NDOA YA KIBA YAACHA VILIO!
DAR ES SALAAM: Wakati mkali wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba āAliKibaā akitarajiwa kuangusha bonge la sherehe baada ya kufunga ndoa nchini Kenya, ndoa hiyo imedaiwa kuacha vilio vikali kwa wanawake ambao waliwahi kushea kitanda na msanii huyo, Ijumaa lina mchapo kamili. Kiba alitarajiwa kufunga ndoa hiyo jana mjini Mombasa nchini Kenya kisha kufuatiwa na bonge la sherehe mjini humo huku sherehe nyingine babākubwa ikitarajiwa kufanyika nchini mwishoni mwa mwezi huu. MTU WA KIBA ANENA Mtu wa karibu na AliKiba, amepenyeza habari kuwa, licha ya kwamba wao wanasherehekea harusi ya mkali huyo anayetamba na Wimbo wa Seduce Me, nyuma yake kuna vilio vingi kutoka kwa wanawake ambao walitembea na Kiba kabla. āKama unavyojua Kiba alishazaa watoto wanne, wale watoto kila mmoja ana mama yake. Sasa mama zao wanalia maana nao walikuwa wana matarajio ya kuolewa,ā alisema mtu huyo wa karibu aliyeomba hifadhi ya jina na kuongeza: BIBI HARUSI NJIA PANDA āKimsingi wamem...