Posts

Showing posts from July 17, 2017

MSEMAJI WA SIMBA HAJI MANARA AFUTIWA ADHABU YA TFF

Image
Haji Manara. KAMATI ya Nidhamu ya  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) , chini ya mwenyekiti wake, Tarimba Abass, leo Jumatatu imefikia uamuzi wa kumfutia adhabu  Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba ,  Haji Manara. Kamati hiyo imefikia uamuzi huo baada ya  Manara  kuomba kupitiwa upya adhabu aliyopewa hapo awali ya kufungiwa kutojihusisha na soka kwa kipindi cha miezi 12 na kulipa faini ya Sh milioni 9. Kutokana na kufutwa kwa adhabu hiyo, Manara kuanzia leo atakuwa huru kuendelea kufanya majukumu yake ya soka ndani ya Simba. Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Tarimba Abbas akizungumza na wanahabari leo mchana ikiwa ni maamuzi waliyoyafikia ya kamati ya nidhamu na kuwafungulia baadhi ya wanafamilia wa mpira waliokuwa wamefungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi. Mbali na Manara, kamati hiyo pia imewafutia adhabu Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Rukwa, Blassy Kiondo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Rukwa, James Mak

Rais Magufuli kuzindua miradi tisa ya barabara na uwanja wa ndege.

Image

DAR: Watuhumiwa 250 Mbaroni, Wamo wa Madawa ya Kulevya

Image
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum DCP, Lucas Mkondya akiwaonyesha wanahabari bangi zilizokamatwa na jeshi hilo. JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limesema kuwa limefanikiwa kuwatia nguvuni watuhumiwa 250 kwa makosa mbalimbali ya kihalifu yakiwemo ya kukutwa na madawa ya kulevya. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Lucas Mkondya ameeleza kuwa watuhumiwa hao walikamatwa kupitia msako mkali kuanzia Julai 16, hadi leo Julai 17 ambapo watuhumiwa hao walikamatwa. Mkondya amesema, miongoni mwa makosa waliyokamatwa nayo watuhumiwa hao ni pamoja na kupatikana na madaya ya kulevya, unyang’anyi wa kutumia silaha, utapeli na kucheza kamari. Aliongeza kuwa upelelezi wa makosa hayo ukikamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria. NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

JK amfuta Machozi Mwakyembe

Image
RAIS Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete amefika Nyumbani kwa Dk Harrison Mwakyembe kumfuta Machozi kutokana na Msiba wa Mke wake Linah Mwakyembe. Kikwete alifika Msibani hapo saa sita  mchana  "Mwakyembe ni rafiki yangu wa siku nyingi, hata wakati mama anaumwa aliniambia na nilienda kumjulia hali alipokuwa Muhimbili, nimtake awe mvumilivu tunajua ana majonzi msiba huu ni wetu sote," amesema. Wengine waliofika kumfariji Dk Mwakyembe ni Jaji Mstaafu Damian Lubuva, ambaye pia alimjulia hali Linah wakati akiwa hospitali. "Mwezi uliopita nilienda Aga Khan kumuona mgonjwa mwingine lakini nikakutana na Mwakyembe, akaniambia mkewe amelazwa nikaona si vibaya kwenda kumjulia hali na alikuwa anaonyesha matumaini," amesema. Wengine waliofika kumfariji Dk Mwakyembe ni Spika wa Bunge mstaafu, Anne Makinda; Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji; Waziri wa Ulinzi, Dk Hussein Mwinyi; Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga na viongozi wengine

STAA DIAMOND PLATNUMZ,BABU TALE NA MKUBWA FELLA WAKIWA MSIBANI KWA WAZIRI MWAKYEMBE

Image
Mwimbaji wa Bongofleva  Diamond Platnumz,   Mameneja wake  Said Fella  na  Babu Tale ni miongoni mwa mastaa wa Bongo waliofika nyumbani kwa Waziri wa Habari  Dr.  Mwakyembe  kutoa pole kufuatia kifo cha Mke wake  Linah George.