Bw. Ben Gitau na Bw. Steve Damelin KATIKA matukio ambayo wanaume wa Kenya wanaoana na wanaume wenzao katika nchi zinazoruhusu jambo hilo, mwanamme mmoja wa Nakuru, Kenya, amefunga ndoa na profesa wa hisabati wa Marekani. Bw. Ben Gitau (33) na Bw. Steve Damelin walioana wiki iliyopita huko Ann Arbor, Michigan, Marekani, Jumamosi alasiri ambapo baada ya tukio hilo wawili hao walionekana wakibusiana na kukumbatiana ambapo marafiki na wanafamilia walipiga vigelegele na kushangilia. Hata hivyo, mshauri mmoja wa masuala ya kifamilia , Mchungaji Philip Kitoto wa International Christian Centre, Nairobi,alilaani ndoa hiyo akisema: “Kiutamaduni na kwa mujibu wa Bibilia, ndoa na kujamiiana kati ya watu wa jinsia moja ni dhambi.” “Biblia iko wazi kwamba Mungu alituumba kwa taswira yake; mme na mke. Katika kitabu cha Mambo ya Walawi 18:22 Mungu anamwonya mwanaume kutofanya ngono na mwanaume mwenzake kama anavyofanya na...