Mwisho Ephraim Mwampamba akiwa Mahakamani. NA Dustan Shekidele, RISASI mchanganyiko MOROGORO: Ikiwa takriban siku 40 tangu baba yao, Dk. Ephraim Njawala Mwampamba, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo Cha Sokoine (SUA) afariki dunia, mwanaye Mwisho Ephraim Mwampamba ameburuzwa mahakamani na kaka yake, Robert Ephraim Mwampamba, Jumatatu iliyopita. Kesi hiyo namba 197/2016 ilisikilizwa katika Mahakama ya Mwanzo Chamwino iliyopo Mazimbu mkoani hapa, ambapo Robert alimburuza mahakamani hapo mdogo wake huyo waliyechangia baba, akimtuhumu kumtukana matusi ya nguoni huku sehemu kubwa ya matusi hayo yakiwa ya kibaguzi. Robert Ephraim Mwampamba anayedaiwa kumbuluza Mwisho mahakamani. Kabla ya kufikishwa mahakamani hapo, Mwisho alitokea mahabusu alikolala kwa siku moja ambapo baada ya kesi kusikilizwa, alipata dhamana huku ikidaiwa kuwa kesi hiyo imemkalia vibaya kutokana na ushahidi unadaiwa upo. Akisoma kesi hiyo mahakamani hapo, Hakimu Amina Chungulu alidai Mwish...