Posts

Showing posts from February 24, 2017

RAIS MSTAAFU ALHAJ ALLY HASSAN MWINYI KATIKA SHEREHE YA UHURU WA KUWAIT JIJINI DAR

Image
Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akipokea zawadi ya mchoro toka kwa Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akikata keki na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akikata keki na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni wazir...

MAHIGA ATOA SABABU ZA WATANZANIA KUFUKUZWA MSUMBIJI

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa Watanzania waliokuwa nchini Msumbiji wamefukuzwa kutokana na kukiuka taratibu na sheria za kuishi nchini humo na akataka suala hilo lisiharibu mahusiano mapana yaliyopo ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Balozi Mahiga alisema Tanzania imekuwa na ushirikiano na Msumbiji kwa muda mrefu hivyo utaratibu walioufuta wa kuwaondoa wahamiaji hao ni wa kiuungwana. Alisema jana mawaziri wa nchi 14 walianza kuwasili nchini kwa ajili ya kikao cha mawaziri ambacho Tanzania ni mwenyekiti wao, na siyo kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya Msumbiji, ila yenyewe ni nchi jirani na watazungumzia masuala ya ulinzi na usalma na ushirikiano wa nchi hizi za SADC. Alisema watu hao ambao waliingia Msumbiji bila kufuata taratibu, wakiwa huko pia wamevunja sheria za nchi hiyo kwa kujihusisha sh...

BAADHI YA VIONGOZI WAKILA KIAPO CHA UADILIFU KATIKA UTUMISHI WA UMMA.

Image
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz Mikomangwa (kushoto) akila Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz Mikomangwa akiweka saini katika Hati ya Kiapo cha Uadilifu leo jijini Dar es Salaam. Anayeshuduia kulia ni Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam. Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela akimkabidhi Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz Mikomangwa (kushoto). Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Ally Malewa(kushoto) akila Kiapo cha Uadilifu mbele ya Kamishna wa Maadili katika Sek...

SERIKALI YAWATAKA WANANCHI KUANZISHA DESTURI YA KUNUNUA KAZI ZA WASANII

Image
Serikali imewataka wananchi kuanzisha desturi ya kununua kazi za wasanii, kwakuwa ndiyo njia pekee inayoweza kuwanufaisha kwa kazi wanazozifanya.Wito huo umetolewa wiki hii na Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa tovuti a Afro Premiere, iliyoanzishwa kwa lengo la kuuza video za muziki za wasanii.Alisema mpango huo unaweza kuwa ni moja ya mikakati muhimu ya kupambana na wezi wa kazi za wasanii, kwakuwa video za muziki zitakuwa zikipatikana kwenye mtandao huo peke yake kwa kipindi maalum na hivyo kuingiza pesa zinazoenda kwa msanii, serikali na watayarishaji moja kwa moja. Pia alidai kuwa kwakuwa Afro Premiere itakuwa ikiweka nyimbo za Kiswahili zaidi, itasaidia kukikuza zaidi Kiswahili, ambacho ni cha 10 kati ya lugha elfu sita duniani na kuahidi kupitia wizara ya mambo ya nje, wizara yake itawaunganisha na Watanzania waliopo nje ya nchi. Prof Ole Gabriel amewataka wasanii w...

MAFUNZO YA UKAKAMAVU KIDATO CHA KWANZA JITEGEMEE JKT SEKONDARY YAFUNGWA RASMI JIJINI DAR

Image
Mgeni rasmi wa kufunga mafunzo ya ukakamavu kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Jitegemee Sekondari Mgulani JKT, Meja Haule (katikati), akiwa na viongozi wengine wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia ni Ofisa Tawala wa Kombania wa shule hiyo, Kepteni Zaujia Shemahonga, Msanifu wa Shule, Meja Rehema Wanjara, , Makamu Mkuu wa Shule Utawala, Kepteni Benitho Lubila na Makamu Mkuu wa Shule Taaluma, Ema Mosha. Paredi la ukakamavu na uzalendo likifanyika. Gwaride likitoa heshima mbele ya mgeni rasmi. Ndugu, wazazi na jamaa wa wanafunzi hao wakifuatilia kwa karibu shughuli hiyo. wanafunzi wa shule hiyo wakifuatilia gwaride hilo. Gwaride likiendelea. wazazi wakiwa kwenye hafla hiyo. Wimbo maalumu ukiimbwa. Kiongozi wa gwaride hilo, Pelegia Nyunga akikabidhiwa zawadi na mgeni rasmi. Francis Christopher akipewa zawadi. Mwanahawa Shabani akikabidhiwa zawadi. Salehe Hem...