SERIKALI YATANGAZA AJIRA KWA WALIMU WAPYA 36,071
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam KATIKA kukabiliana na uhaba wa walimu nchini serikali imetangaza kuajiri walimu wapya 36,071 ambapo watapangiwa vituo vya kazi mwezi ujao. Hatua hiyo ni mikakati ya serikali katika kukabiliana na uhaba wa walimu ambapo sasa watakuwa na upungufu wa walimu 21684 kutoka 57755 iliyokuwepo kabla ya kutanga ajira hizo mpya. Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia Elimu, Kassim Majaliwa, alisema jana kuwa walimu hao watasambazwa katika shule za msingi na sekondari nchini. Alisema taratibu zote za ajira kwa walimu hao wapya zimekamilika na kwamba mwezi ujao wote walioajiriwa watakuwa wamepangiwa vituo vyao vya kazi. Majaliwa alisema majina ya walimu wote walioajiriwa na vituo vyao vya kazi tayari kwa kuanza majukumu na serikali itaendelea kuhakikisha uhaba wa walimu nchini unakuwa historia. Hata hivyo alisema kati ya walimu hao wapya 36021 watakuwa chini ya TAMISEMI na waliobaki watapelekwa kuwa chini ya...