Posts

Showing posts from February 3, 2018

Makamu wa Rais aguswa na Cover ya wimbo wa Nandy na Aslay

Image
Makamu wa Rais, Bi Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwa na wasanii Nandy na Aslay. MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana jioni aliwakaribisha nyumbani kwake wasanii wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka ‘Dogo Aslay’ na Faustina Charles maarufu kama Nandy kwa ajili ya mazungumzo mafupi na chakula cha jioni. Katika mazungumzo yake na wasanii hao, Bi Samia alieleza kuvutiwa sana na marudio ya kibao cha SUBALKHERI kilichorudiwa na wakali hao wa Bongo Fleva hivi karibuni na kuwapa wosia wa kuendelea kufanya kazi nzuri zaidi na kujiepusha na makundi mabaya.

Esma aweka wazi mahaba yake kwa Wema Sepetu

Image
Esma Abdul ‘Esma Platnumz’ MWANADADA Esma Abdul ‘Esma Platnumz’ ameonesha mahaba yake kwa staa mkubwa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akidai kuwa, amekuwa shosti wake kwa muda mrefu na hivyo hawezi kujitenga naye. Akipiga stori na gazeti hili, Esma alisema Wema ametoka naye mbali kiasi kwamba leo hii hawezi kumuweka pembeni na kujiweka zaidi kwa wifi wake wa sasa,  Zarina Hassan ‘Zari’. “Jamani Wema hata kidogo siwezi kumuweka pembeni, hata kama aliachana na kaka yangu lakini kwangu bado ana umuhimu. Kama kila anayeachana na kaka basi niwe naye mbali, nikifa inabidi nikazikwe Uganda au Sauzi maana Bongo sitakuwa na rafiki,” alisema Esma

JOKATE: 2018 NI NDOA NA FAMILIA PIA

Image
Jokate Mwegelo MWANAMITINDO ambaye ni kada wa CCM, Jokate Mwegelo baada ya kuanika kuwa mwaka huu ni sahihi kuingia kwenye maisha ya ndoa, ameibuka tena na kuanika kuwa 2018 ni mwaka wa kuwa na familia pia. Akiongea na Risasi Jumamosi Jokate alisisitiza kuwa mwaka huu ni wa neema kwake na kufafanua kuwa ana mpango wa kuanzisha familia yake. “Watu wajue tu kuwa mwaka huu nitaanzisha familia, sio kama ninawafumba lakini kwa uwezo wake Mungu wataona tu, wakae wakisubiri kwani lisemwalo lipo kama halipo linakuja,” alisema Jokate ambaye hakuweka wazi mwanaume atakayemuoa na kuanzisha naye familia

KISA BONGO FLEVA…AGNESS WA PICHA ZA UTUPU ASHAMBULIWA

Image
       Agness Mmasi MUUZA  nyago aliyejipatia umaarufu kwa kutupia picha za utupu mtandaoni, Agness Mmasi ameshambuliwa na mashabiki baada ya kujikita rasmi kwenye Muziki wa Bongo Fleva na kuachia Wimbo wa Danga unaoonekana  kukosa maadili. Akipiga stori na Mikito Nusu Nusu mara baada ya kuachia ngoma hiyo ambayo imejadiliwa sana kwa sababu ya maneno makali yaliyomo kwenye mashairi yake alisema, ngoma hiyo ameiimba kwa kuanika ukweli wa kile kinachoendelea kwenye jamii. “Nashangaa wanaonishambulia lakini ninachojua watu wengi   walikuwa hawaelewi nafanya kazi gani ya kunipa umaarufu, nikaona isiwe tabu bora nitimize ndoto yangu ya kuwa msanii wa muziki, sioni kama nimeimba maneno yasiyo na maadili ni vitu ambavyo vipo kwenye jamii, “alisema.