EVENTS


Faida zitokanazo na kucheka pekee


Bila shaka umewahinkusikia mtu akisema, wach nicheke niongoze siku za kuishi. Kama umewahi kusikia nataka nikuongezee kitu ya kwamba wataalam wa saikolojia wanasema kuwa kucheka au kufurahi ni moja ya tiba kwa afya ambayo huifanya miili yetu kubaki na afya bora zaidi.

Naomba leo nikwambie haya mambo kadhaa ambayo utayapata endapo utakuwa ni mtu wa kucheka na kufurahi.

1. Kwanza kabisa kitendo cha kucheka au kufurahi husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongo wa mawazo na kumfanya mhusika kuwa vizuri kiakili.

2. Husaidia kuimarisha afya ya mapafu
Unapocheka husaidia mapafu yako kutanuka na kuingiza ndani hewa ya safi yaani oxygen. Hivyo unapocheka zaidi tambua kuwa unasaidia kiwango cha hewa kuingia cha kutosha ndani ya mwili na kusaidia damu kusambaa vyema mwilini.

3. Husaidia kuboresha utendaji kazi wa moyo
Kitendo cha kucheka au kufurahi husaidia kukuweka mbali dhidi ya shinikizo la damu la kushuka, kwa sababu husaidia kuongeza mzunguko wa damu mwilini na pia kusaidia mishipa ya damu kutenda kazi vizuri.

4.Huboresha kinga za mwili
Kucheka ni muhimu kwani husaidia kuongeza homoni za hisia ndani ya mwili. Kutokana na mabadiliko hayo huenda.

Hizo ni faida chache kati ya nyingi ambazo mtu akiwa nazo sinamsaidia pia hata kuishi miaka mingi.
...............................................................................................................................................................


Alichosema Wema Sepetu baada ya Nduguye kudaiwa kupigwa na Polisi

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ametoa yake ya moyoni na kutoa tuhuma kwa jeshi la polisi nchini kufuatia baadhi ya polisi kumpiga ndugu yake ambaye juzi alikwenda naye mahakamani kusubiri kesi ya Tundu Lissu.

Wema Sepetu anasema kuwa ndugu yake huyo kwa sasa anapatiwa matibabu hospitalini kufuatia kipigo alichopata kutoka kwa polisi hao kwa kile anachosema kuwa kijana huyo alipigwa kufuatia kupita katika mlango wa mahakama.

"Ninachojua mimi ni kwamba binadamu ana haki ya kwenda mahakamani kusikiliza kesi ya ndugu yake... Imeniuma sana kilichomtokea kaka yangu jana, Only now nakuja kujua kwamba alichukuliwa na polisi wakaenda kumpiga mpaka sasa yupo hospitali amelazwa. Kosa lake ni kupita pale mlango wa mahakamani na akasema kabisa yupo pamoja na mimi na mama yangu" alisema Wema Sepetu

Hata hivyo Wema Sepetu anasema wakati anasubiri kesi ya Tundu Lissu juzi  mahakamani alikuja kuitwa na polisi na kuambiwa kuwa aondoke eneo hilo na arudi nyumbani kwake

"Maana jana tulivyokuwa tumekaa tunasubiri kesi ya Mh. Tundu Lissu itajwe, Nilikuja kuitwa walitaka niondoke eneo hilo na nirudi nyumbani... Nilikuwa mkali kidogo, wakanijia na huyo kaka yangu ambaye alisema kuwa yupo pamoja na mimi" alisema Wema Sepetu

Mbali na hilo Wema Sepetu alisema kuwa namna ambavyo jeshi la polisi linafanya si jambo zuri na kusema matendo ya namna hii yanaweza kuleta shida au matatizo siku za usoni

Mwishoni mwa mwezi wa pili mwaka huu msanii Wema Sepetu alifanya maamuzi magumu na kuamua kuhama chama kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya msanii huyo kutuhumiwa na serikali kuwa anajihusisha na Uuzaji na matumizi ya madawa ya kulevya ambapo mpaka sasa bado kesi yake inaendelea katika Mahakama Kuu Tanzania (KISUTU)

 

 .................................................................................

MATUKIO YA KIKAO CHA 11 MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO

 Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongoza kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017.
 Naibu Waziri wa Ujenzi uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Nyonyani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017. 
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017. 
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017. 
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017. 
Mbunge wa Viti Maalum Morogoro (CCM) Mhe Dkt Christina Ishengoma akiuliza swali katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017. 
Mbunge wa Songwe (CCM) Mhe. Philipo Augustino Mulogo akiuliza swali katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017. 
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017.
Mbunge wa Kilindi (CCM) Mhe Omari Mohamed Kigua akiuliza swali katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017. 
Wabunge wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017. 
Baadhi ya wazee walioshiriki katika kuchanganya mchanga wakati wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wakifuatilia shughuli za Bunge katika katika kikao cha kumi na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 24, 2017. Picha na Raymond Mushumbusi, Dodoma.

Mambo Si Mambo..Kuelekea Vita na Korea Kaskazini..Marekani Waamua Kutumia Helment Hizi Ghali Zaidi Duniani..Moja Inauzwa Milioni 900..!!!

Marubani wanaotumia ndege za kivita za Marekani F-35 stealth fighter watakuwa wakitumia helmet ghali zani duniani. 
Kupitia helmet hii, rubani ataona kila kitu cha dunia kinachoonwa na camera za ndege.
Bei ya helmet moja ni dola za Marekani 400,000 sawasawa na milioni 900 za Kitanzania.

 ...................................................................................

Mechi kati ya Senegal na Ivory Coast yavunjika kutokana na vurugu za mashabiki

 Mechi ya kirafiki kati ya Ivory Coast na Senegal ilisimamishwa wakati mashabiki waliingia uwanjani mjini Paris.

Timu hizo kutoka Afrika zilikuwa sare ya bao moja dakika ya 88, wakati mashabiki wachache waliingia uwanjani huku mmoja akionekana akimrukia mchezaji wa Senegal Lamine Gassama.

Wachezaji walitoka kutoka uwanajania na refa Tony Chapron akaamua kusimamisha mechi hiyo.
Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane alikuwa ameipa Senegal bao la kwanza mnamo kipindi cha pili, lakini Bi Gohi Cyriac akasawazisha dakika tatu baaadaye.

Mwandishi wa habari wa shirika la L'Equipe Herve ambaye alikuwa uwanjani wakati huo aliambia BBC kuwa kisa hicho kingekuw kibaya.

"Sitaweza kusema kuwa watu hao walikuwa na ghasia, lakini ni kama walikuwa wanajaribu kuwafikia wachezaji," mwandishi huyo aliongeza.

Hii ndiyo mara ya pili ndani ya miaka mitano mechi kati ya chi hizo imesimamishwa kutokana na vurugu za mashabiki.

...................................................................................................................................................................








Mwenyekiti wa kitongoji auawa kwa Bastola

Mwenyekiti wa kitongoji cha Kifuru, kijiji cha Ikwiriri, wilayani Rufiji,  Hemed Abdallah Njiwa ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake.
Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Ikwiriri, Iddy Malinda amethibitisha mwili wa mwenyekiti huyo kufikishwa kituoni hapo ukiwa na jeraha kubwa mgongoni lililotokana na risasi aliyopigwa kifuani, upande wa moyo.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Njwayo pia amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema watu wasiojulikana walifika nyumbani kwa mwenyekiti huyo kisha kumpiga risasi na kutokomea kusikojulikana.
Habari zaidi zinadai watu hao baada ya kutekeleza mauaji hayo hawakuchukua kitu chochote kile

 

................................................................................................................

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka Makao Makuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Dodoma ambapo Mkutano Mkuu unaendelea ni kwamba, baadhi ya wananchama wa CCM wamevuliwa uanachama huku wengine wakipewa onyo kali kwa sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni usaliti katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Miongoni wa waliofukuzwa uanachama ni pamoja na mwanachama mkongwe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Sophia Simba huku Adam Kimbisa akisamehewa na Emmanuel Nchimbi akipewa onyo kali. Onyo kali alilopewa Nchimbi ina maana kuwa hatoruhusiwa kugombea nafasi yoyote kwa miaka minne.
Kufuatia maamuzi hayo, Sophia Simba amepoteza rasmi nafasi yake ya Ubunge wa Viti maalumu na Uenyekiti wa UWT kwani nafasi hizo zinahitaji mtu ambaye ni mwanachama wa chama aweze kuzishika. Hivyo, CCM italazimika kupeleka jina jingine Tume ya Uchaguzi kuteua mbunge wa kuziba nafasi ya Sophia, huku nafasi yake ya Uenyekiti UWT ikisubiri uchaguzi baadae mwaka huu.
Wengine waliovuliwa uanachama ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Madenge, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Assa Simba, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Christopher Sanya, Mwenyekiti Mkoa wa Shinyanga Ernest Kwirasa, Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa, Nesta Msabatavunga, Mjumbe wa Halamshauri Kuu (NEC) ya CCM, Ali Sumaye, Mjumbe wa NEC Arumeru, Mathias Manga.
Pia, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Longido Leiza amefukuzwa uanachama pamoja na Mwenyekiti wa CCM Arusha Mjini, Saileli Molleli, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo, Omary Hawadhi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Muleba, Mwenyekiti wa CCM Babati, Mwenyekiti wa CCM Wilaya Bunda, Mjumbe wa NEC Gureta.
Waliopewa onyo kali kwa makosa mbalimbali ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini, Ahmed Kiponza ambaye amepewa onyo kali na kuondolewa madarakani, Mjumbe wa NEC Mkoa wa Singida, Hassa Mzaha, Mwenyekiti wa UWT Gezabulu, Mjumbe wa NEC Kilwa, Ali Mchumo na Mjumbe wa NEC Tunduru, Cheif Kalolo ambao wamevuliwa ujumbe huo na kupewa onyo kali

..................................................................................

MREMBO LULU DIVA AWATAJA WASANII WATANO ANAOWAKUBALI ZAIDI BONGO

Lulu Diva ambaye ni msanii mpya kwenye ramani ya muziki wa Bongo Flava amewataja wasanii watano wa muziki huo anaowakubali.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio Jumatatu hii, muimbaji huyo amewataja wasanii hao kuwa ni pamaoja na Vanessa Mdee, Belle 9, Dogo Janja, Madee na Barnaba.
Diva ameongeza kuwa baada ya kuingia kwenye tasnia ya muziki hataacha kufanya kazi hiyo mpaka mwisho wa uhai wake huku. Kwa sasa msanii huyo ameachia wimbo wake wa pili ‘Usimwache’ ambao video yake imeongozwa na Nicrux kutoka Afrika Kusini.

...................................................................................

RAIS DKT. MAGUFULI AMUAPISHA KAMISHNA JENERALI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI PAMOJA NA MABALOZI WANNE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Thobias Andengenye kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Pindi Chana kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Silima Kombo Haji kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sudani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Abdallah Kilima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Matilda Masuka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akila kiapo cha Ahadi ya Uadilifu pamoja na Mabalozi Pindi Chana, Balozi Silima Kombo Haji, Abdallah Kilima pamoja na Balozi Matilda Masuka mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi (wapili kutoka kushoto), Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba(Wakwanza kulia) , Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Hamad Masauni (Wakwanza kushoto) pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye(Watatu kutoka kushoto waliosimama mstari wa nyuma) na Mabalozi Pindi Chana(Wakwanza kulia walisimama mstari wa nyuma ) , Balozi Matilda Masuka(Wapili kutoka kulia waliosimama mstari wa nyuma), Balozi Abdallah Kilima(Wapili kutoka kushoto mstari wa nyuma) na Balozi Silima Kombo Haji (Wakwanza kushoto waliosimama) mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

................................................................................

TAZAMA PICHA ZA HARUSI YA MCHEKESHAJI MASELE CHAPOMBE

 BI Specioza Malick  mke wa msanii wa vichekesho nchini aliyejipatia umaarufu mkubwa kwa mtindo wake wa kuchekesha, Chrispine Lyogello ‘Masele Chapombe’,  ni vyema akajitayarisha kucheka na kuvunjika mbavu kutokana na sanaa hiyo ambayo mumewe anaiweza ilivyo.
 Mrembo huyo, aliyefunga ndoa na msanii huyo mwezi huu wa Januari,  ameshauriwa na mashabiki wa sanaa ya mumewe ajitayarishe kucheka zaidi na wakati huohuo awe na ubavu wa kutenganisha kazi ya Masele na maisha yake halisi.
“Mke wa Masele ajiandae kucheka mpaka kuumwa mbavu siku Masele akiamua kumletea nyumbani vituo anavyofanya kwenye televisheni nyumbani.   Bi Specioza ajiandae kuwa maarufu kwani kwa sasa ameungana mwili mmoja na mtu maarufu nchini,” alisema shabiki mmoja aliyejitambulisha kama Bondi Masaba wa jijini Dar es Salaam.


Ndoa ya wawili hao ilifungwa katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Consolata lililopo Mbezi-Makabe jijini Dar es Salaam.


















  ..............................................................................

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA WABUNGE MSIBA WA MHE. TAHIR


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na wabunge wakiwa wamesimama kimya kwa dakikika moja kwa heshima ya mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. Hafidh alifariki dunia usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mbunge wa Dimai Hafidh Ally Tahir, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Spika wa Bunge, Job Ndugai akitoa heshima za mwisho kwa mbunge wa Dimani, marehemu Hafidh Ally Tahir kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 11, 2016. Mbunge huyo alifariki dunia mjijini Dodoma usiku wa kuamkia leo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (wapili kulia) na Katibu wa Bunge, Dkt.Thomas Kashililah wakisubiri kupokea mwili wa Mbunge wa Dimani, marehemu Hafidh Ally Tahir kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma ambako ulisafirishwa kwenda Zanzibar kwa Mazishi Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai na Kiongozi wa Upinzania bungeni, Freeman Mbowe (kulia) wakishuhudia wakati mwili wa mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir ukipandishwa kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa Dodoma ili kusafirishwe kwenda Zanzibar kwa mazishi Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza wabunge kuuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Dimani, Zanzibar Mheshimiwa Hafidh Ally Tahir.

Bw. Tahir amefariki saa 9 alfajiri ya kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na mwili wake kuagwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar kwa mazishi.

Akizungumza katika tukio hilo, Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, familia ya marehemu na wabunge wote.“Tumepokea taarifa za msiba huu kwa mshtuko mkubwa. Leo tupo katika wakati mgumu sana. Tumeondokewa na viongozi wengi,” amesema.

Amesema wafiwa wanatakiwa kuishi kwa upendo. “Tumuombee marehemu, tuiombee familia iwe na moyo wa utulivu katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.”

Bw. Hafidh alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta.Enzi ya uhai wake, alishiriki kikamilifu katika masuala ya michezo; alikuwa mwamuzi wa soka mwenye beji ya FIFA na kocha msaidiizi wa timu ya soka ya Bunge.

Hadi jana, Bw. Hafidh alishiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa kupata viongozi wa Tawi la Umoja wa Wabunge WanaYanga mjini Dodoma ambapo yeye alichaguliwa kuwa Katibu.




IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, NOVEMBA 11, 2016.

..................................................................................

 Anti-Trump Waanzisha Vurugu na Kuandamana Kupinga Matoke

anti-trump-1
MAREKANI: Watu watano wamejeruhiwa kwa risasi kufuatia maandamano yanayoendelea katika majimbo ya , Oakland, New York, Los Angeles, New Orleans na Washington DC yakipinga ushindi wa Donald Trump.anti-trump-25
Licha ya Rais Obama kuhimiza umoja na Bi Clinton kuwaambia wafuasi wake kwamba Bw Trump anafaa kupewa “nafasi ya kuongoza”, ushindi wake bado umeendelea kuzua maandamano katika miji na majimbo kadha Marekani.
anti-trump-2Mamia ya waandamanaji wanaompinga Trump walikusanyika nje ya jumba kuu la Bw Trump, Trump Tower eneo la Manhattan jijini New York Jumatano jioni, wakibeba mabango yaliyokuwa na ujumbe “Not my president” (Si Rais wangu), pamoja na mabango mengine.
anti-trump-3Polisi hapo awali waliweka vizuizi vya saruji pamoja na kuchukua hatua nyingine za kiusalama nje ya jumba hilo refu linalopatikana barabara ya 5th Avenue, jumba ambalo huenda likawa makao makuu ya Bw Trump wakati wa kipindi cha mpito kabla yake kuingia White House.
  anti-trump-4
Kuliripotiwa pia taarifa za waandamanaji kuziba lango la kuingia jumba la Trump Tower mjini Chicago Jumatano jioni, wakiimba: “No Trump, No KKK, No Fascists USA” (Hatumtaki Trump, Hatutaki KKK, Hatutaki Wafashi Marekani) na “Not my president!” (Si Rais wangu).anti-trump-5
Mjini Oakland, California, na Portland, Oregon, waandamanaji waliteketeza bendera za Marekani.
 anti-trump-6
akati wa hotuba yake baada ya kutangazwa mshindi mapema Jumatano, Bw Trump aliahidi kuponya vidonda vya migawanyiko, baada ya uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali, na kuahidi kwamba atakuwa “rais wa Wamarekani wote”.
anti-trump-7Msemaji wa White House Josh Earnest amesisitiza kwamba Bw Obama atakuwa na uwazi kuhusu kuhakikisha shughuli laini ya mpito atakapokutana na Bw Trump, ingawa aliongeza kwamba: “Sijasema kwamba utakuwa mkutano rahisi.”
anti-trump-8Rais huyo mteule atasindikizwa kwenda White House Alhamisi na mkewe, Melania, ambaye atakutana na Mke wa Obama, Michelle.
  anti-trump-9
Bw Obama, aliyempongeza mrithi huyo wake kwa njia ya simu mapema Jumatano, alisema si siri kwamba yeye na Bw Trump wana tofauti nyingi.
anti-trump-10Lakini aliongeza kwamba wanataka kuhakikisha wanalinda maslahi ya taifa na kwamba alitiwa moyo na yale Bw Trump alikuwa amesema usiku uliotangulia.
anti-trump-11Kundi la kushughulikia shughuli ya mpito la Bw Trump litaongozwa na Chris Christie, gavana wa New Jersey, na lina wiki 10 kukamilisha maandalizi hayo.
anti-trump-12Rais huyo mteule, ambaye hajawahi kuhudumu katika wadhifa wowote wa kuchaguliwa au kuteuliwa serikalini, amesema kipaumbele chake kitakuwa kufufua na kuimarisha miundo mbinu ya nchi hiyo pamoja na kukuza ukuaji wa uchumi wa taifa hilo maradufu.
anti-trump-13Mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha Republican Reince Priebus alisema: “Donald Trump anachukulia hili kwa uzito sana,” na kuongeza kwamba mfanya biashara huyo tajiri atatumia uwezo wake wa kutetea na kufanikisha mikataba ya kibiashara kuhakikisha mambo mema “yanatendeka kwa Wamarekani” haraka iwezekanavyo.
    anti-trump-14
Kama Rais mteule, Bw Trump ana haki ya kupokea taarifa za kila siku za ujasusi sawa na Rais Obama, ambazo ni pamoja na habari kuhusu operesheni za kisiri za Marekani pamoja na habari za kijasusi zinazokusanywa na mawakala 17 wa ujasusi za Marekani.
anti-trump-15Bw Trump na kundi lake wanaaminika kuwa tayari kujaza nafasi kuu za usalama wa taifa haraka iwezekanavyo watakapoingia madarakani.anti-trump-21
Lakini haijabainika nani atakuwa kwenye baraza lake la mawaziri au atakayejaza nyadhifa kuu wakati wa utawala wake kama vile mkuu wa majeshi.
  anti-trump-22
Kunao wanaotarajiwa kupewa nyadhifa kuu wakiwemo Christie, spika wa zamani wa bunge Newt Gingrich na meya wa zamani wa New York Rudy Giuliani, mmoja wa washauri wakuu wa Bw Trump ambaye wengi wanasema huenda akafanywa mwanasheria mkuu au mshauri mkuu wa masuala ya usalama wa taifa.anti-trump-23
Baada ya kupata hasara kubwa kutokana na ushindi wa kushangaza wa Bw Trump, masoko ya hisa yameanza kuimarika.
 anti-trump-24  anti-trump-27anti-trump-26anti-trump-38anti-trump-37anti-trump-36anti-trump-35anti-trump-34anti-trump-33anti-trump-32anti-trump-31anti-trump-30anti-trump-29anti-trump-28anti-trump-27anti-trump-25anti-trump-24anti-trump-23anti-trump-22anti-trump-21anti-trump-15anti-trump-14anti-trump-13anti-trump-12anti-trump-11anti-trump-10anti-trump-9anti-trump-8anti-trump-7anti-trump-6anti-trump-5anti-trump-4anti-trump-3anti-trump-2anti-trump-1 anti-trump-28 anti-trump-29 anti-trump-30 anti-trump-31 anti-trump-32 anti-trump-33 anti-trump-34 anti-trump-35 anti-trump-36 anti-trump-37 anti-trump-38 anti-trump-26
Tupia Comment Yako Hapa

................................................................................

Mbunge Sadifa Afunguka Ishu ya Ulevi


sadifa-6NA IMELDA MTEMA | RISASI JUMAMOSI: WIKI hii tumefunga safari mpaka visiwani Zanzibar, ambapo imeenda kuyadadavua maisha halisi ya mbunge wa Donge na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM), Sadifa Juma.
sadifa-5Sadifa akiwa na familia yake.
Mbunge huyo mwenye umri wa miaka 35, anaishi Uwanja wa Ndege visiwani humo akiwa na mkewe kipenzi aitwaye Salma pamoja na watoto wake wawili ambao ni  mapacha waitwao Sammy na Sameer (2). Bila hiyana mbunge huyo alianza kuelezea maisha yake ya kila siku nje ya siasa. Ungana nami hapa chini kwa kujua mengi zaidi:
sadifa-4Anapata muda wa kukaa na familia yake kutokana na kazi yake ya siasa?
“Kiukweli kabisa muda wa kukaa na familia yangu ni mdogo sana mara nyingi nakuwa kwenye kazi na kama kukaa nayo ni muda mchache sana lakini kwa sababu ni kazi inabidi iwe hivyo maana sina namna nyingine.
sadifa-3
Mke hapati shida kutokana na muda wake mdogo kwa familia?
“Mke wangu niko naye sasa miaka minne  lazima tu atakuwa amezoea na anajua taratibu zangu, hana shida japokuwa najua kabisa kuna wakati anapokosa uwepo wangu ananimisi na hata mimi kuna kipindi naikumbuka sana familia yangu.
sadifa-2…Akiwa na Wananchi jimboni kwake.
Nini anachopenda anapokuwa nyumbani kwake?
Kutokana na kutokuwa muda mwingi na familia yangu ninapokuwa nyumbani muda mwingi natumia kucheza na wanangu na kukaa na mke wangu kujadili vitu mbalimbali vya maisha yetu.
sadifa-1Ni chakula gani anapendelea kula anapokuwa nyumbani kwake?
“Mimi jiko la jeshi bwana sichagui chakula, chochote nakula mradi tu kisiwe na sumu lakini sina tabia ya kutaka hiki na hiki sikitaki, vyote nakula.
akiwa-na-wapigakura-wake-jimboniAnazungumziaje wanaosema yeye ni mlevi?
“Ndio mimi ni mlevi wa mafanikio ya jimbo langu na si vinginevyo.
akitoa-misaada-jimboniAnamsaidia mkewe kupika, kufua?
“Dooh sitaki kudanganya kabisa mimi sijawahi kuingia kupika au kufua kwa sababu hata mke wangu mwenyewe hafanyi hivyo vitu, wapo watu wanaomsaidia lakini kama siku nitakuwa peke yangu kabisa hakuna mtu, naweza kufanya hivyo vitu.
akikagua-mradi-wa-umeme-jimboni-kwakeVipi kuhusu kudaiwa ni mkali kupitiliza?
Hapana ukali wa nini sasa jamani ndio maana nasema kuwa mtu anaweza kutafsiri tofauti mimi sina ukali wowote zaidi zaidi muda wote ni kufurahi na watoto wangu na ndio maana unaona kutwa hawawezi kubanduka wakiniona sehemu.
akila-fenesi-jimboni-kwakeAkioa wake wawili ataweza kugawa upendo wake?
Unajua ni hivi hata kabla ya kuoa unashauriwa kuwa kama huwezi kuhudumia mke utakayemuongeza ni bora uwe na mmoja hivyo unapoamua kuoa mke mwingine ni lazima chochote anachopata mwenzake naye apate na upendo uwe hivyohivyo hivyo ikitokea nimeoa wa pili lazima nitaweza kumhudumia.
akila-chakula-na-mkeweAnapendelea mavazi gani zaidi nyumbani?
“Kama unavyoniona hapa mimi bado ni kijana kabisa napendelea zaidi mavazi ya vijana kama tisheti na jinzi naona nikivaa ndio vinanitoa zaidi.
Nini anachokitamani katika maisha yake ya kila siku?     
Natamani sana amani ndani ya familia yangu na pia natamani pia kila kitu ambacho niliwahaidi wananchi wa jimbo langu nikitimize kwa wakati kwa maana hata muda wangu ukiisha nijue kuna kitu nilikifanya katika jimbo langu.”





















 .........................................................................................................

Mfalme Wa Jordan Azuru Kenya, Ashuhudia Mazoezi Ya Kijeshi

kenyatta-force-4Mfalme wa Jordan, King Abdullah wa II akisalimiana na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mapema leo.
kenyatta-force-5…Akisalimiana na viongozi wa ngazi za juu wa jeshi la Kenya (KDF).
kenyatta-force-6…Akisaini kitabu cha wageni.
kenyatta-force-7…Akiteta jambo na mwenyeji wake Rais Kenyatta.
kenyatta-force-9Mfalme Abdullah II akizungumza na wanajeshi kwenye hafla hiyo.
kenyatta-force-13Kiongozi wa ngazi za juu wa KDF akizungumza mbele ya Mfalme Abdullah II.
kenyatta-force-2Mfalme Abdullah II akiteta jambo kabla ya kuanza kwa mazoezi ya kijeshi.
kenyatta-force-11…wakishuhudia mazoezi hayo ya kijeshi.
kenyatta-force-1…mazoezi ya kijeshi yakiendelea.
kenyatta-force-10Helikopta ya kijeshi ikiwa katika mazoezi hayo.
kenyatta-force-12kenyatta-force-12Viongozi hao wakiteta jambo huku mazoezi ya kijeshi yakiendelea.kenyatta-force-8Viongozi hao wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa shughuli hiyo.
NAIROBI KENYA: Mfalme Abdullah wa II  wa nchi ya Jordan leo amewasili nchini Kenya na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta kwenye Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyetta.
Baada ya kuwasili nchini humo mfalme huyo ameshuhudia utiaji saini wa mkataba wa kusaidiana kijeshi kati ya mataifa hayo mawili ambapo watakuwa wakibadilishana ujuzi kuhusu namna ya kupambana na suala la ugaidi kwenye nchi zao.
Majeshi ya KDF na Royal Jordanian Armed Forces kwa pamoja yamefanya mazoezi na kushuhudiwa na viongozi hao kwenye eneo la mazoezi ya kijsehi ya KDF.
Nchi zote mbili zimekumbana na matukio ya kigaidi miaka ya hivi karibuni na kupitia mkataba huu mataifa hayo yamekubaliana kwa pamoja kusaidiana kupambana na masuala ya kigaidi.
Mfalme Abdullah II amerejea nchini kwake baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo.
Na Leonard Msigwa/GPL

.......................................................................................................................................................
Fiesta Yawapagawisha Wabunge Na Mawaziri Dodoma
 jux-vanesa-001Mwanamuziki Vanessa na Jux wakitumbuiza kwenye tamasha hilo.wabunge-001Baadhi ya waheshimiwa wabunge waliohudhuria tamasha hilo akiwemo Profesa Maji Marefu (wa pili kulia), Venance Mwamoto (wa kwanza kulia) na William Ngeleja (katikati).
img_0697-001Mheshimiwa Waziri Nape Nnauye akiwa na Naibu Spika Dkt. Tulia na Waziri January Makamba.
weusi-001Kundi la weusi likitumbuiza jukwaani kwenye tamasha hilo lililohudhuriwa na mashabiki wengi.
adam-mchomvu-001Mwanamuziki Adam Mchomvu akitumbuiza mbele ya mashabiki lukuki ndani ya Uwanja wa Jamhuri.
b12-adam-001 belle-9-001Mwanamuziki Belle 9 naye alikuwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza kwenye tamasha hilo, usiku wa kuamkia leo.darasa-001Mwanamuziki Darasa akitumbuiza mbele ya mashabiki.darasaaaaaa-001Mwanamuziki Darasa akitumbuiza mbele ya mashabiki.
fiesta-1-001Baraka The Prince akitumbuiza usiku wa kuamkia leo.fiesta-2-001Sehemu ya umati mkubwa wa mashabiki waliohudhuria tamasha hilo kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma, usiku wa kuamkia leo. fiesta-4-001Mwanamuziki Jux akionesha madoido ya kucheza na jukwaa na mpenzi wake ambaye pia ni mwanamuziki Vanessa Mdee.img_0321-001  sehemu ya mashabiki ambao walifika mapema uwanjani hapo kushuhudia tamasha hilo.img_0335-001
Mmoja wa mashabiki aliyejishindia moja ya zawadi (T-shirt) kutoka kwa waandaaji wa tamasha hilo.
DODOMA, Usiku wa kuamkia jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kulifanyika tamasha la Fiesta ambako mamia wa wakazi wa manispaa ya Dodoma na vitongoji vya jirani walihudhuria onesho hilo wakiwemo pia baadhi ya waheshimiwa wabunge na mawaziri wa serikali ya tano wakiongozwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mheshimiwa Nape Nnauye.
Baadhi ya waheshimiwa wabunge waliohudhuria tamasha hilo ni pamoja na William Ngeleja, Steven Ngonyani maarufu kwa jina la Profesa Maji Marefu, Venance Mwamoto pia alikuwepo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Attickson na Waziri January Makamba.
Tamasha hilo lilivunja rekodi baada ya kuhudhuriwa na mashabiki wengi na kuacha historia ndani ya viunga hivyo yalipo makao makuu ya nchi yetu.
Wasanii wote walioshiriki kwenye tamasha hilo walifanya ‘show’ kali iliyowapagawisha mashabiki wao na kufanya tamasha hilo liwe la kipekee.
Imeandaliwa na Leonard Msigwa/GPL.
 

........................................................................................................

Hali Ilivyokuwa Wakati wa Kupatwa kwa Jua Rujewa

Solar Eclipse (4)
Jua lilivyokuwa likionekana kupitia miwani maalum ya kuchuja mionzi ya jua mjini Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya leo.
Solar Eclipse (1)
Raia wa nchi mbalimbali wakishuhudia kupatwa kwa jua kwa kutumia vifaa maalum vya kuchuja mionzi ya jua katika mji wa Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya leo.
Solar Eclipse (2)
Baadhi ya wananchi wakishuhudia kupatwa kwa jua katika mji wa Rujewa wilayani Mbarali, mkoani Mbeya.
Solar Eclipse (3)
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa wakishuhudia kupatwa kwa jua katika mji wa Rujewa wilayani Mbarali mkoani Mbeya leo, jua lilipatwa kuanzia saa 4:15 hadi saa 7:00.

 .............................................................................................................

DC Atoa Mwezi 1 Waliovamia Hifadhi Kuhama

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu akimsikiliza Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaugere, Beatus Kapatya akitoa taarifa juu ya kusimama kwa ujenzi wa zahanati.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jumanne Mtaturu.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaugeri wakati akitoa maelezo kwenye kikao cha serikali ya kijiji.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali wakati wa ziara yake wilayani humo.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaugere, Beatus Kapatya akitoa ufafanuzi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Jumanne Mtaturu.
Umakini wa wananchi ukiwa umetawala wakati wa mkutano wa kijiji, wilayani Ikungi.
Na Mathias Canal, Singida
Serikali ilitangaza eneo la Hifadhi ya msitu wa wananchi waliomo ndani mwaka 2003 ambao kutangazwa huko kuliashiria wananchi kuhama katika maeneo hayo ili kutoa fursa kwa serikali kusimamia kwa karibu eneo hilo lakini wananchi hao mpaka sasa hawajahama kwa kukaidi agizo hilo.
Jambo hili limemsukuma Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kufanya ziara na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo kwa lengo la kuwaelemisha juu ya uvunjaji sheria za nchi kwa kuendelea kusalia katika maeneo ambao wametakiwa kuhama jambo ambalo kama watashindwa
kulitekeleza serikali itawatoa kwa nguvu kwani kwa kiasi kikubwa wanaharibu mazingira.Akizungumza na Wananchi hao katika Kijiji cha Kaugeri Kata ya Mwaru Wilayani hapa Dc Mtaturu ametoa mwezi mmoja kwa wananchi hao kuhama haraka iwezekanavyo ili kupisha eneo hilo la Hifadhi ya msitu kufanya Kazi iliyokusudiwa kwa zaidi ya miaka kumi sasa.Mtaturu amesema kuwa Kwa mujibu wa sheria Kijiji kinapaswa kutoa Ardhi hekari zisizozidi hamsini kwa mwekezaji lakini uongozi wa Kijiji hicho umegawa kwa mwekezaji hekta 150 hadi 200 kinyume kabisa na taratibu za kiutendaji ukiwa ni pamoja na kuingia mikataba ya kinyonyaji.Pamoja na hayo pia viongozi hao wametoa Ardhi hiyo bila kushirikisha wananchi jambo ambalo limeibua hisia Kali kwa wananchi ambao wanatambua uporwaji huo wa maeneo yao. Kufuatia kadhia hiyo ya viongozi hao kugawaji Ardhi kinyume na taratibu Dc Mtaturu amewaweka lumande Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaugeri Mange Nkuba, Aliyekuwa Kaimu Afisa Mtendaji Laurent Bomba, na mjumbe wa serikali ya Kijiji Paul Kilo huku Amani Clement ambaye alitoweka kabla Ya mkutano kumalizika anaendelea kutafutwa mpaka apatikane.
Katika hatua nyingine Dc Mtaturu ameagiza mkandarasi Samwel John kukamatwa na kuhojiwa kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji tangu Mwaka 2013 ambapo tayari alishapewa kitita cha shilingi milioni 19 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.
Hata hivyo pamoja na mkandarasi kukabidhiwa fedha hizo alianza ujenzi lakini jengo hilo halijafika hata kwenye Renta huku likiwa limejengwa chini kiwango.
Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi amemuagiza mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya hiyo kupitia idara ya ujenzi kutoa taarifa kwanini hawakushiriki kutoa huduma za kiutaalamu katika kusimamia jengo hilo la umma kabla na wakati ujenzi unaanza.

 .......................................................................................................

Salva Kiir Akutana na Museveni Uganda


Kiir na Museveni (1) Kiir na Museveni (2) Kiir na Museveni (4) Kiir na Museveni (5) Kiir na Museveni (6)
Na Leonard Msigwa/GPL
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ameitwa na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni kwenye Ikulu ya nchi hiyo na kufanya mazungumzo naye.
Ziara hiyo ya ghafla imekuja siku chache baada ya kutokea kwa mapigano makali kwenye mji wa Juba ambao ndiyo makao makuu ya nchi ya Sudan Kusini.
Mapigano hayo yalivihusisha vikosi vitiifu kwa Rais Kiir dhidi ya vile vinavyomuunga mkono Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Riek Machar ambaye mpaka sasa hajulikani wapi alipo tangu kuzuka kwa mapigano hayo.
Lengo la ziara hiyo ya ghafla ni kujaribu kutatua mgogoro baina ya Rais Kiiir dhidi ya makamu wake na baada ya mazungumzo hayo Rais Kiir amerejea nchini kwake.

 

.......................................................................................................

BASI LA TAHMEED KUTOKA TANGA KWENDA DAR ES 

SALAAM LATEKETEA KWA MOTO
index1
Basi la TAHMEED lililokuwa likitoka mkoani Tanga kuelekea jijini Dar es salaam limeungua moto na kuteketea kabisa maeneo ya Kabuku mkoani humo Habari zinasema abiria wote wamenusurika katika tukio hilo baya lakini mizigo na basi lenyewe vimeungua na kuteketea kabisa kwa moto kwa jinsi inavyoonekana katika tukio hilo katika picha inaonekana moto ulianzia mwenye magurudumu ya nyuma upande wa kulia kama inavyoonekana.
(PICHA KWA HISANI YA MITANDAO YA KIJAMII)
index2Hapa likionekana limeteketea kabisa  na haikuwezekana

......................................................................................................................................

  Wasanii wafanya uchafu!

Zainabu Ally na Naomy Mmbaga wakifanya yao.
Stori: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Katika hali ya kushangaza, wasanii wa kike wanaochipukia kwenye anga la filamu Bongo, Zainabu Ally na Naomy Mmbaga, wamenaswa wakifanya vitendo vichafu wakiwa lokesheni.
Tukio hilo lililopigwa chabo na kachero wetu, lilijiri juzikati katika Hoteli ya KD iliyopo maeneo ya Akachube, Kijitonyama jijini Dar wakati wasanii hao walipokuwa wakiigiza muvi yao ndipo walipofanya uchafu huo baada ya kukolea na ‘ulabu’.
“Awali kabla ya kuanza kurekodi walianza kupiga mambo yao, baada ya kurekodi ndipo wakaongezea tena mitungi na hapo ndipo walipokolea na kuanza kufanya mambo ya ajabu,” alizungumza kachero wa kujitegemea aliyeshuhudia tukio hilo.
Kachero wetu alifanikiwa kuwafotoa picha kadhaa lakini alipojaribu kuwauliza kulikoni wafanye vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya Kitanzania, wasanii hao hawakutoa majibu ya moja kwa moja kutokana na kukolea ulabu.
Hata hivyo, kesho yake Naomy alipatikana na alipoulizwa kwa nini walifanya vitendo hivyo aliomba stori hiyo isitoke kwa madai itamharibia.
“Please iache hiyo bwana, itaniharibia. Si unajua yale ni mambo ya lokesheni tena, mzee akijua itakuwa noma,” alisema Naomy ambaye ameshauza nyago kwenye Sinema ya Laghai, Penzi la Giza, F.B.I, Part of Job Samira na nyingine kibao.
..................................................................................................................................................

MASTAA WA BONGO WANAOONGOZA KWA SKENDO ,KILA KUKICHA KWENYE MITANDAO.

Wema Sepetu.
Mastaa mbalimbali wa Bongo wamekuwa wakiandamwa na skendo huku baadhi wakiona ndiyo njia ya kujing’arisha kisanii.Skendo zao zimekuwa za aina mbalimbali lakini wengi wamekuwa wakiandamwa na skendo za ngono.Katika makala haya utaipata Top 10 ya mastaa wa kike waliondamwa na skendo za ngono. Baadhi wamekumbwa na skendo za kunaswa kwenye mitego ya kujiuza na wengine wakiingia kwenye listi hii kutokana na tabia ya kubadili wanaume kama nguo.
Kwa maana hiyo kumi bora hii itawagawa katika Kundi A na B ambapo Kundi A ni la wale ambao walikanyaga skendo ya kujiuza na Kundi B ni la waliogandwa na skendo ya ngono kwa tabia zao za kubadili wanaume.
Jokate Mwegelo.

KUNDI A
Mmoja kati ya mastaa wanaoingia kwenye kundi hili ni Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’. Huyu aliwahi kuwekewa mtego na kunaswa baada ya kukubali kujiuza kwa mwanaume aliyemtajia dau kubwa na hatimaye akaingia mkenge.
Lulu Semagongo; aliwahi kuingia kichwakichwa kwenye mtego kama wa Jack Chuz ambapo naye aliwahi kutegeshewa mwanaume na kuulizwa kama anaweza kukubali kuuza ngono kwa kiasi gani.


Kuashiria kuwa ndo’ zake, akitoa dau lake na mchezo ukaenda hadi gesti ambapo alifumwa laivu na mwanaume huyo kitandani.Baby Madaha; Licha ya kipindi f’lani kudaiwa kuwa kwenye uhusiano na meneja wake aitwaye Joe Kairuki, aliwekewa mtego kwa kutumiwa meseji na mwanaume kuulizwa kama wanaweza kukutana faragha na kwa kiasi gani ambapo naye alitoa dau lake.

 
Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’.

Hata hivyo, baadaye alishtukia mchezo licha ya mawasiliano yake na mwanaume huyo kuonekana wazi kwamba alikuwa anaelekea kuingia kingi. Isabella Francis ‘Vai wa Ukweli; Naye aliwahi kudaiwa kuyaendesha maisha yake kwa kuigiza na kujiuza pia, akawekewa mtego kama ilivyo kwa wenzake na siku ya tukio, alifika hadi ‘kiwanja’ huku akisisitiza kwamba fedha mbele. Kutokana na maelezo yake hayo, ikaonekana ni kweli huwa anafanya k’abiashara hako’ haramu.

Elizabeth Michael ‘Lulu’.

KUNDI B
Hili ni wale ambao wanasifika kwa katabia ka’ kubadili wanaume kama nguo.
Elizabeth Michael ‘Lulu’; Kiumri anaonekana mdogo lakini naye yumo. Huyu aliwahi kuripotiwa kuwa kwenye uhusiano wa siri na marehemu Steven Kanumba kisha baadaye akadaiwa kutoka na mheshimiwa John Komba (marehemu ambaye aliwahi kukanusha uvumi huo).

Pia binti huyo anadaiwa kuwa eti alikuwa mpenzi wa huyu bilionea wa Arusha aliyefariki dunia, juzikati aitwaye Lusekelo Samson ‘Seki’ ambaye kuna kipindi pia Husna Maulid na Lulu waliwahi kudaiwa kugombana kisa kikiwa ni mwanaume huyo.

Wema Sepetu
Ukiacha wale ambao sisi hatuwajui, Wema amekuwa na msururu wa wanaume huku staili yake ikiwa ni ile ya bandika-bandua. Wanaume ambao wengi ni mastaa waliowahi kumgusa ni Herry Samir ‘Mr Blue’, marehemu Steven Kanumba, Hartman Mbilinyi, Yusuf Jumbe, Chaz Baba, CK na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Huyu pia aliwahi kupiga picha za utupu kadhaa katika kipindi chake cha ustaa, hali inayomfanya afiti kwenye Top 10 hii.

Jacqueline Wolper.

Jokate Mwegelo; ni mwanadada anayeonekana mpole sana lakini naye hawezi kukosekana kwenye orodha hii. Ni kati ya mastaa waliowahi kuwa na uhusiano na wanaume mbalimbali wakiwemo Hasheem Thabit, Diamond aliyempora kutoka kwa Wema na wengine ambao amekuwa akifanya siri.Pia ni kati ya mastaa wanaopenda sana kupiga picha za nusu utupu, tabia inayomfanya wakati mwingine atafsiriwe kuwa anatangaza biashara.

Jacqueline Wolper; Anaingia kwenye orodha hii kutokana na ukweli kwamba amekuwa akibadili wanaume mara kwa mara huku wakati mwingine akiingia kwenye migogoro ya kugombea wanaume.Aliwahi kuingia kwenye mvutano na Husna Maulid wakimgombea mwanaume aitwaye Radjabu Mwami. Pia mwanadada huyu amekuwa akihusishwa na kale kamchezo ka’ usagaji ambapo mwenyewe amekuwa akikanusha mara kwa mara.

Agness Gerald ‘Masogange’.

Agness Gerald ‘Masogange’; Nani asiyemjua mwanadada huyu kwa kupiga picha za nusu utupu huku akidaiwa kuwa ni mmoja wa mastaa ambao wanaendesha maisha yao kwa kutegemea wanaume?Mkanda wake wa ngono uliwahi kuvuja na mwenyewe amekuwa hajali kulianika umbo lake tata.

Stara Thomas; ni staa ambaye amekuwa kwenye gemu la muziki kwa muda mrefu. Naye anaingia kwenye orodha hii kutokana na madai kuwa, aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa siri na marehemu Adam Kuambiana. Pia hivi karibuni mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mumewe aitwaye Raumu Ally alimfumania na mwanaume mwingine. 
Hao ni baadhi ya mastaa ambao wanaingia kwenye orodha.

 .......................................................................................................

Julieth Katebe Atwaa Taji la Miss Dar City Centre 



Miss Dar City Centre (1)
Mshindi wa shindano la Miss Aqua Dar City Centre, Julieth Katebe akiwa katika pozi baada ya kutangazwa mshindi.
Miss Dar City Centre (2)
Tano Bora ya Miss Aquar Dar City Centre.
Miss Dar City Centre (3)
Kaimu wa nafasi ya Miss Aquar Dar City Center ambaye anamaliza muda wake, Sabina Thomas akiwa kwenye pozi. Katika mashindano yaliyopita aliibuka mshindi namba tatu.
Miss Dar City Centre (4)
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed ‘TID’ akikamua jukwaani katika shindano hilo.
Miss Dar City Centre (5)
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Elias Barnabas ‘Barnaba Boy’ naye akifanya yake.
Miss Dar City Centre (6)
Afisa Masoko wa Global Publishers, Yohanna Mkanda akiwa red carpet na mrembo.
Miss Dar City Centre (7)
Top Ten ya Miss Dar City Centre wakiwa kwenye pozi baada ya kutangazwa.
Miss Dar City Centre (8)
Wanamitindo maarufu Bongo, Martin Kadinda na Hamisa Mobeto wakiwa kwenye pozi katika tamasha hilo.
Miss Dar City Centre (9)
Top 5 ya Miss Dar City Centre wakiwa kwenye pozi.
Miss Dar City Centre (10)
Warembo wakiwa kwenye red carpet na Miss Aquar Dar City Centre.
Stori: Boniphace Ngumije
Usiku wa kuamkia leo palikuwa hapatoshi ndani ya Ukumbi wa Mtana (Jengo la LAPF), Kijitonyama jijini Dar, kulimofanyikia shindano kubwa la warembo lililojulikana kwa jina la Zan Aqua Miss Dar City Centre.
Katika shindano hilo ambalo lilikuwa linadhaminiwa na Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Global Publishers, kulifanyika pia burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii Khalid Mohamed ‘TID’ na Elias Barnabas ‘Barnaba’ lakini pia watu waliohudhuria shindano hilo waliburudika kwa vinywaji na muziki mzuri.
“Shindano limekwenda vizuri, mshindi wetu Julieth Katebe amejinyakulia zawadi ya shilingi milioni moja taslimu na nywele bandia zenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka katika kampuni ya Prima Afro, washindi wengine wamebeba zawadi mbalimbali lakini pia mshindi wa kwanza mpaka wa tano wameingia kwenye kinyang’anyiro cha Miss Ilala,” alisema mratibu wa shindano hilo, Nancy Joseph.

 

.......................................................................

Busu la Penny lazua utata

Busu ambalo mtangazaji Peniel Mungilwa ‘Penny’ amempiga mwigizaji Shamsa Ford limezua utata kufuatia watu kumhusisha na tabia isiyofaa.

Hayo yalijiri hivi karibuni baada ya mtangazaji huyo kutupia picha kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram ndipo wafuasi wa mtandao huo walipoanza kumsema vibaya wakidai anajiabisha kwa vitendo visivyofaa.

Alipoulizwa kuhusiana na jambo hilo, Penny alisema: “Hayo ni maneno tu huwa hayani sumbui, lile ni busu la kawaida. Nimembusu kama rafiki lakini nawashangaa hao wanaozua mambo yao na kuzungumza tofauti.

 

...................................................................................................

Mabasi yaendayo kasi katika majaribio Dar



DART (1) DART (2) DART (3) DART (4) DART (5) DART (6) DART (7)
Kamera za tovuti hii leo zimenasa taswira saba za mabasi yaendayo kasi yakiwa katika majaribio kwenye maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabasi hayo ya Mradi wa Dart  yanatarajia kuanza rasmi kutoa huduma Mei 10, mwaka huu.
Mbali na majaribio hayo, bado mabasi yaendayo kasi yanakutana na changamoto zikiwemo za waendesha pikipiki, raia na daladala kupita kwenye njia ya mabasi hayo na kusababisha msongamano wa magari kitendo ambacho kinalazimu mabasi hayo nayo kujikuta yakikaa foleni.
Kupitia taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi (Dart), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar es Salaam (Darcoboa), Sabri Mabrouk ni kwamba Daladala zote zinazofanya safari zake katikati ya jiji zimetakiwa kuondoka ifikapo Mei 2, mwaka huu huku akieleza kuwa tayari wamiliki wote wa mabasi walishalipwa fidia ya kubadili njia.
“Wamiliki wote wa mabasi wameshalipwa fedha zao tangu Desemba mwaka jana, hakuna anayedai na tumewapa siku saba kuondoka barabarani kabla ya Mei 2,” amesema Mabrouk.
(Picha na Salum Yasin / GPL)
......................................................................................................................









Hatarii..!!!






......................................................................................................................

SHEIKH PONDA AONDOLEWA HOSPITALI NA KUPELEKWA GEREZA LA SEGEREA.....WAKILI WAKE ALAANI TUKIO HILO


Wakili Nassor Jumaa anayesimamia Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (54) ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi mpya ya kufanya uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezungumzia kitendo cha kumhamisha mteja wake kutoka hositalini hadi Segerea.

Leo hii majira ya saa 7 mchana nje ya viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar  es Salaam amesema kuwa amesikitishwa na hatua  ya vyombo vya dola kumuondoa Sheikh Ponda aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Kitengo  cha Taasisi ya Tiba  ya Mifupa  na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu na kisha kumhamishia katika gereza la Segerea.


Wakili Jumaa amesema amesikitisha na kitendo hicho kwani muda mfupi baada ya wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kumaliza kumsomea Sheikh Ponda shitaka linalomkabili, Hakimu Hellen Riwa alitoa amri ya kukaa chini ya ulinzi Sheikh Ponda aendelee na matibabu.

Jumaa akaongeza  kuwa   ameshangazwa kuona leo, wanausalama wamemtoa Sheikh Ponda wodini na kumpeleka katika gereza la Segerea na kwamba atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapojatwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

“Kwa kweli kitendo hicho kime nisikitisha na kunishitua sana… ila tunatafakari ni hatua gani za kisheria tutazichukua huko siku za usoni,”alisema Jumaa.

 Kwa upande wao familia ya Sheikh Ponda wamesema wanalaani kitendo kilichofanywa na serikali cha kumuondoa ndugu yao hospitalini huku akiwa anaendelea kupata matibabu.

Msemaji wa familia hiyo Is-haq Rashid, alisema kutokana na hali hiyo kama familia wanalirudisha suala la Sheikh Ponda kwa uongozi wa jumuiya na Taasisi za kiislamu kwa ajili ya hatua zaidi ya kuhakikisha kiongozi mwenzao anakuwa salama.

“Uporaji huu wa mgonjwa unazidi kutupa mashaka juu ya dhamira ya serikali hasa ikiwa tunalituhumu jeshi la polisi katika kumdhuru Sheikh,hatujui kwanini kila wakati wanafanya mambo yao kwa kuvizia kama mwanzoni tuliwaomba viongozi wenzie wawe na subira juu ya yaliyotokea sasa tunaachia hili walizungumzie wao.”alisema Is-haq.


Wakati huo huo taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa viongozi wa Jumuiya na Taasisi zaKiislamu  walikuwa katika kikao kizito cha kujadili hatua hiyo ya kuporwa kwa Sheikh Ponda akiwa katika matibabu

  ................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

MAJANGA: BABA MZAZI AMBAKA BINTI YAKE


Aziza Kibibi alikuwa na umri wa miaka minane tu wakati baba yake - Mwongozaji wa Tuzo za muziki za MTV - alipoanza kumbaka.

Alipofika miaka 10, somo ambalo Aswad Ayinde alikuwa akimfundisha binti yake 'jinsi ya kuwa mwanamke' likabadilika na ubakaji wake wa mara kwa mara ukazaa watoto watano kutokana na makosa ya kujamiiana kwa kisingizio cha kujaribu kutengeneza damu 'halisi'.

Kwa namna ya ajabu mwanamke huyo jasiri, ambaye sasa ana miaka 35, ameolewa na anaendesha biashara inayoshamiri ya uokaji, alizungumza hadharani kuhusu maisha yake ya utoto yaliyojaa kiwewe wiki hii kwa mara ya kwanza.

Kibibi alielezea maisha yake ya utoto kwamba yalianza katika hali ya kawaida. Aliishi na mama yake na baba kwenye ghorofa ya tatu ya jengo moja huko Paterson, New Jersey, huku babu na bibi yake wahamiaji kutoka Jamaica wakiishi ghorofa ya chini.

Kibibi alikuwa akisomea nyumbani lakini bado aliruhusiwa kucheza na watoto wa jirani. Pale familia yake ilipoongezeka na kufikisha watoto wanane wakahamia kwenye nyumba kubwa zaidi katika jengo hilo.

Hapo ndipo Kibibi akaanza kukua kiasi cha baba yake kuanza kumtazama kwa jicho la matamanio.

"Aliniambia nilikuwa wa kipekee. Mwanzoni, ilikuwa ni katika kunifundisha jinsi ya kuwa mwanamke," alisema. 


"Wakati huo alianza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mimi, aliendelea kutumia nguvu zaidi na zaidi. Pale nilipoanza kupigana naye, alinipiga. Alinipa vitisho vingi mno."

Baba yake akaanza kubadilika, na kuitawala mno familia kimabavu. Aliwahamisha kutoka kwenye nyumba ya babu yao na kuwapeleka kwenye nyumba nyingine huko Paterson kabla ya kuwahamishia Eatontown huko Southern New Jersey. Watoto hao walikuwa wakiruhusiwa tu kutazama televisheni kwa muda mchache mno, na hakuna ambacho kilielezea asili ya maisha ya familia.

Dawa za kisasa zilipigwa marufuku katika nyumba hiyo, na alimweleza mkewe kwamba uhusiano wake na Kibibi ulikuwa katika kumtibia ukurutu.

Kibibi hakuwa pekee ambaye Ayinde alikuwa akifanya naye mapenzi. Alikuwa na mwanamke wa makamo - mwanasheria wa Manhattan ambaye alizaa naye watoto wawili - na pia alikuwa akimdhalilisha kijinsia mmoja wa dada zake Kibibi.

Alijiita mzee wa mitala na nabii. Familia yake ilikuwa ikiruhusiwa kumwomba Mungu lakini wanaweza tu kufanya hivyo kupitia kwake.

"Alisema dunia ilikuwa ikielekea ukingoni, na angebaki yeye tu na watu wake na kwamba alikuwa amechaguliwa," mkewe wa zamani, Beverly Ayinde alitoa ushahidi kwenye kesi moja mwaka 2010. Alisema alikuwa akijaribu kutengeneza damu yake 'halisi' kwa kuzaa na binti zake mwenyewe.

Pale mtoto wa kwanza wa Kibibi alipozaliwa bila matatizo, Ayinde alitumia kigezo hicho kama uthibitisho na kuendelea kumbaka msichana huyo hadi kumpa ujauzito.

Watoto waliofuatia hawakuwa na bahati hivyo.

Mabinti wawili waliofuatia waliozaliwa kutokana na baba yake waligundulika na ugonjwa wa phenylketonuria (PKU) ambao huzuia mwili kuweza kuvunja amino acid. PKU inaweza kusababisha kuharibika ubongo na kifafa.

Dk Anna Haroutunian, mtaalamu wa PKU ambaye aliwatibu watoto wa Kibibi, alisema hakika wamepata ugonjwa huo sababu ya uzao baina ya wazazi wa nasaba moja.

Katika miaka hiyo, Kibibi amekuwa akikumbwa na shinikizo la kutoroka. Aliweza tu kulala sababu ndoto zake zilikuwa nzuri kuliko maisha halisi.

"Nilikuwa na ndoto ya kukimbia. Niliwaza kuwachukua kaka na dada zangu wote - mmoja wa dada zangu alikuwa mtoto, na nilikuwa nikimlea - nilikuwa na mawazo ya kuota matiti na kupata maziwa na kukimbia nao mahali fulani," alisema.

Pale alipokuwa mtu mzima na mmoja wa watoto zake wa kiume alipougua, hatimaye akapata hamasa kumpeleka hospitalini wakati Ayinde alipokuwa amekwenda mjini kwa safari ya kibiashara.

Lakini hakuwa akijua jinsi ya kuongea na madaktari na mfanyakazi wa jamii akaingia, akaitaarifu Idara ya Vijana na Huduma za Familia.

Pale Ayinde aliporejea kutoka safari yake ya kibiashara aligadhibika, na kutishia kumrejesha kwa nguvu mtoto wake kutoka hospitali.

Huduma za Watoto waliingia kabla hajachukua uamuzi huo na kuwaweka katika nyumba tofauti.

Baada ya hapo Kibibi, mama yake na dada yake walimtoroka Ayinde wakati akifanya harakati za kuwarejesha nyumbani watoto wake.

Akipambana kuwarejesha watoto katika himaya yake pia Kibibi aliwezeshwa, na kubadili maisha yake baada ya udhalilishaji. Sasa anaishi huko East Orange, New Jersey pamoja na mumewe.

Alirejea shule na atamaliza shahada yake ya sanaa kwenye Chuo cha Essex County mwaka huu. Pia anaendesha biashara yake ya uokaji na siku moja anapanga kuanzisha mgahawa.

Kibibi na dada yake mwishowe wameamua kufungua mashitaka dhidi ya baba yao mdhalilishaji. Walichelewa kufungua mashitaka kutokana na kutokuwa na uhakika wa athari ambazo zingeweza kuwapata watoto wao.

Ameeleza hadharani stori yake kwa matumaini ya kuweka utofauti kwa wote waliopitia maisha kama yake.

"Badala ya kuwa uzoefu niliokuwanao, pengine hii imeniimarisha. Kile kisichotusambaratisha kinatufanya tuwe imara zaidi."



SHEREHE YA MAKABIDHIANO YA MAGARI YA JESHI 591 LEO KUTOKA KATIKA SERIKALI YA INDIA

SERIKALI YA INDIA IMEKABIDHI MAGARI 591 KWA JESHI LA ULINZI MAGARI HAYO YALIKABIDHIWA LEO



MKUU WA JESHI LA ULINZI DAVIS MWAMUNYANGE AKISALIMIANA NA WAGENI



MKUU WA JESHI LA ULINZI DAVIS MWAMUNYANGE AKISALIMIANA NA WANAJESHI


BAADHI YA VIONGOZI WA JESHI LA WALIOHUDHURIA
WAZIRI AKISALIMIANA NA WANAJESHI
WAZIRI AKISALIMIANA NA WAGENI
WAZIRI AKISALIMIANA NA WAGENI
BRASS BANDI
KIKUNDI CHA SANAA CHA JKT MGULANI WAKIONYESHA UMAHILI WAO WA KUCHEZA NGOMA YA MSEWE
WAZIRI WA ULINZI SHASI VUAI AKISOMA HUTUBA YAKE



BALOZI WA INDIA DEBNATH SHAW AKIMKABIDHI WAZIRI WA ULINZI FUNGUO
WAZIRI WA ULINZI AKIWA KWENYE MOJA YA GARI LA JESHI MARA BAADA YA MAKABIDHIANO

WAZIRI WA ULINZI NA USALAMA SHASI VUAI NA BALOZI WA INDIA WAKIONDOKA 

PICHA YA PAMOJA
WAZIRI WA ULINZI NA USALAMA SHASI VUAI NA BALOZI WA INDIA WAKIONDOKA
BRASS BAND WAKITUMBUIZA



WAZIRI WA ULINZI NA USALAMA SHASI VUAI AKIAGANA BALOZI WA INDIA NCHIN DEBNATH SHAW

MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT JIJINI MBEYA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 30 NA VIBOKO 12 BAADA YA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI


MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka 19.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema Mahakama imemtia hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na Shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema Beni(19).

Amesema Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 hadi Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 130(2)e na 131 (1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji.

Kutokana na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta Mtuhumiwa na makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai kuwa Shitaka limedhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.

Kwa upande wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kutokana na mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na umri wake na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka 19 ili hali Mtuihumiwa akiwa na Miaka 57.

Pia alidai kuwa Mtuhumiwa huyo alimharibia masomo na maisha yake binti huyo na vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani , hivyo aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya Watoto kwa kutumia amri ya kutaifisha.

Hata hivyo Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kuhusu kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa huyo aliomba kupunguziwa adhabu kwa madi kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na msaada.

Aidha kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30 na viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili amehukumiwa kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania kwa familia ya Mhanga.

Ameongeza kuwa Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya kama hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama yake.

MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi yake.
Wananchi Mbalimbali wakisubiri Kusikiliza Kesi ya MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi



   MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe   akiwa anatolewa mahakamani Baada ya kusomewa kifungo cha Miaka 30 Jela

  Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa wanatoka Mahakamani Baada ya Baba yao kusomewa kifungo
  Mtoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa anaongeaa na waandishi wa Habari baada ya kesi kumalizika
 Waumini Mbalimbali wakiwa nje Baada ya kesi kumalizika


Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa nje hawaamini  baada ya kusikia Baba yao anafungwa Miaka 30

  Binti  anaye daiwa kufanyiwa kitendo hicho akilia kwa Uchungu baada ya kesi kwisha

Mbeya yetu 

    

NANDO WA TANZANIA APENDEKEZWA KUTOKA NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER...KURA YAKO INAHITAJIKA


Mchezo unazidi kuwa mgumu kadri siku zinavyozidi kwenda sababu idadi ya wanaopaswa kuendelea na mchezo ndivyo inavyohitajika kuwa ndogo mpaka siku ya 91 atakapobaki mtu mmoja wa kukabidhiwa $300,000 kama zawadi ya BBA The Chase. 

Nominations za wiki hii zimewagusa baadhi ya washiriki ambao hawajawahi kabisa kupendekezwa kutoka, na wengine ambao wameshawahi kupendekezwa mara moja na zaidi lakini waliokolewa na kura za watazamaji.


Baada ya kupona kutoka wiki iliyopita na kuwa HOH , cheo kilichompa nafasi ya kujiokoa katika nomination zilizopita Nando wa Tanzania ameungana na washiriki wengine 6 katika orodha ya majina yaliyotajwa na Biggie kuingia katika kikaango cha eviction ya wiki hii.


Washiriki ambao wameingia kwa mara ya kwanza katika nominations za wiki hii ni pamoja na aliyekuwa kipenzi cha Huddah mjengoni, Angelo wa Afrika Kusini ambaye amewekwa na HOH wa wiki hii Elikem aliyejiokoa na nafasi yake kumuwekea yeye.


Fatima wa Malawi, Bimp wa Ethiopia pamoja na Cleo wa Zambia ndio washiriki wengine ambao wameingia dangerzone kwa mara ya kwanza toka mchezo umeanza.


Washiriki ambao waliwahi kupendekezwa na kuokolewa na kura za watazamaji na wameingia tena wiki hii ni pamoja na Pokello wa Zimbabwe, Hakeem wa Zimbabwe pamoja na Nando wa Tanzania.


Wiki hii Ghana na Nigeria ndio zimekalia viti vya utawala wa nyumba, Ruby ikiongozwa na Elikem na Melvin akiiongoza Diamond.


Kura yako inahitajika kumwokoa Nando ili aendelee kubaki na kuiwakilisha Tanzania katika msimu wa 8 wa BBA The Chase unaoendelea Afrika Kusini.

  Je, wajua ni nini  unapaswa kufanya Unapotokea kumpenda mtu aliye na mpenzi wake,


Tumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametuwezesha kuonana tena wiki hii tukiwa wazima. Lakini pia tumshukuru kwa kutuletea kitu kinachoitwa mapenzi.

Mapenzi yamekuwa yakichukua nafasi kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku na yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa furaha kwa kila mtu.


Kama huamini, angalia wale waliotokea kupenda na wao wakapendwa, utabaini nyuso zao zimetawaliwa na

furaha isiyo na kifani. Lakini mapenzi hayo hayo yamekuwa ni chanzo cha vilio kwa baadhi ya watu.

Mpenzi msomaji wangu, kupenda hakuna macho! Moyo ukishapenda hausikii la kuambiwa. Katika hili ndiyo maana unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa demu ambaye hawaendani kabisa lakini moyo wake ndiyo umeshapenda.


Ilishawahi kutokea msichana akampenda kijana mmoja ambaye ni fukara kupita maelezo. Yeye akawa ndiyo anamhudumia kwa kila kitu. Akamfanyia mpango wa ajira na mwisho wake wakafunga ndoa.


Sasa hivi wanaishi maisha ya furaha na amani. Wamegeuka mfano wa kuigwa kwa jinsi wanavyopendana lakini huko nyuma msichana huyo alikuwa akichekwa kwa kutoa penzi kwa mwanaume asiye na mbele wala nyuma.


Hayo ndiyo mapenzi jamani! Lakini pia katika kufurukuta kumtafuta mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume anaweza kujikuta unaangukia kwa demu ambaye tayari ana mpenzi wake.


Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje?


Utapambana kuhakikisha unapata kile ambacho moyo wako umekipenda au utakubaliana na ukweli kwamba huwezi kuwa naye kwa kuwa ana mtu wake? Inapofikia hatua hiyo unaweza kujikuta upo njia panda hasa pale ambapo huyo mwenye mtu wake naye anaonesha kuwa na chembechembe za mapenzi kwako.

Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kukabiliana na hali hii.


Chunguza

Tumia muda wako mwingi kuchunguza juu ya uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye ‘future’ naye. Ndiyo maana nikasema chunguza uhusiano wake kwanza.


Usitafute uadui

Baada ya kuchunguza, ukibaini kwamba uhusiano wao hauko ‘siriasi’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na likaufurahisha moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na wanaelekea kuoana, usitafute uadui bure, kaa pembeni.


Una nafasi kwake?

Sawa umetokea kumpenda msichana aliye na mtu wake, umeshawahi kujiuliza kama una nafasi ndani ya moyo wake? Anaonesha dalili fulani za kukupenda kama unavyompenda na ni mtu anayeonesha kukumisi anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi.


Ni rahisi kubadili uamuzi wake?

Unadhani huyo uliyetokea kumpenda anaweza kubadili maamuzi ya kumuacha huyo aliyenaye kama kweli hawana ‘future’? Utagundua hilo kwa kuongea naye na kumsikia kama anaweza kufanya maamuzi hayo ili awe na wewe.


Pingana na moyo wako

Ifike wakati upingane na moyo wako. Unajua moyo wako kukuambia kuwa unataka kuwa na uhusiano na demu ambaye tayari ana mpenzi wake wakati mwingine utakuwa unakupotosha.


Kwa hiyo ukiona vipi, pingana nao. Acha kumng’ang’ania msichana mwenye mpenzi wake licha ya ukweli kwamba, huenda wewe ndiye mwenye nafasi ya kuwa mume wake na siyo huyo aliye naye.


Urafiki ni poa?

Umempenda sana na hauko tayari kumkosa katika maisha yako lakini imetokea kwamba tayari yuko na mtu na umebaini huna nafasi kwake kabisa? Usiumie, omba angalau urafiki. Siyo urafiki wa kivile sana ila angalau pale unapotaka kusikia sauti yake kwa kumsalimia tu, upate nafasi hiyo.


Usiumie, yupo mwingine

Haina haja ya kujitafutia vidonda vya tumbo bure kwa kuwa tu umebaini uliyetokea kumpenda tayari ana mtu. Chukulia ni hali ya kawaida, mademu wazuri ambao wanaishi singo wapo kibao huko mtaani, ni suala la wewe kutulia tu. Amini yupo mwingine ambaye atayafanya maisha yako yawe ya furaha.


Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, unapotokea kumpenda mtu fulani, pambana kuhakikisha unampata kwa sababu ukimkosa maisha yako yanaweza kuwa gizani. Ila pale utakapoona uwezekano wa kuwa naye haupo, usilazimishe ndugu yangu. Kumbuka haya ni maisha tu!

MAKAHABA WANAOJIUZA SINZA WATIWA MBARONI NA MGAMBO WA JIJI





Mgambo wa jiji la Dar es Salaam wakiwa katika zoezi la kuwakamata akinadada wanaofanya biashara ya kuuza miili yao maarufu kama Machangudoa katika eneo la Sinza. 

Picha hizi ( juu)  zinaonesha  namna walivyokuwa wakipakiwa ndani ya Gari tayari kwa kupelekwa katika vyombo vya sheria



JOHN MNYINKA ADAI KUWA KESHO WATAWASHA MOTO TENA JIJINI ARUSHA


WAKATI Jeshi la Polisi Mkoani Arusha ikiendelea kumsaka Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema,Mbunge wa Ubungo John Mnyika kesho atawasha moto mwingine wa maombolezo uliotawanywa kwa mabomu jana.

Mnyika atakuwa msatari wa mbele kuongoza wafuasi wa Chadema kuaga miili ya watu watatu waliouawa katika shambulio la kigaidi Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Soweto.


Mbali na Mnyika zoezi hilo pia litasimamiwa na wabunge wanne wa Chadema walioachiwa huru kwa dhamana leo kwakua upelelezi wa kesi zao hazijakamilika.


wabunge hao waliachiwa huru kwa dhamana katika Kituo Kikuu cha Polisi Mkoani hapo kabla ya kufikishwa Mahakamani na kutakiwa kurudi Polisi Julai 22 mwaka huu .


Wabunge hao Said Arfi (Mpanda Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti Maalumu), walipewa dhama hiyo majira ya saa nane mchana.


Kabla ya Wabunge hao kuachiwa huru kwa dhamana, maelfu ya wafuasi wa Chama hicho walijazana katika Mahakama hiyo wakisubiri msafara wa wabunge hao, na mara baada ya kupewa taarifa kwamba wabunge hao wameachiwa huru wakiwa Polisi,maandamano makubwa yakaelekea katika Kituo cha Polisi.


Akizungumza baada ya dhamana hiyo Tundu Lissu alisema kwamba, Jeshi la Polisi limempa hasara kubwa baada ya kuvunja mawani yake na kwamba hivi sasa hawezi kufanya kazi yoyote mpaka atakapo pata mawani mapya.



Mbunge wa Ubungo John Mnyika aliyefika jijini Arusha kwa ajili ya kuwawekea dhama wabunge hao alisema kwamba, Chama hicho bado kitaendelea na mipango yake ya kuomboleza na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu waliouawa kwa shambulio la bomu katika mkutano wa kisiasa wa Chama hicho Juni 15 mwaka huu katika Uwanja wa Soweto, marehemu hao ni pamoja na Judith Moshi, Ramadhan Juma na Amir Ally, waliofariki kwenye mlipuko wa bomu.


Akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutoka Polisi Mnyika alisema, "Kesho tutaendelea na zoezi la kuwaaga wenzetu waliofariki dunia katika mkutano wetu, na watazikwa kwa heshima zote za Chama,zoezi litaanzia kanisani kabla ya kwenda katika eneo maalum ilipoandaliwa kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho".


Hata hivyo Mnyika alikataa kujata jina la kanisa muda wala eneo iliyopangwa kwa madai kwamba ni mapema sana.

 VURUGU ZA ARUSHA: CHADEMA YAGOMA KUTOA USHAHIDI POLISI, LEMA AJIFICHA KWA MCHOMA NYAMA ....WAANDISHI WAAMBULIA KICHAPO

Wabunge wanne wa Chadema, Said Arfi (Mpanda Mjini), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Mustapha Akunaay (Mbulu) na Joyce Mukya (Viti Maalumu) wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika na mkusanyiko usio halali kwenye Uwanja wa Soweto jana.
Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Kamishna Paul Chagonja alisema jana kwamba pamoja na wabunge hao pia wamewakamata watu wapatao 60 kutokana na vurugu zilizozuka jana baada ya Polisi kuwatawanya kwenye uwanja huo waliokuwa wamekusanyika kuomboleza vifo vya watu watatu; Judith Moshi, Ramadhan Juma na Amir Ally waliofariki kwenye mlipuko wa bomu uliotokea kwenye uwanja huohuo, Jumamosi iliyopita.
Mbali ya viongozi hao, alisema wanawasaka Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.
“Tunawasaka wabunge ili tuwajumuishe na watu hawa kwa kosa la kuhusika na mkusanyiko usiokuwa halali. Hadi sasa tumefanikiwa kulinasa gari la Mbowe,” alisema Chagonja.
Pia kamatakamata hiyo imemkumba Mpigapicha wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Ashraf Bakari. Polisi walilazimika kutumia nguvu kuwatawanya waombolezaji hao.
Awali, Kamishna Chagonja alisema jana asubuhi kuwa wamelazimika kuzuia viwanja hivyo kutumika baada ya wamiliki wake, AICC kuzuia shughuli za Chadema kwenye eneo lao na kwamba upelelezi bado unaendelea katika viwanja hivyo.
Kamishna Chagonja aliwaonyesha waandishi wa habari barua aliyosema imeandikwa na uongozi wa AICC kuzua Chadema kuendelea kuutumia Uwanja wa Soweto.
Mabomu yarindima
Dalili za kuzuka kwa vurugu zilianza kuonekana asubuhi baada ya polisi kuzingira uwanja huo na kuzuia watu waliokuwa wameanza kufurika katika eneo hilo kuanzia saa moja kuingia kwa ajili ya maombolezo.
Wakati Polisi wakiwa uwanjani, wananchi walijaa nje ya uwanja na kuonekana kama wamewazingira.
Viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mbowe waliwasili uwanja hapo yapata saa nane mchana na kukuta zuio hilo na kuanza kuzungumza na wananchi ingawa FFU walikuwa wakiwataka watu kutawanyika. Mabomu yalianza kurindima wakati Arfi aliposimama na kuwahimiza wananchi kuelekea Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kuaga miili ya marehemu.
“Tuna muda mfupi sana wa kuzungumza hapa, tunaomba wote tuelekee Hospitali ya Mount Meru kuaga miili ya marehemu kwa sababu uwanja huu umezuiwa na polisi,” alisema Arfi kabla ya kukatishwa na milipuko ya mabomu.

Awali, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema alitoa msimamo wa chama hicho kuwa Mwenyekiti wao, Mbowe na Lema hawatatoa ushahidi wa tukio la bomu wala kujisalimisha polisi kwa sababu hawana imani na jeshi hilo.

“Namtaka Chagonja atangulie mahakamani, tutakutana hukohuko. Mbowe na Lema hawatatoa ushahidi wala kujisalimisha polisi...
” alisema Lissu na kuongeza:

“Kisheria haiwezekani polisi ambao ndiyo watuhumiwa ndiyo wadai kukabidhiwa ushahidi ili wauharibu.”

Mapema Kamishna Chagonja aliwataka Mbowe na Lema kutoa ushahidi wa polisi kuhusika na tukio la kurusha bomu kwenye mkutano wa Chadema la sivyo polisi watatumia sheria kuwalazimisha kufanya hivyo.

Hekaheka

Baada ya polisi kuanza kutupa mabomu saa 8.45 mchana, wabunge, viongozi waandamizi wa Chadema na watu waliokuwa wamekusanyika walilazimika kutimua mbio.

Watu walioshuhudia tukio lile wanasema viongozi hao akiwamo Mbowe na mwenzake Lissu walikimbilia kwenye magari yao. Lema alilazimika kukimbilia kwa wachoma nyama ya nguruwe, (kitimoto) kwenye maeneo ya Kaloleni.

Kabla ya polisi kurusha bomu mahali alipokuwapo Lema, mbunge huyo alisikika akisema:

“Jaribuni kuvumilia, tunajaribu kuwasiliana Serikali ya Mkoa, ili watupe kibali cha kuleta miili ya wapendwa wetu hapa, kuweni wastaarabu kwa sababu mbele yetu kuna wana usalama ambao wanalinda amani, ingawa kufa ni kufa tu, wenzetu wameshakufa na sisi ipo siku tutakufa, lakini kila anayetangulia lazima tumzike kwa heshima zote.”

Kauli hiyo iliwachefua polisi ambao walishatangaza amri ya watu kutawanyika katika viwanja hivyo na kwamba hakutakuwa na suala la kuaga miili ya watu hao katika eneo hilo. Ghasia hizo zilisababisha kusimama kwa shughuli za biashara na kijamii kwa muda jijini Arusha huku watu waliokuwa katika nyumba zilizokuwa karibu na maeneo yalikorushwa mabomu wakilazimika kutoka nje kupata hewa safi baada ya nyumba hizo kujaa hewa ya mabomu.

Polisi waliokuwa wakirusha mabomu waliwakimbiza wananchi hadi maeneo ya Sakina huku wakiendelea kufyatua mabomu kila walipoona mkusanyiko wa watu.

Katika eneo la Kaloleni
, mkabala na Ofisi ya Mtendaji wa Kata hiyo baadhi ya wafuasi wa Chadema walichoma matairi barabarani na kusababisha ifungwe. Pia walichoma matairi katika eneo la Mianzini


Katika eneo la Tanki la Maji
, Barabara ya kwenda Moshi, baadhi ya wafuasi wa Chadema walipanga mawe barabarani na kusababisha msongamano wa magari.

Katikati ya jijini Arusha barabara zilikuwa hazipitiki kutokana na nyingine kufungwa na kusababisha usumbufu mkubwa.

Waandishi nao matatani

Katika vurugu hizo, baadhi ya waandishi wa habari walishambuliwa na polisi. Hao ni pamoja na Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la The Citizen, Zephania Ubwani ambaye kabla ya kuchomoka katika mikono ya askari, alikuwa akiwaonyesha kitambulisho chake cha kazi.

Hata hivyo, askari hao walimtishia kumtandika na kisha kumwambia aondoke katika eneo hilo kwa kuwa haijalishi yeye ni nani.

Mwingine ni mwandishi wa gazeti la Nipashe, Cnythia Mwilolezi ambaye alilazimika kuacha viatu na vitendea kazi vyake katika Uwanja wa Soweto na kukimbilia kwenye moja ya nyumba zilizopo jirani na eneo la tukio.

Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha, Moses Kilyinga alipigwa na polisi baada ya kuonekana akichukua maelezo.

Kilyinga ambaye alishambuliwa na askari hao alisema mara baada ya askari hao kumkamata, alijitambulisha lakini hawakumwelewa na wakaendelea kumchapa kabla ya kufanikiwa kuchomoka.

Polisi wavamia hospitali
Wakati baadhi ya majeruhi wakidai kushuhudia polisi wakiwapiga risasi watu waliokuwa wakimkimbiza mtu aliyerusha bomu katika tukio la Jumamosi, askari hao juzi walifika katika Hospitali ya Seliani saa mbili usiku wakitaka kumchukua mmoja wa majeruhi kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo. Hata hivyo, hawakufanikiwa baada ya mgonjwa kutokomea kusikojulikana baada ya kupata taarifa za kutaka kuhusishwa na tukio hilo.

Ingawa si polisi wala Chadema waliokuwa tayari kumtaja mgonjwa huyo, inaelezwa kwamba majeruhi anayesakwa ni Abdallah Alila aliyekaririwa na vyombo vya habari jana na juzi akidai kumshuhudia aliyerusha boma akiondoka kwenye moja ya magari ya polisi.

Hata hivyo, Kamishna Chagonja jana alisema kwamba jeshi lake linapenda kushirikiana na raia kupata taarifa na si kutumia nguvu katika kukusanya ushahidi wake.


Mwananchi

MTANGAZAJI WA TIMES FM ( KHADIJA SHAIBU) AJIANIKA "AKIKATA GOGO " CHOONI


MTANGAZAJI wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amewashangaza watu baada ya kutundika mtandaoni picha zinazomuonesha akioga bafuni huku nyingine akiwa chooni  akikata  gogo.
Picha hizo zinapatikana kwenye mtandao wake na hakueleza ilikuwa wapi ila akasema ilikuwa ni siku alipoamua kuitumia wikiendi yake ipasavyo katika hoteli ambayo hakuitaja jina.
 
Baadhi ya watu waliyoziona picha hizo walimponda wakidai eti ni ulimbukeni lakini wapo waliomtetea kwa kusema, ni staili tu ya maisha aliyoamua kuishi.


“Ushamba tu, ndo nini sasa?  alisema mmoja wa wadau huku mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Dick akisema: “Msimuonee wivu mwenzenu, anakula bata zake na nyie hamjakatazwa.”
 
Dida alipoulizwa kuhusu kujianika hivyo alisema, hizo ni ishu zake binafsi na wapenzi wake wanapenda kuona kila anachokifanya, ndiyo maana anawawekea kwenye blogu yake.

 

MAREKANI YAUNDA SHERIA KUWADHIBITI WANAUME WANAOVAA SURUALI CHINI YA MAKALIO YAO


Sina shaka umeshasikia style za uvaaji wa suruali hususan kwa wanaume zenye majina kama mlegezo au kata k, au yawezekana ukawa huzijui kwa majina lakini umeshashuhudia vijana wamevaa suruali chini ya makalio. Kama ambavyo mabinti wamekuwa wakilaumiwa kwa mavazi ya kuonyesha miili yao hasa sehemu nyeti, na upande wa wanaume wamekuwa wakilalamikiwa kwa style hiyo ya uvaaji ambayo imeonekana kuigwa hata na vijana wadogo ambao bado wako shuleni. Katika hali ya kukerwa na tabia ya vijana kuvaa suruali chini ya makalio uongozi wa Wildwood, New Jersey nchini Marekani umeandaa sheria mpya itakayoweza kuwadhibiti wale wote...

 

HUU NDIO USHAHIDI WA MADAWA YA KULEVYA ALIOKAMATWA NAYO MSICHANA HUKO MISRI, NDIO YULE MSICHANA ALIYESEMEKANA ATANYONGWA.

Mrembo Fatma aka Brown Berry katika poseMrembo Fatma aka Brown Berry katika pose
Hizi picha ni za msichana anayetajwa kuwa ni Fatma aka Brown Berry wa Ilala Dar es Salaam ambae amekamatwa akisafirisha madawa ya kulevya au “unga” nchini Misri. Pia chini kuna video inayoonyesha maafisa wa Egypt wakionyesha jinsi unga huo ulivyofichwa ndani ya begi kabla ya kubambwaFatma akiwa na inayesemekana kuwa ni mwanaeFatma akiwa na inayesemekana kuwa ni mwanaeFatma aka Brown Berry akiwa na mpenzi wake Fatma aka Brown Berry akiwa na mpenzi wake
Hapa chini ni video inayoonyesha kukamatwa kwake na unga huo
Kumekua na taarifa kwamba msichana huyu amehukumiwa kunyongwa. Hata hivyo baadhi ya watu wametuma message kadhaa kwa bloggers kwenye mitandao ya kijamii kusema kwamba ni kweli ndugu yao amekamatwa lakini taarifa za hukumu ya kunyongwa sio za kweli, na hata hajahukumiwa bado Source: jestina-george

 

RASIMU YA KATIBA MPYA YAPENDEKEZA KUWEPO KWA SERIKALI TATU.....


Leo ni ufunguzi wa rasimu  ya katiba  mpya  na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema  kwamba  Rasimu hiyo  imependekeza kwamba matokeo ya rais yahojiwe mahakamani.

Kwa lugha nyingine ni kwamba katiba ijayo itaruhusu Rais kushtakiwa mahakamani endapo matokeo yake yatatiliwa shaka na wagombea wengine. 
Jaji Warioba ameyasema hayo  wakati wa uzinduzi wa Rasimu ya Katiba Mpya katika tukio la kihistoria nchini Tanzania.

"Imependekezwa kwamba matokeo ya Rais yatashikiwa mahakamani lakini kwa masharti," amesema Jaji Warioba hivi punde.

Jaji Warioba ametaja masharti hayo ni kwamba wagombea wa urais ndio watakuwa na haki ya kuhoji matokeo ya rais na si vinginevyo. Pili, matokeo hayo yanatakiwa kuhojiwa ndani ya mwezi mmoja tu na si vinginevyo.

Amesema pia tume imependekeza kuwapo kwa wabunge wa aina mbili ambao ni wabunge wa kuchaguliwa na wabunge wengine wa kuteuliwa na Rais.
 Pia amesema kwamba kutakuwapo kwa utaratibu wa wanawake kugombea katika majimbo. Kwa maana hiyo hakutakuwapo  wabunge wa Viti Maalumu.
Pamoja  na hayo, tume ya jaji Warioba imependekeza   kuwepo  kwa  serikali tatu ambazo ni  -serkali ya zanzibar, ya tanganyika na ya muungano.
mambo ya muungano  yaliyopendekezwa:
1)katiba ya jamhuri ya muugano wa tanzaia
2)sarafu na benki kuu
3)mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa
4)ushuru
5)ulinzi na usalama
6)usajili wa vyama vya siasa
7)uraia na uhamiaji

 

 

 

PICHA ZA TUKIO LA USIKU WATARAHE 08/04/2013 ZA KUMUENZI STEVEN KANUMBA LILIO FANYIKA LEADERS CLUB.


Pichani kushoto ni aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye usiku wa kumbu kumbu ya Marehemu Steven Kanumba,Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh Yusuph Mwenda akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Mama wa Marehemu Steven Kanumba,kwa niaba ya Mh Rais Jakaya Kikwete,kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu kufarikii kwa nyota huyo wa Filamu hapa nchini na kwingineko.Kumbukumbu hizo zimefanyika jana jioni kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali wa tasnia hiyo,wasanii wa muziki na kada nyinginezo mbalimbali,aidha katika Kumbukumbu hiyo pia kulizinduliwa Filamu ya mwisho aliyokuwa akiigiza Marehemu Kanumba kabla ya kufariki iliyoitwa Love & Power.
Pichani kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Mama wa Marehemu Steven Kanumba,kwenye maadhimisho kumbukumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu kufarikii kwa nyota huyo wa Filamu hapa nchini na kwingineko, Steven Kanumba.Kumbukumbu hizo zimefanyika jana jioni
kwenye viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali wa tasnia hiyo,wasanii wa muziki na kada nyinginezo mbalimbali,aidha katika Kumbukumbu hiyo pia kulizinduliwa Filamu ya mwisho aliyokuwa akiigiza Marehemu Kanimba kabla ya kufariki iliyoitwa Love & Power.
Mwakilishi kutoka Kampuni ya Clouds Media Group,Zamaradi Mketema akipokea tuzo ya heshima kwa niaba ya kampuni hiyo iliyotoa mchango mkubwa katika tasnia ya Filamu hapa nchini,kutoka kwa Mama yake,Marehemu Steven Kanumba,kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya kutimiza mwaka mmoja tangu afarikii nyota huyo wa Filamu hapa nchini na kwingineko, Steven Kanumba.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers wakipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Mama yake Marehemu Kanumba,kwa mchango wao mkubwa walioutoa kwenye tasnia ya Filamu hapa nchini.
Jacqueline Wolper looking fine















KWA PICHA ZAIDI BOFYA Michuzijr

Comments

Popular posts from this blog