Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bi. Jessica Mkuchu (kulia) akiongea kabla ya kuanza kwa mkutano wa Baraza Maalum la Katiba kwa Watu Wenye Ulemavu mjini Dodoma leo (Alhamisi, Agosti 15, 2013). Wengine ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Warioba (katikati) na Mjumbe mwingine Bw. Ally Saleh. Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Maalum la Katiba kwa Watu Wenye Ulemavu wakijadili rasimu ya katiba mjini Dodoma leo (Alhamisi, Agosti 15, 2013). Mkurugenzi wa Shirikisho la Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Bw. Novatus Rukwago akiongea leo (Alhamisi, Agosti 15, 2013) katika mkutano wa Baraza Maalum la Katiba kwa Watu Wenye Ulemavu linalofanyika mjini Dodoma. Mkalimani wa Lugha ya Alama Bw. Kudra Mnisi akiongea na wajumbe wa Baraza Maalum la Katiba kwa Watu Wenye Ulemavu leo (Alhamisi, Agosti 15, 2013) mjini Dodoma. Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Wakili Amon Anastaz akiongea katika B...