EXCLUSIVE: Rachel Kizunguzungu amrudia Mungu… ni baada ya yote aliyofanya na kupitia.
Mwimbaji Rachel ambaye ujazo wa jina lake uliongezeka baada ya kujiunga na nyumba ya vipaji Tanzania ( THT ) na kuanza kuachia nyimbo zake, amekaa kwenye Excluvie na mtangazaji wa Amplifaya ya CloudsFM Millard Ayo na kueleza kilichotokea mpaka akakwama na kukaa kwenye nchi ya watu kwa zaidi ya miezi saba, ishu yake ya kuvuta bangi na mengine. KUHUSU KUMRUDIA MUNGU: Ni kweli nimemrudia Mungu, ni maamuzi ambayo nimeyafanya mwenyewe baada ya kuona vitu ni vilevile, dunia ni ileile na watu ni walewale ndio maana nikaona sio vibaya nikaja na upande mwingine lakini hii haimaanishi kwamba nitakua nafanya muziki wa Injini, nitaendelea na bongofleva lakini muda mwingi nitautumia kanisani. KUHUSU OMAN: ‘Ni kweli nimekaa nchini Oman kwa zaidi ya miezi saba, nilikwenda kwa ajili ya kufanya shows tu lakini nikapata tatizo kwenye VISA yangu, nilifanya show za kuandaa mwenyewe ikafanikiwa mwanzoni lakini baadae hali ikabadilika, nilikua na VISA ya miezi mitatu na...