA atakuwa anachukua fomu na foleni itakuwa kubwa pia itahusisha magari, pikipiki, guta, baiskeli na helikopta na wameweka jina langu, pili amesema maandamano yataanzia makao makuu ya CUF Ilala saa tatu asubuhi, njia waliyoandaa jeshi la polisi ya kiusalama itaanzia UFIPA, Kinondoni kupitia Salender Bridge kuelekea ofisi za NEC. Amewaambia wananchi waje mjini kama kawaida kwa sababu wengine rizki yao inategemea kuamka kwake na kujishughulisha asubuhi mpaka jioni na ukiwaachia tu watu kwa ajili ya kuchukua fomu itakuwa tatizo. Tunachukua fursa hii kukanusha haya maelezo sio ya kwetu hata jinsi jinsi tangazo sio namna yetu ya kuandika taarifa na watu waache kupotesha watu kupitia mitandao kwa sababu masuala ya kiusalama ni nyeti sana. Maandamano ni kitu sisi Polisi tunara...

Batuli aeleza sababu za kutoolewa.

Image
Yobnes Yusuph ‘Batuli’. Brighton Masalu STAA wa filamu Bongo, Yobnes Yusuph ‘Batuli’, ameeleza sababu zinazochangia yeye kutoolewa kuwa ni umaarufu wake. Akizungumza na mwandishi wetu pande za Mlimani City jijini, alisema kuwa wanaume wamekuwa wakiwahofia kwa sababu wao ni mastaa kama wengi wanavyoamini ukimuoa staa umeumia.“Natamani sana kuolewa ila wanaume ndiyo tatizo, wanatuhofia sisi mastaa, nawaambia wasiwe na hofu na mimi kwani nimetokea kwenye familia bora ambayo imenilea vyema,” alisema Batuli.

MAELFU YA WANACHAMA WA CUF WAJITOKEZA KUMLAKI LOWASSA BUGURUNI LEO, ANGALIA PICHA HAPA

Image