Posts

Showing posts from November 6, 2017

Kunyonyana ulimi au kula mate Kunasababisha kuambukiza VVU?

Image
Swali:  Je kunyonyana ulimi au kula mate kunaweza kuambukiza VVU? Jibu: Njia ya mdomo inaweza kuchangia mtu kupata VVU kama mtu atakutana na mtu mwenye VVU mwenye vidonda au michubuko mdomoni nawe pia ukawa una michubuko au vidondamdomoni, ili kuweza kupata VVU kwa njia ya mate inabidi kulambamate lita 2 jambo ambalo ni gumu.

RAIS DKT. MAGUFULI AKIFUNGUA UWANJA WA NDEGE WA BUKOBA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wa pili kutoka (kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Serikali kuashiria ufunguzi rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na viongozi hao mara baada ya ufunguzi wa rasmi wa Uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mkono na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald mara baada ya ufunguzi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Andre Bald kuas...

Wakili Msomi Atinga Mahakamani Kudai Wanaume Wafutiwe Mahari

Image
Wakili msomi nchini Zimbabwe, Bi. Priccilar Vengesai ameanzisha kesi mahakamani ya kufutilia mbali mahari zinazotolewa na wanaume pale wanapooa akidai kuwa ni mila iliyopitwa na wakati. Tokeo la picha la pete ya ndoa Wakili huyo amewasilisha malalamishi yake katika mahakama juu nchini humo akitaka kusikilizwa kwa kesi yake huku akilalamika kuwa utamaduni huo unakiuka haki za kibinaadamu. Bi. Priccilar Vengesai anaamini kuwa endapo utamaduni huo utaendelea ,familia zote za mume na mke zinatakiwa kulipa mahari kwa maslahi ya usawa wa kijinsia. Akizungumza na gazeti la serikali nchini Zimbabwe la Herald, Wakili huyo amesema kuwa anataka kuolewa upya baada ya ndoa yake ya kwanza kuvunjika kwani hakuwa na sauti ya kuhoji kiasi cha mahari iliyotolewa na kujiona kama bidhaa. “Nataka kuolewa tena sitaki kupitia kama niliyopitia kwenye ndoa yangu kwani sikushiriki katika kuuliza gharama ya mahari. Sikupewa fursa ya kuuliza kwa nini mahari ilitolewa wa...

RAIS MAGUFULI AAMURU WATATU KUCHUNGUZWA KWA KUTAKA KUIIBIA SERIKALI MABILIONI

Image
RAIS Dk. John Magufuli, ameamuru kukamatwa kwa watumishi watatu wa serikali, kwa tuhuma za kuandika madai yasiyo halali, kwa lengo la kuiibia serikali.Rais Magufuli ametoa amri hiyo wakati akizindua Uwanja wa Ndege wa Bukoba wenye urefu wa kilomita 1.5 ambapo amewataja watumishi hao kuwa ni Jackson Kaswahili Robert, Mwachano Msingwa na Gidioni Zakayo. Alifafanua kwamba, Jackson alijaza fomu zinazoonesha kwamba anaidai serikali shilingi bilioni 7.626 lakini madai hayo yalipochunguzwa, ilibainika kuwa hadai chochote.Akaongeza kwamba Mwachano yeye alijaza nyaraka zinazoonesha kwamba anaidai serikali shilingi bilioni 7.754 wakati ukweli ni kwamba anaidai shilingi milioni 2 tu huku Gidioni ZakayoAkijaza nyaraka zinazoonesha kwamba anaidai serikali shilingi milioni 104 wakati si kweli.Hawa wote pamoja na maofisa wizarani walioidhinisha malipo haya, naagiza vyombo vya dola viwashughulikie. Tumekuwa na watu ambao hawana uchungu na wengine,” alisema Rais Magufuli.

Wanachama 12 wa Chadema Wafikishwa Makamani Arusha

Image
Wanachama 12 wa Chadema mkoani Arusha wanaotuhumiwa kumshambulia mgombea udiwani wa CCM katika Kata ya Muriet, Francis Mbise wamefikishwa Mahakama ya Mwanzo ya Maromboso iliyopo jijini Arusha leo. Miongoni mwa washtakiwa hao ni Kaimu Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha, Innocent Kisanyage na mwenyekiti wa chama hicho Mtaa wa Mlimani, Yohana Gasper. Baada ya kufikishwa mahakamani wamepelekwa mahabusu wakisubiri kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka yanayowakabili

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WADAU WA ELIMU YA UFUNDI NA MAFUNZO JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa Wadau wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ulioanza leo tarehe 6 na unatarajiwa kumalizika tarehe 8 november, katika ukumbi wa APC Bunju, Jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)         Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna ya mashine ya kuchora kadi za mifumo ya umeme inavyofanya kazi na Mhandisi Vedastus Sichilima kutoka D.I.T (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)​ Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, leo amefungua Mkutano wa Kimataifa wa wadau wa elimu na mafunzo ya ufundi. Mkutano huo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hotel ya APC Bunju wilayani Kinondoni, umeandaliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa kushirikianana Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ya nchini Finland. Akihutub...

Mwanamfalme Wa Saudi Arabia Afariki Katika Ajali Ya Ndege

Image
MWANA wa mfalme  nchini Saudi, Arabia Mansour bin Muqrin,  amefariki baada ya helikopta aliyokuwa akisafiria kuanguka karibu na mpaka wa nchi hiyo na Yemen, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti. Mwana mfalme huyo,  Mansour bin Muqrin, naibu gavana wa mkoa wa Asir, alikuwa akisafiri  na maofisa kadhaa wa serikali helikopta hiyo ilipoanguka, kituo cha runinga ya Al-Ikhbariya imesema. Chanzo cha ajali hiyo hakijabainika hadi sasa. Kuna habari kwamba Saudi Arabia ilkuwa imetungua kombora la masafa marefu lililokuwa limerushwa kutoka Yemen likiwa karibu na uwanja wa ndege wa Riyadh Jumamosi. Pia, wakati wa wikiendi, watu wengi wakiwemo wana wa wafalme 11 na mawaziri wanne walikamatwa katika kampeni ya kukabiliana na rushwa ambayo inatazamwa kama njama ya kuimarisha mamlaka ya mrithi mtarajiwa wa ufalme.  Taasisi hiyo ya kukabiliana na ufisadi iliundwa na mwanamfalme wa kwanza kwenye urithi, Mohammed bin Salman. Mansour bin Muqrin, al...

SIMBA 6 WATOROKA KWENYE HIFADHI YAO WAINGIA MTAANI.

Image
Simba wapatao sita wa Mbuga ya Taifa ya nchini Nairobi wametoroka kwenye hifadhi hiyo na kuingia mjini kwenye makazi ya watu na baade kurudi wenyewe kwenye hifadhi yao.Simba hao walionekana majira ya asubuhi maeneo ya Hhospitali ya Langata wakizunguuka na baadae maeneo ya Kibera ambapo huishi watu wengi hayo yamezungumzwa na Muhudumu wa hifadhi hiyo Paul Udoto kwa mujibu wa chanzo cha habari hii. Aidha baada ya muda wahusika wa hifadhi hiyo kuona Simba hao hawapo walianza kuwafuatilia na baada ya nuda wakiwaona wakirudi wenyewe kuelekea kwenye hifadhi hiyo ambapo hakuna aliyepatikana kujeruhiwa na simba hao