Wabongo wafungukia simu feki kuzimwa
Stori: Gladness Mallya, Risasi Jumamosi DAR ES SALAAM: Baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania āTCRAā kutangaza kuzima simu feki usiku wa Juni 16, mwaka huu, wananchi mbalimbali wa Jiji la Dar, wamefunguka ya moyoni: BARIKI GASTON (MWENGE) āKuzimwa simu feki kumeniumiza sana na siyo mimi tu wapo wengi hasa wenye hali ya chini japokuwa zina madhara wangetuachia kwa muda mrefu kidogo ili tujipange kwanza.ā HIDAYA SAID (MWANANYAMALA) āSerikali ilivyofanya siyo vizuri kwa sababu hali ya maisha ni ngumu, nafanya mama ntilie hapa sina uwezo wa kununua simu orijino, wangetuangalia sisi watu wa vipato vya chini wasingezima ila wangezuia zile zinazoingia nchini lakini hizi tunazomiliki tubaki nazo.ā JOSEPH VENANCE (MWENGE) āSuala la simu feki kuzima limetuchanganya sana maana tulishazoea kununua kwa bei rahisi lakini sasa haya ni majanga kwa sababu mpaka upate hela ya kununua simu orijino ni kazi sana lakini inabidi tukubaliane tu hali halisi maana zina ...