Waziri Mkuu: Nitahamia Dodoma Septemba Mwaka Huu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akiwasalimia na kuwashukuru mamia ya wakazi wa mji wa Dodoma mapema leo asubuhi waliojitokeza kushuhudia maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma. *Asema akishahamia, Mawaziri na Naibu Mawaziri wote wafuatie mara moja WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atahamia Dodoma ifikapo Septemba, mwaka huu kuonyesha kuwa Serikali imedhamiria kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi. Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumatatu, Julai 25, 2016) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mkoa wa Dodoma na kuwashukuru kwa ushiriki wao kwenye maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa zilizofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa, mjini Dodoma. “Jana nilimwita Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na kumwambia akamilishe matengenezo kwenye nyumba yangu kwa sababu ninataka kuhamia Dodoma ifikapo Septemba,” amesema na kushangiliwa na m...