Posts

Showing posts from April 27, 2015

UMESIKIA HII YA MTOTO WA MIAKA 13 KUKUTWA MTUPU USIKU AKIWANGA, UNAAMBIWA ANAFUNGUA HADI KUFULI ZA MADUKA KICHAWI

Image
Mtoto mwenye umri wa miaka 13 amekamatwa usiku akiwa uchi kwa madai kuwa alikuwa akiwanga katika duka moja lililopo kijiji cha mpunguti Mkoa wa Mbeya. Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa mtoto huyo ni mzoefu kwa kuwa wafanyabiashara wamekuwa wakipotelewa na fedha katika mazingira ya utata ambapo walitega mtego ili kubaini upotevu huo na kumbaini akiingia kwenye duka moja ambalo linadaiwa kuzindikwa. Taarifa za awali kutoka kwa wakazi wa eneo hilo walidai taarifa za mtoto huyo ambaye alikuwa anaishi na bibi yake aliyemfukuza kutokana na tuhuma za ushirikiana na kukimbilia msituni kutokana na kukosa pa kuishi. Inasemekana mtoto huyo aliishi misituni kwa zaidi ya miezi mitano ndipo aliporejea na kuolewa lakini ndoa yake haikudumu kutokana na maisha kuwa magumu na akaamua kuanza mbinu za kichawi kwa kuibia watu. Alianza kufungua kufuli za maduka kwa kutumia kidole gumba huku akiwa uchi na alinaswa na kupelekwa kwenye ofisi za kata ambapo anashikili...

INAUMA SANA MTOTO AFANYIWA BETHIDEI, AFARIKI DUNIA ILIKUWA NI BAADA YA KUKATA KEKI.

Image
Inauma sana! Mtoto mzuri wa kiume aitwaye Jumanne Mwinyimbegu, mwenye umri wa mwaka mmoja amefariki dunia ghafla muda mfupi baada ya kufanyiwa sherehe ya kutimiza mwaka mmoja ‘bethidei’. Tukio hilo la kusikitisha lilijiri nyumbani kwa wazazi wa Jumanne Mtaa wa Saadan Kata ya Mwembesongo mkoani hapa mwishoni mwa wiki iliyopita na kuibua simanzi nzito kwa kuwa alikuwa haumwi na ilikuwa muda mfupi baada ya kukata keki, kulishwa na kuimbiwa ‘happy bethidei tuyuuuuu’. Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa uchungu mama mzazi wa mtoto huyo, Khadija Salum alisema: “Inaniuma sana jamani. Jumanne ni mtoto wangu pekee ambaye ametimiza umri wa mwaka mmoja. Nikaona nimfanyie ‘bethidei’. “Niliwashirikisha majirani zangu, cha ajabu baada ya sherehe kukamilika majira ya saa 3:00 usiku mwanangu alijisikia uchomvu, nikaenda kumlaza lakini hakuamka tena. “Nimemkimbiza kwenye Zahanati ya Ngeta (Mwembesongo), nilipofika manesi walimcheki wakaniambia mbona amekufa muda mrefu, nikarudi...

KAMPUNI YA KICHINA YANASWA IKITENGENEZA CONDOM FAKE ONA HAPA HABARI KAMILI LIVE!!

Image
The demand for goods of reputable or status-oriented brands has always been high, if not always growing. This is what makes the goods vulnerable to being counterfeited. It seems that condoms are not exempt from this Police in Shanghai on Tuesday uncovered a manufacturing workshop making bogus Durex condoms which were to be sent to Kenya, reported Kenya Today . The fake condoms were reportedly sold online under well-known brands like Durex and Jissbon to Kenyan hotels. About 3 million condoms which were being sold at $0,05 each are reported to have been confiscated. In addition to being of an inferior quality, the condoms are said to contain an offensive smell, according to Chinese police. While we may be accustomed to seeing rip-offs of popular labels being sold on street corners and in some shops, condoms are obviously are different matter. This ought to be seen as a crime against humanity!

SERIKALI YAZIFUTIA USAJILI TAASISI 24 ZISIZO ZA KISERIKALI

Image
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa asasi za kiraia (NGOs) zilizoorodheshwa hapa chini zimefutiwa usajili wake kuanzia tarehe ya tangazo hili; kutokana na kukiuka matakwa ya kisheria katika utendaji kazi. Kwa tangazo hili, uhalali wa kufanya kazi kwa mashirika haya umekoma na kuendelea kufanya kazi baada ya kufutiwa usajili ni kosa la jinai. Viongozi wa NGOs tajwa wanaagizwa kurejesha vyeti vya usajili kwa Msajili ndani ya siku thelathini baada ya tangazo hili. Orodha hii inahusisha mashirika ya kimataifa yanayofanya kazi Tanzania. Orodha ya mashirika ya ndani inachambuliwa na itatangazwa muda wowote kuanzia sasa; 1. AFRICA CALL MANAGEMENT INSTITUTE (ACMI) 2. AFRICA CENTRE FOR PEACE AND DEVELOPMENT 3.AIDOS - TANZANIA 4. ASSOCIAZIONE CASAGLIA ROSETTA 5. COPE-COOPERATION DEVELOPMENT COUNTRIES 6. DAN CHURCH AID 7. DIGITAL LINKS TANZANIA 8. EKKLESIA INTERNATIONAL TANZANIA 9. FEED THE CHILDREN TANZANIA 10. GLOBAL ALLIANCE F...

TAZAMA DIAMOND NA ZARI WALIVYOJIACHIA VISIWANI ZANZIBAR

Image
Mwanamuziki Nasibu Abdul 'Diamond' akijiachia na mpenzi wake Zarinah Hassan 'The Boss Lady' Visiwani Zanzibar. Diamond akilibusu tumbo la mpenzi wake Zari ambaye ni mjamzito. Zari na Diamond wakizidi kula maisha huko Zanzibar walipokwenda kwa ajili ya shoo iliyofanyika Juni 25, mwaka huu.STAA wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul 'Diamond' na mpenzi wake Zarinah Hassan 'The Boss Lady' wamezidi kuonyesha kuwa penzi lao linazidi kuimarika baada ya Zari kuachia picha Instagram wakiwa 'close' walipokwenda Visiwani Zanzibar juzi. Wapenzi hao walikuwa Zanzibar kwa ajili ya shoo ya Diamond iliyofanyika Jumamosi (Aprili 25, mwaka huu) usiku huko Ngome Kongwe. Mojawapo ya picha za wapendanao hao imbayo imeenea mitandaoni ni ile ambayo Diamond analibusu tumbo la Zari mwenye ujauzito unaodaiwa kuwa wa staa huyo.

MASKINI WEMA SEPETU! MAMA'AKE APOTEZA UWEZO WA KUONA KWA 78%

Image
Mwandishi Wetu Pole sana mama! Staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amefunguka kuwa mama yake mzazi, Miriam Sepetu anasumbuliwa na macho ambapo madaktari wamegundua kwamba amepoteza uwezo wa kuona kwa asilimia sabini na tano (75%). Kwa mujibu wa Wema, aliamua kumpeleka mzazi wake huyo hospitalini (hakuitaja) ndipo alipohakikishiwa tatizo hilo ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu. “Kumnusuru mama yangu asipate upofu wa moja kwa moja inabidi afanyiwe operesheni ya macho,” alisema Wema kwa huzuni kwa kuwa hakuna kama mama.