Edward Mordrake; Binadamu Mwenye Sura Mbili.
Edward Mordrake NI vigumu kuamini! Edward Mordrake ni Mwingereza mashuhuri wa karne ya 19 ambaye alijinyakulia tuzo za Nobel. Mordrake aliyetokea kwenye ukoo mashuhuri na wenye hadhi kubwa nchini humo, alitambulishwa zaidi kwa sura zake mbili, moja ikiwa kwenye uso wake wa kawaida na nyingine nyuma ya uso (kwenye kisogo). Cha kushangaza zaidi inasemekana kuwa sura yake ya kisogoni haikuweza kula wala kuongea chochote na hata ikijaribu kuongea maneno yalikuwa hayasikiki lakini iliweza kulia, kucheka na kusikia kila neno. Sura yake ya mbele ya uso imeelezwa kuwa ilikuwa ni nzuri na ya kuvutia (handsome). Watu waliomuona na kuzungumza naye, wanamsifu Mordrake kwa uzuri wa sura yake ya usoni na tabasamu lake, lakini balaa lipo kwenye sura yake ya kisogoni ambayo ni ya kutisha na inayofanana na sura ya “bibi kizee mchawi”. Simulizi za wafanyakazi wa jumba la kifahari alimoishi Mordrake, zinatolewa kwa siri, ambapo zinaeleza hali ya maisha ya huzuni y...