Posts

Showing posts from June 1, 2018

Wachezaji wa Real Madrid waandika haya baada ya Zidane kutangaza kustaafu

Image
Wachezaji wa Real Madrid kwa sasa watakuwa wapo katika wakati mkgumu baada ya kocha wao aliyewapa mafanikio makubwa katika kipindi kifupi Zinedine Zidane, Alhamisi hii kutangaza kustaafu kuifundisha timu hiyo. Wachezaji hao wakiongozwa na Cristiano Ronaldo, Sergio Ramos, Karim Benzema wameonyesha kusikitishwa kwa maamuzi ya kocha huyo na mpaka kushindwa kuzuia hsia zao na kuamua kumuandikia ujumbe wa kuumbuka mchango wake katika kipindi walipokuwa pamoja. Cristiano Ronaldo I’m just proud of being your player. Mister, thanks for so much. Sergio Ramos Mister, as a player and now as a coach, you decided to fire you at the top. Thank you for two and a half years of soccer, work, love and friendship. You leave but your legacy is already indelible. One of the most successful chapters in the history of our beloved @realmadrid As a player and coach you decided to say goodbye at the top. Thank you for two and a half incredible years. Your legacy will never be erased,

Zinedine Zidane kuifundisha timu ya Qatar

Image
Zinedine Zidane ambae alikuwa Kocha wa Klabu ya Real Madrid ameingia mkataba wa miaka minne ya kuifundisha timu ya taifa ya Qatar. Mapema hii leo habari zimeenea kuwa meneja huyo wa Real, Zinedine Zidane atakuwa akilipwa Euro milioni 15 kwa mwaka hii ikiwa na lengo la kuisaidia nchi hiyo inayotarajia kuanda michuano ya kombe la dunia mwaka 2022. Zidane ameiyongoza Real Madrid kwa misimu miwili na nusu, akifanikiwa kutwaa mataji tisa huku Jumamosi iliyopita akiipatia timu yake kombe la klabu bingwa barani ulaya.

Mkataba TanzaniteOne kufumuliwa

Image
WAZIRI wa Madini, Angellah Kairuki, amesema serikali imeagiza leseni ya uchimbaji wa ubia baina ya Shirika la Madini la Taifa (Stamico) na Kampuni ya TanzaniteOne Mining Limited (TML) ili utaratibu mpya uandaliwe kwa manufaa ya pande zote mbili. Aliyasema hayo bungeni jana alipowasilisha hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha. Alisema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kasoro iliyoibuliwa na Kamati Maalum ya Spika Kuchunguza Uchimbaji na Biashara ya Tanzanite katikati ya mwaka jana. “Serikali imeagiza leseni ya uchimbaji wa ubia baina ya Stamico na TML irudishwe serikalini ili utaratibu mpya uandaliwe utakaoiwezesha serikali, TML na mwekezaji wa kimkakati kushirikiana katika uchimbaji, uendeshaji katika mgodi huo kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Madini, Sura ya 123 kama ilivyorekebishwa na Bunge mwaka 2017,” alisema. Alibainisha kuwa mgodi wa ubia kati ya Stamico na TML ni miongoni mwa migodi ya tanzanite iliyopo Mirerani mkoan

WALIOISHIA VETA SASA WANAWEZA KUSOMA ELIMU YA JUU CHUO CHA UFUNDI ARUSHA

Image
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) imethibitisha matumizi ya mtaala unganishi wa masomo ya ufundi nchini utakaowawezesha wahitimu wa vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi(Veta) kuendelea na elimu ya juu.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtaala huo,Mkurugenzi wa Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi nchini,Dk Noel Mbonde amesema utasaidia kuwapa fursa vijana wengi waliotamani kuendelea na masomo ya ufundi ya juu kunufaika. Amesema serikali inathamini maboresho hayo yanayotoa nafasi ya kuwanoa wataalamu wa kutosha inayoenda sambamba na sera ya serikali ya awamu ya tano ya kufikia uchumi wa viwanda. Mkurugenzi wa Ufundi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Standi nchini,Dk Noel Mbonde akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mtaala Unganishi katika Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)jijini Arusha ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi(ATC),Dk Erick Mgaya. “Kulikua na tatizo la wanafunzi wetu wanaohitimu Veta kuendelea na kozi za juu za ufundi na sababu kubwa ilikua ni kukoseka

Tanzia: Mama wa Mbunge Hussein Bashe Afriki Dunia

Image
Mama mzazi wa Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini mkoani Tabora (CCM), Hussein Bashe amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa, katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhumbili jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa. Kupitia akaunti yake ya Twitter, Bashe amesema; “Ndugu zangu nimeondokewa na mama yangu mpendwa. Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.” Taarifa zaidi zitafuata baadaye.

ORODHA YA WAHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOCHAGULIWA JKT

Image
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) , limefanya uteuzi wa wanafunzi waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kutoka shule zote za Tanzania Bar a kwa mwaka 2018, kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria. Sanjari na uteuzi huo, JKT limewapangia Makambi ya JKT watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01-10 June 2018. Wahitimu hao, wamepangiwa katika Kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutupora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Makuyuni – Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, Nachingwea- Lindi na JKT Mtabila – Kigoma. Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti kambi ya Ruvu JKT iliyopo mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia wa jamii hiyo. Vijana watakaochaguliwa watatakiwa kujigharamia nauli za kwenda na kurudi kwenye makambi ya JKT w

Mwanafunzi aunda gari linalobadili jua kuwa Umeme

Image
Mwanafunzi mmoja nchini Kenya ameunda gari linalotumia kawi ya jua, gari ambalo limekuwa likiwavutia watu kutokana na kubadili jua kuwa umeme. Samuel Karumbo, 30, ni mwanafunzi katika chuo cha mafunzo anuwai cha serikali mjini Kitale, Magharibi mwa Kenya, amesema gari lake, ambalo lina mitambo mitatu ya sola iliyobandikwa, linaweza kusafiri umbali wa kilomita 50 kwa siku. Karumbo anasema mchana, sola huchukua nishati ya jua na kuibadilisha kuwa umeme ambao unahifadhiwa kwenye betri ambazo ndizo zinazotumiwa moja kwa moja kuliendesha gari hilo na pia wakati jua halijawaka sana. Gari hilo lina uzani wa kilo 120 na kwenye mteremko hutumia mvuto wa nguvu za ardhi badala ya umeme. Nguvu hutumia tu kwenye kupanda milima au maeneo yenye miinuko.