Posts

Showing posts from September 18, 2013

ANGALIA PICHA YA DENTI WA MWAKA WA KWANZA AIBA SIMU NA KUWEKA SEHEMU ZA SIRI.

Image
Tukio hili limetokea huko Nigeria ambapo binti anayesemekana ni wa mwaka wa kwanza alikwenda kutembea katika hostel za wenzake na alipopata mwanya akaiba simu aina ya Black Berry. Hata hivyo baada ya mwenye simu kushtuka binti huyo aligoma kuichukua simu hiyo na ndipo watu walipoamua kuipiga simu na kuanza kuita ikiwa sehemu za siri. Baada ya tukio hilo wavulana kutoka vyumba vya pembeni walikuja na kumsachi huku wakimvua nguo, hakuwa na la ziada zaidi ya kuwa mpole wakati watu wakimpiga      

Mbwa waliotumika kumlinda Prince William jeshini wauawa

Image
-Kwa sababu ya kushidwa kupangiwa majukumu mapya au kupelekwa nyumbani kwa mwana mfalme  Mbwa wawili walinzi wa Prince William wa Uingereza wameharibiwa na kuondolewa katika viwanja vya kifalme vya ndege za kivita wakati Prince huyo ambaye alikuwa akifanya kazi ya kijeshi ya anga baada ya kushidwa kupangiwa kazi zingine mbwa hao waliteketezwa siku chache kabla ya mwana wa mfalme kuondoka. Prince William ambaye amepata mtoto hivi karibuni alikuwa katika majukumu yake ya kijeshi na mazoezi ya utafutaji na uokoaji katika eneo la kijeshi la North Wales wiki iliyopita. Ndani ya siku moja baada ya kuhama, walinzi wake mbwa wawili waliharibiwa kabisa siku ya Ijumaa wiki iliyopita. Msemaji wa Wizara ya Ulinzi Uingereza amesema mbwa hao aina ya shepherd Brus toka Ubelgiji na Ujerumani walikuwa wameezeka na hawakuweza kupangiwa majukumu mengine.

ANGALIA PICHA ZA PICHA MAMBA ALIVYO ZUA BALAA BAADA YA KUINGIA CHINI YA KITANDA HOTELINI

Image
Katika hali isiyo ya kawaida mamba mkubwa mwenye futi 8 amezua tafrani baada ya kuingia chini ya kitanda cha Mkurugenzi wa hoteli moja ya kitalii iitwayo Humani iliyopo pembezoni mwa mto Turgwe huko nchini Zimbabwe na kukaa zaidi ya masaa 8. Mr Whittall, ambaye ni mkurugenzi wa hoteli hiyo alisema kuwa mamba huyo aliingia kwa siri chumbani kwake na kukaa chini ya kitanda chake usiku na kugundulika asubuhi ya siku iliyofuata. Alisema kuwa mamba huyo alitoka nyuma ya pori lililopo karibu na hoteli hiyo ambapo hata yeye alipoamka hakumuona na alining’iniza miguu yake huku mamba huyo akiwa chini ya kitanda ambapo alitoka kwenda kupata kifungua kinywa kwenye mgahawa wa hoteli hiyo. Inaelezwa kuwa mamba huyo aligundulika na mfanyakazi aliyekuwa akifanya usafi katika chumba hicho na kupiga mayowe yaliyomshtua Mr Whittall ambapo alitoka mbia kwenda kushuhudia kulikoni na kumkuta mamba huyo akiwa chini ya kitanda chake kumbe ...

SEREKALI KUMLIMA BARUA BALOZI WA CHINI BAADA YA KUJIHUSISHA NA CCM

Image
Dar es Salaam. Serikali imesema mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini wanapaswa kutambua kuwa, wanawajibika kuheshimu Mkataba wa Kimataifa wa Vienna unaoainisha taratibu za diplomasia. Pia, inasema inajiandaa kumwandikia barua Balozi wa China nchini, Lu Younqing kutokana na hatua yake ya kujihusisha na mambo ya siasa. Wiki iliyopita, Balozi Lu alijitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika mkoani Shinyanga, huku akiwa amevalia moja ya sare za chama hicho, hatua ambayo imezusha mjadala miongoni mwa vyama vya siasa na wachunguzi wa mambo ya kidiplomasia. Akizungumzia kitendo hicho jana, Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, alisema Serikali inajiandaa kumwandikia barua ya kumkumbusha wajibu wake na kwamba itafanya hivyo baada ya kukusanya taarifa zake. Hata hivyo, Mahadhi alisema Tanzania na China zitaendelea kuwa marafiki wanaoshirikiana kwenye nyanja mbalimbali kw...

Waliolipua mabomu katika mkutano wa CHADEMA jijini Arusha wakamatwa

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo.  WATUHUMIWA walioingiza mabomu ya kurushwa kwa mkono yaliyotupwa Arusha Mei na Juni katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti na kwenyemkutano wa wa hadhara wa Chadema, Soweto mkoani Arusha, wamekamatwa. Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alisema hayo jana katika mkutano wa siku moja wa kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha, uliofanyika eneo la Olasiti.   “Watuhumiwa hawa siku si nyingi Kamanda wa Polisi wa Arusha, ataweka majina hadharani, watu wawajue na si wageni, ila kwa sasa kinachochunguzwa ni kutaka kufahamu waliowatuma kuingiza mabomu hayo na kwa lengo gani."   Mulongo alisema kwa sasa Polisi iko katika hatua za mwisho za mahojiano na watuhumiwa hao, ambapo mbali na kutaka kufahamu waliowatuma na malengo yao, pia wanatarajia kupata taarifa za waliorusha mabomu hayo.   Malengo mengine kwa mujibu wa Mulongo ni kuwafahamu watu wote w...