Posts

Showing posts from June 28, 2017

Viongozi wawili wa serikali wauawa Kwa Kupigwa Risasi Kibiti

Image
Viongozi wawili wa serikali za mtaa katika Kijiji cha Mangwi wilayani Kibiti mkoani Pwani wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumatano, Juni 28. Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga zimeeleza kuwa waliouawa ni Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi, Shamte Makawa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus. Aidha, kamanda wa polisi amesema kuwa tayari askari wamekwenda eneo hilo kwa ajili ya hatua zaidi. Hadi sasa watu zaidi ya 37 tayari wameuawa katika mfululizo wa matukio ambayo bado Polisi hawajafahamu ni nani mhusika na lengo haswa la kufanya hivyo.

Rais Wa TFF Na Katibu Wake Watiwa Mbaroni

Image
Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wanashikiriwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wapo katika Kituo cha Polisi Salander Bridge ili kupisha uchunguzi dhidi yao.  Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba alipokuwa akihojiwa na kituo cha Radio EFM leo. Misalaba amesema ni kweli wanawashikilia na taarifa zaidi wataitoa baada ya kumaliza uchunguzi wao. Licha ya kuwa tuhuma zinazowakabili hazijawekwa wazi, lakini mwezi uliopita ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliripoti kuhusu mabilioni ya shilingi yaliyobainika kuchotwa kwenye akaunti za TFF na kulipwa kwa wadau wa soka kinyume cha sheria. Miongoni mwa waliotuhumiwa kunufaika na fedha hizo ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi na aliyekuwa msaidizi wake, Juma Matandika. We

MBUNGE WA CHADEMA ASIMAMISHWA KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE

Image
Siku kadhaa zilizopita kutoka Bungeni Dodoma Wabunge wa CHADEMA Halima Mdee wa Kawe na Ester Bulaya wa Bunda Mjini walisimamishwa kutohudhuria vikao vya Bunge, leo June 28, 2018 Mbunge Conchesta Rwamlaza wa Viti Maalum CHADEMA amesimamishwa. Conchesta Rwamlaza amesimamishwa kutohudhuria Vikao vitatu vya Bunge linaloendelea kwa kosa la kusema uongo mbele ya Bunge akimtuhumu Mbunge wa Muleba Kusini Prof. Anna Tibaijuka kujimilikisha ardhi yenye ukubwa wa ekari 400 kinyume cha sheria taarifa ambazo sio za kweli. Aidha, Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imetoa msamaha kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari kwa kosa alilolifanya May 30, 2017 kudharau mamlaka ya Spika ikiwemo kupiga kelele Bungeni na kutupa karatasi ovyo. Nassari amepata msamaha huo kwa kuwa imeonesha ni mara yake ya kwanza kutenda kosa kama hilo kisha kupelekwa mbele ya Kamati.