HOFU imezidi kutanda kwa wakazi wa Mkoa wa Geita kufuatia matukio ya watu waliofariki dunia na kuzikwa miaka iliyopita kuibuka wakiwa hai. Mgonda Thomas (22), aliyefariki dunia kwa kujinyonga Mei 28, mwaka jana na kuzikwa siku iliyofuata, Ijumaa iliyopita aliibukia karibu na mlango wa nyumbani kwao akiwa hai. Tukio hilo ambalo bado la moto, lilijiri katika Kijiji cha Rumasa, Kata ya Buseresere, wilayani Chato mkoani Geita. Kwa mujibu wa chanzo, majirani ndiyo waliomshuhudia Mgonda akitembea barabarani saa tisa alasiri hatua chache kutoka kwenye mlango wa nyumba hiyo huku nguo zake zikiwa zimechakaa. Baba mzazi wa kijana huyo, mzee Thomas Msalaba (60) akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema majirani hao ndiyo waliomtaarifu kwamba mwanaye Mgonda alikuwa barabarani. āNiliondoka kwenda kumshuhudia kama kweli ni mwanangu. Nilipofika, nilimchunguza kwa umakini sana na kubaini alikuwa yeye. āAlama kubwa iliyokuwa kwenye mwili wa mwanangu ni kovu kwenye mkono wa...