Vurugu Zatanda Kenyatta Akiapishwa, Polisi Wafunga Mtaa Kuzuia Mkutano wa NASA
Polisi wakiimarisha ulinzi eneo hilo. MTAA wa Jacaranda jijini Nairobi, Kenya, leo umefungwa na polisi ili kuzuia mkutano wa umoja wa vyama vya upinzani nchini humo, National Super Alliance (NASA) uliopangwa kwa ajili ya kuwakumbuka wafuasi wake 27 waliouawa wakati wa maandamano ya kupinga uchaguzi wa marudio uliofanyika zaidi ya wiki moja iliyopita. Mataili yakiwa yamechomwa moto. Mkutano huo ulipangwa kufanyika leo ambapo Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa kwa kipindi cha pili katika uwanja wa michezo wa Kasarani. Chumba vya kutunzia maiti katika jiji hilo pia kimefungwa na polisi ambapo watu hawatakiwi kufika hapo. Hali ilivyokuwa eneo la tukio. Polisi waliokuwa na zana zote za kuzuia fujo wamekuwa wakirusha mabomu ya machozi sehemu nyingi yakiwemo maeneo ya wafuasi wa NASA ambao wamefunga barabara kadhaa jijini humo. Wafuasi wa NASA wakipambana na polisi. Mpinzani mkuu nchini humo, Raila Odinga, amepinga mipango ya kumwapisha katika nafasi ya urais, a...