Posts

Showing posts from June 15, 2018

MZEE MWINYI AONGOZA SWALA YA EID EL FITR DAR

Image
Mzee Ali Hassan Mwinyi akitoa nasaha zake kwa waumini wa dini ya Kiislamu. Mzee Ali Hassan Mwinyi (kulia) akijumuika na waumini wengine wa Dini ya Kiislam katika  swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar esa Salaam. Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum akitoa nasaha zake kwa waumini  wa dini ya Kiislamu. Taswira ya baadhi ya waumini waliojitokeza katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ilivyoonekana. Meneja wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia) akiwa ameungana na  waumini wengine wa Dini ya Kiislam katika swala ya Eid El Fitr iliyoswaliwa kwenye Viwanja  vya Mnazi Mmoja jijini Dar esa Salaam. Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (katikati) akisalimiana na mmoja wa waumini  baada ya kumalizika kwa swala ya Eid El Fitr. Sehemu ya waumini akinamama waliojitokeza katika swala hiyo kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja. Wa...

Phars blogspot Inawatakia Eid Njema

Image
Wafanyakazi wote wa Kampuni ya Global Publishers & Ent. Ltd inayochapisha Magazeti ya Amani, Championi, Ijumaa, Risasi na Uwazi na Spoti Xtra tunawatakia heri ya   Sikukuu ya Eid El Fitr wadau na wasomaji wetu wote. Aidha tunawashukuruni sana sana wadau wetu wote kwa sapoti yenu kubwa mnayotupatia na kutufanya tuendelee kuwa namba moja kwenye tasnia ya habari za magazeti pendwa na michezo hapa nchini. Nasi tunaahidi kuendelea kushirikiana nanyi kwa asilimia zote.

MO SALAHA YUKO FITI KUWAVAA URUGUAY LEO

Image
HATIMAYE Kocha Mkuu wa Misri,Hector Cuper amesema mshambuliaji wa timu hiyo Mohamed Salah yupo kamili kwa takribani asilimia 100 kucheza mechi yao ya kwanza ya fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Uruguay leo Ijumaa, Juni 15, 2018. “Ninaweza kusema karibu asilimia 100 mchezaji Mo Salah yuko vizuri kucheza mchezo wa wetu dhidi ya Uruguay, yeye binafsi yupo tayari kucheza tunachojaribu sisi ni kumpa ujasiri tu”, amesema Cuper. Mohemed Salah aliumia bega kwenye mchezo wa fainali ya UEFA Mei 26, kufuatia kukumbana na mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos. Awali ilihofiwa kuwa huenda akakosa fainali hizo lakini sasa inaonekana yupo vizuri kuiwakilishi nchi yake. Misri ambayo ipo Kundi A na timu za Russia, Saudi Arabia na Uruguay leo itaanza rasmi kampeni ya kusaka ubingwa wa dunia ambapo haikupata nafasi ya kucheza fainali hizi tangu mwaka 1990 ambapo Salah alikuwa hajazaliwa. Mechi hiyo itachezwa majira ya saa 9:00 Mchana kwa saa za Afrika Mashariki, kwen...

Wanawake Urusi watakiwa kutofanya mapenzi na raia wa kigeni

Image
Mbunge mmoja nchini Urusi anasema kuwa wanawake hawafai kufanya mapenzi na wageni wakati wa kombe la dunia huku akionya kuhusu watoto wanaozaliwa kutoka rangi tofauti. Tamara Plentyova mkuu wa kamati ya familia, wanawake na masuala ya watoto bungeni, alisema kuwa hata iwapo uhusiano huo utasababisha kufanyika kwa harusi, wanawake au watoto wao watachukuliwa na nwanamume huyo ambaye atakuwa raia wa kigeni. Mbunge huyo ni wa chama cha Kikomunisti, ''Hata wakiolewa, watawachukua, halafu watashindwa namna ya kurudi," Bi Pletnyova alisema katika kituo cha Govorit Moskva. "Baadaye watakuja kwangu, wasichana wakilia kwamba watoto wao wamechukuliwa''. Alisema kuwa wanawake waliopata watoto na raia wa kigeni wakati wa michezo ya Olimpiki ya 1980 mjini Moscow walisalia kuwa wanawake wasio na wanaume. ''Ni vyema iwapo ni mtu wa rangi inayofanana na yako lakini iwapo ni mtu wa rangi tofauti basi kunakuwa na shida''. '...