Posts

Showing posts from June 1, 2014

MWANAMUZIKI SHAA AWEKA PICHA ZA UTUPU INSTAGRAM

Image
Nashindwa kufahamu kama ni ulimbukeni au ni kulewa ustaa ama kitu gani kingine, hebu fikiria katika hali hii ambayo imetokea kwa staa wa muziki nchini Tanzania Sarah Kais maarufu kama Shaa baada ya kupiga picha za utupu katika mtandao wa kijamii wa Instagram, ziko hapa. Kama unam-follow kwenye instagram @Shaa_tz basi utakuwa umesha like au kuona jinsi comment na like nyingi zinazopata picha hizi

TAIFA STARS YA SONGA MBELE YATOA SARE 2-2

Image
Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imefanikiwa kuvuka hatua ya kwanza ya michuano ya kuwania kucheza michuano ya kombe la mataifa huru ya Afrika linalotarajiwa kufanyika mwakani. Stars leo ilikuwa inacheza Zimbwabwe kwenye mchezo wa m arudiano baada ya kuwafunga Zimbwabwe 1- 0 uwanja wa taifa wiki moja iliyopita, kwenye mchezo huo Stars imefanikiwa kufuzu baada ya kulazimisha sare ya 2-2. Zimbwabwe walianza kufunga dakika ya 24, kabla ya Stars kusawazisha dakika kadhaa baadae kupitia Nadir Haroub 'Cannavaro' dakika ya 28.  Muda mchache baadae Thomas Ulimwengu aliongezea Tanzania bao la pili dakika ya 46, kabla ya dakika 10 baadae Zimbwabwe kusawazisha na kufanya matokeo 2-2. Mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho matokeo yalibaki 2-2, na sasa Tanzania wanaingia hatua ya pili ambapo watacheza na Msumbiji.

MTOTO WA PELE AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 33

Image
Edinho, mtoto wa Pele amehukumiwa kifungo cha miaka 33 jela. Kwa mujibu wa BBC, Edinho mwenye umri wa miaka 43, amepewa hukumu hiyo kwa kosa la ulanguzi wa fedha kwa ajili ya kusafirisha dawa za  kulevya. Alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005 na kutumikia kifungo jela kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya na kujihusisha na genge la wahalifu. Aliwahi kuichezea klabu ya Santos katika miaka ya 1990, kama golikipa. Kwa sasa anafanya kazi kama kocha wa makipa wa Santos. Amekiri kuwa ni 'mteja' wa dawa za kulevya, lakini amekanusha kuhusika na uuzaji wake. Anatarajiwa kukata rufaa.

TASWIRA ZA KUWASILI KWA MWILI WA MAREHEMU GEORGE TYSON KATIKA HOSPITALI YA KAIRUKI

Image
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere, akiwasili katika Hospitali ya Kairuki kusubiri mwili wa marehemu. Steve alivalia tisheti yenye ujumbe 'Why always me'. Mke wa marehemu Tyson, Beatrice Shayo akiwa na simanzi wakati akiusubiri mwili wa mumewe. Dada wa marehemu Tyson, aitwae Doreen akisubiri mwili wa kaka yake. Ni majonzi kwa kila mmoja aliyefika kuusubiri mwili wa marehemu Tyson Hospitali ya Kairuki, Mikocheni, Dar. Msanii wa filamu za Kibongo, Kelvin akihojiwa kuhusu alivyopokea taarifa za kifo cha mwongozaji filamu, George Tyson. Mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live kinachoruka kwenye runinga ya EATV, Joyce Kiria akilia kwa uchungu. Mwigizaji Aunt Ezekiel naye alikuwepo kupokea mwili wa Tyson. Wema Sepetu akihojiwa na mwanahabari wakati wa kupokea mwili wa Tyson. Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steve Nyerere akibadilishana mawazo na mmoja wa waombolezaji. Mlinzi wa mochwari katika Hospitali ya Kairuki akiusubiri mwili wa Tyson. Waombolezaji wak...

BREAKING NEWS:MTOTO ALIYEWEKWA KWENYE BOKSI MIAKA MINNE AFARIKI DUNIA

Image
Nasrah Rashid (kulia) enzi za uhai wake. Kushoto aliyekaa ni baba yake mzazi Rashid Mvungi. MTOTO Nasrah Rashid (4) aliyekuwa akitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kuugua na kupata ulemavu kwa kufungiwa kwenye boksi miaka minne amefariki dunia. Nasrah alifichwa kwenye boksi na mama yake mkubwa aitwaye Mariamu Said mkazi wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro tangu akiwa na miezi tisa baada ya mama yake mzazi kufariki. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.

BREAKING NEWZZ: MAMA ZITTO KABWE AFARIKI

Image
Mama Mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, Bi. Shida Salum enzi za uhai. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mama Mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, Bi. Shida Salum wakati alipokuwa amelazwa ICU katika Hospitali ya AMI jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Zitto Kabwe akiwa na mama yake Shida Salum enzi za uhai wake. MAMA mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, Bi. Shida Salum amefariki dunia akiwa katika Hospitali ya AMI jijini Dar es Salaam!

ANGALIA PICHA JINSI KILI TOUR ILIVYOFUNIKA NDANI YA JIJI LA MWANZA

Image
Zembwela na Dullah wakifanya yao kwenye jukwaaa ndani ya mwanza Rich Mavoko na dancers wake wakiwa back stage

Venessa Mdee Afunguka Kwanini Aliacha Kufanya Kipindi cha The One Show, Amtaja Marehemu George Tyson

Image
Venessa Mdee hajawai kusema sababu ya kuacha kufanya The One show ambayo alianza hadi ku-shoot. Hivi sasa amesema sababu hiyo akimhusisha George Tyson kama mtu aliyempa moyo kwenye maamuzi yake Soma Hapa Chini:

DIAMOND NDANI YA WASHINGTON, DC, APIGA PICHA NA MASHABI WAKE, LEO KUFANYA SHOW NEW JERSEY

Image
 Diamond Plutnumz akiongozana na wasafi pamoja na Dj Romy Jons (Dj wake) kulia wakiwa na mwenyeji wao DMK wakiwasili tayari kukutana na mashabiki wake waliofika kwenye mgahawa wa Safari, Washington, DC kumsubili na kupiga nae picha.   Diamond Plutnumz akiwa ndani ya mgahawa wa Safari na kruu wake katika picha na mashbiki waliofika kumsabai na kupiga nae picha.  Mashabiki wa Diamond wakipata ukodak moment na Diamond Plutnumz mara tu alipotua ndani ya mgahawa wa Safari siku ya Ijumaa May 30, 2014.  Shabiki akiwa bado na kiu ya kupata ukodak na Rais wa Wasfai, Diamond kulia ni DMK poromota wa msanii huyo ambaye ndie anayekimbiza sasa hivi na akiwa nominee wa MTV africa na BET award itakayofanyika nchini Marekani June 29, 2014.  Diamond akiongea jambo na Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka  Mashabiki wa Diamond Plutnumza wakipata picha ya pamoja na Rais wa Wasafi.  Mas...