Posts

Showing posts from October 10, 2013

MAZISHI YA BABA MZAZI WA MSANII WA KIZAZI KIPYA 20 PERCENT YAFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA KIMANZICHANA ... NI AIBU TUPU

Image
Abas Kinzasa kwa jina la usanii anaitwa 20 Percent akiwa kwenye majonzi baada ya kufiwa na Baba yake mzazi Mzee Kinzasa aliyefariki juzi siku ya Jumapili na kuzikwa siku ya Jumatatu kwenye kijiji cha Kimanzichana kilichopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani. Hapa ndipo alikozikwa Mzee Kinzasa baba mzazi wa 20 Percent aliyefariki siku ya jumapili na kuzikwa siku ya jumatatu kwenye kijiji cha Kimanzichana kilichopo Wilaya ya Mkuranga Msanii 20 Percent na ndugu zake wakiweka udongo kwenye kaburi la marehemu baba yake mzazi mzee Kinzasa Abas Kinzasa kwa jina usanii anaitwa 20 percent akieleza jambo kandokando ya kaburi la Baba yake mzazi Mzee Kinzasa aliyefariki siku ya jumapili na kuzikwa siku ya jumatatu kwenye kijiji cha Kimanzichana kilichopo Wilaya ya Mkuranga Marehemu mzee Kinzasa akiombewa dua baada ya kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele Hii ndio nyumba aliyoicha marehemu Mzee Kinzasa iliyoko kwenye kijiji cha ...

AGNESS MASOGANGE ATUA BONGO SHUHUDIA MWENYEWE HAPA ALIVYOPOKELEWA

Image
Kupitia Instagram jana Agnes alipost picha (hapo juu) akiwa uwanja wa ndege na kuandika “am cmng homeeeeeeeee”. Ikiwa ni wiki chache toka kesi ya video vixen Agnes Gerald a.k.a Masogange ya kutuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya kuisha kwa kulipa faini nchini Afrika Kusini na kuwa mtu huru, hatimaye jana Jumanne amerejea nyumbani Tanzania. Mwishoni mwa mwezi uliopita (September) mrembo huyo aliachiwa huru pamoja na mdogo wake Melissa Edward ambaye mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, Afrika Kusini ilimuachia huru baada ya kukosa ushahidi wa kumtia hatiani.

CHADEMA, CUF na NCCR Mageuzi wakubaliana kusitisha MAANDAMANO yao leo tarehe 10

Image
Viongozi Wakuu wa vyama vya siasa nchini Tanzania, NCCR-Mageuzi, CHADEMA na CUF wametangaza kusitisha mpango wa maandamano uliokuwa umepangwa kufanyika siku ya Alhamisi, Oktoba 10, 2013 katika maeneo ya mikoa ya Unguja, Dar es Salaam, Mbeya, Kigoma, Dodoma, Tanga, Mwanza na Arusha kwa lengo la kudai upatikanaji wa muafaka wa mchakato wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba yatakayowezesha kuundwa kwa Katiba Mpya inayokubalika na wananchi. Mwenyekiti wa CUF akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake katika ofisi za Makao Makuu ya NCCR-Mageuzi jijini Dar es Salam, Profesa Ibrahim Lipumba amesema sababu kubwa ya kusitisha mikutano iliyopangwa inatokana na kuitambua nia ya Rais Kikwete aliyoionesha katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi, ambapo alibainisha wazi kuwa atakutana na viongozi wa vyama hivyo kuzungumzia suala hilo la Muswada wa Katiba. Kutokana na nia hiyo, alisema vyama hivyo havina budi kusubiri mazungumzo na Rais Kikete yatakayotoa dira ya kitakachoendelea katika...

Mama aliyejifungua ajirusha ghorofani MUHIMBILI na kufariki dunia hapo hapo

Image
WATU wawili wameripotiwa kufariki dunia jijini Dar es Salaam katika matukio mawili tofauti akiwamo mzazi aliyejirusha kutoka ghorofani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marieth Mnangi, alisema jana kuwa mzazi huyo, Lewana Melkiory (38) mkazi wa Sinza, alijirusha kutoka wodi ya wazazi ghorofa ya pili juzi usiku na kufariki dunia papo hapo. Alisema mwanamke huyo alijifungua Oktoba Mosi na kulazwa hospitalini hapo na mtoto wake.Kamanda Marieth alisema sababu za kujirusha kwa mwanamke huyo hazijafahamika, na maiti imehifadhiwa hospitalini hapo. Katika tukio jingine, dereva wa pikipiki T 774 CKK Fekon aliyefahamika kwa jina la utani Kwea pipa, amefariki dunia baada ya kugongana uso kwa uso na gari lisilofahamika. Ajali hiyo ilitokea juzi, barabara ya Kitunda, eneo la Hali ya Hewa TANESCO. Abiria katika pikipiki hiyo, Robiso Hamazima (21) mkazi wa Ubungo, alijeruhiwa na amelazwa hospitali ya Amana. Maiti imehifadhiwa ...

Uzuri wangu upo ndani ya MAPAJA yangu na Sihangaiki na dawa za kichina kama wenzangu"..Ray C"

Image
Huyu ni Msanii mkongwe maarufu kwa jina la Ray C ambaye leo hii ameamua kuyanadi mapaja yake akidai kwamba hiyo ndo sehemu muhimu ya mwili wake... Kila mwanamke ana mvuto wake, wapo wanaojivunia nyuso zao zenye macho yaliyoumbwa yakaumbika, nyuso zisizo na chunusi wala aina yoyote ya kovu... Wapo pia wanaojivunia makalio yao na sote tumekuwa tukishuhudia jitihada mbali mbali za akinadada za kujitengenezea makalio ya bandia ( ya kichina ) ili kujiongezea mvuto kwa wanaume. Hali ni tofauti kidogo kwa msanii Ray C.Yeye anaamini kwamba mapaja ndo kila kitu na kwamba ni hicho kigezo muhimu kinachoangaliwa na wanaume wengi wa siku hizi... "Nani asiyejua kwamba kuna makalio ya kichina? Umewahi sikia wapi mapaja ya kichina? .. Haya tunayo wachache ambao tumejaliwa na muumba wetu" .Hii ni kauli ya Ray C alipokuwa akipiga stori na mpekuzi wetu. Akiongelea ku...

PICHA ZA DIAMOND NA WEMA WAKIWA NDANI ZAENDELEEA SAMBAA

Image
Utata umeendelea kuibuka kuhusu picha zinazosadikiwa ni za hivi karibuni zikimwonesha Wema Sepetu na Nasib Abdul "Diamond Platnumz" katika nyakati tofauti kwenye nchi moja huko Asia wakiwa kimahaba CHUMBANI Picha hizi zimehusishwa na usaliti wa Diamond kwa mpenziwe wa sasa aitwaye Penny, na gazeti moja la udaku lilichapisha habari kuwa wawili hao hawapo katika hali nzuri baada ya Diamond kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake, Wema. Wakati Wema akiripotiwa kuwa alikuwa China kwa ajili ya sherehe za kumbukumbu ya sikukuu yake ya kuzaliwa, Diamond aliripotiwa kipindi hicho hicho akiwa Malaysia kwa ajili ya shughuli zake za kutumbuiza na burudani. Baada ya picha hizi kuvuja,Diamond amefunguka na kujitetea kuwa eti walikuwa wana shoot movie yao mpya, lakini hembu tutumie macho kwa kufananisha hizi picha ili tuupate ukweli. Angalia picha ya juu hair style ya Diamond na mawani aliyovaa. Picha ya juu alipiga Diamond akiwa dukani huko Malaysia ...

Wasanii wa Nigeria wanavituko: Msanii mwingine wa kike apanda jukwaani akiwa hajavaa kitu ndani

Image
Ni msanii mwingine wa kinigeria ambaye kaamua kujitafutia umaruufu kwa staili ya kutovaa nguo za ndani.... Kwa mujibu wa mitandao ya kinigeria, msanii huyu ambaye ni underground anaripotiwa kunywa pombe kupita kiasi kabla ya show kuanza , hali iliyomfanya asijitambue na kuona kila kitu ni kizuri mbele ya macho yake. Baada ya show kuanza, mrembo alipanda jukwaani kama kawaida huku akiwa na kivazi kinachoziba makalio yake kwa juu tu.Ndani hakuwa na kitu.Mziki ulipokolea, kila kitu kilianikwa hadharani. <<BOFYA HAPA>>