Posts

Showing posts from August 19, 2015

Jokate: Wazazi wasiingilie mapenzi ya watoto

Image
Staa wa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’. Brighton Masalu SIKU chache baada ya gazeti dada ya hili la Ijumaa Wikienda kuripoti juu ya wazazi wa Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ kumkataa Ali Kiba kama mchumba wake, binti huyo ameibuka na kuwataka wazazi kote nchini kuacha kuwaingilia watoto wao katika masuala ya kimapenzi, akidai jambo hilo ni vema wakiachiwa wenyewe. Akizungumza na gazeti hili, Jokate alisema ni vyema kama wazazi wakawaacha watoto wao waoe au kuolewa na watu wawapendao, kwani vinginevyo ni kuwaingilia maisha na uhuru wao binafsi, jambo ambalo si jema. “Unajua nimelala, madai ya Ally (Kiba), sitaki kuyazungumza sana, unajua mimi ni binti mtu mzima, ninao uhuru wa kumchagua nimpendaye kwa ajili ya maisha yangu, ifike mahali wazazi wawape uhuru watoto wa kufanya mambo yao, awamu hii siko tayari kuona naumizwa tena na familia juu ya uhusiano wangu,” alisema binti huyo kwa njia ya simu juzi.

Lulu amchokonoa Zari

Image
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’  akiendelea ‘kujibebisha’ kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Mwandishi Wetu UCHOKOZI! Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine baada ya kudaiwa ‘kujibebisha’ kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni kumchokonoa mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Tukio hilo lilijiri usiku mnene Jumapili iliyopita kwenye Ukumbi wa House Club uliopo Masaki, Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya bethdei ya DJ wa Diamond, Rommy Jones. Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyeweka kambi ukumbini humo, Lulu, bila kujali kwamba, Diamond alimwacha Zari nyumbani akimnyonyesha ‘baby girl’ wao, Latifah Nasibu a.k.a ‘Princess Tiffah’, alionekana akijiachia naye kimahaba huku akionesha ‘kummisi’ kinoma jamaa huyo. Mastaa mbalimbali wakiwa katika sherehe hiyo. ILIANZA HIVI Lulu, al...

HIKI NDICHO ALICHOKIJIBU ZARI THE BOSS WA DIAMOND PLATNUMZ KUHUSU MPANGO WA IVAN NA KING LAWRENCE

Image
Hatimaye Zari The Bosslady ameamua kumjibu ex wake Ivan na swahiba wake King Lawrenc ambao wamekuwa wakimtupia madongo kuwa mtoto wake Tiffah si wa Diamond, ni wao. King Lawrence alienda mbali zaidi kwa kutumia kampuni ya wanasheria kumtaka achukue vipimo vya DNA vya kichanga hicho chenye zaidi ya followers 80k kwenye Instagram. Zari ametumia Instagram kuwajibu kwa kudai kuwa wanachofanya wawili hao ni visasi ambavyo anaamini hufanywa na vilaza! “Visasi hufanywa na vilaza,” ameandika Zari kwenye Instagram. “BO$LADY anafahamu kuwa huzuni aliyonayo mtu mwenye chuki wakati akiangalia furaha na mafanikio yake ni adhabu tosha. Inabidi niyageuzie mgongo mambo yate ya kijinga yanayoendelea. Naendelea kuwaua kwasababu watu hutaka kuzima taa inayowaka zaidi kwao,” ameongeza. Diamond tayari ametoa majibu yake kufuatia hatua hiyo ya Ivan na Lawrenc

Asasambua mchana kweupe kumkomesha mchepuko

Image
M UME wa mtu sumu! Kitendo cha wanawake kutembea na waume za watu ni cha kawaida kabisa katika maeneo mengi nchini na wengi wamejikuta wakikutana na balaa, lakini tabia hiyo inaendelea kila kukicha. Samora Abdallah (pichani), Afisa Mtendaji wa Mtongani, Kata ya Mbuyuni, Kinondoni jijini Dar es Salaam, anao mkasa wa kusisimua ambao ni moja kati ya kesi nyingi alizopata kuzifanyia kazi ofisini kwake kama anavyosimulia; “Hata sijui nianzie wapi, kuna siku kundi la watu walifika ofisini kwangu, nilipohoji ujio huo kwa kuwa haukuwa wa amani, nikajibiwa kwa kuoneshwa kidole kwa dada mmoja aliyeshukiwa kuchukua mume wa mwenzie. Mara wakaanza kurushiana maneno machafu, nusura wakunjane, nikawazuia na kutaka kujua kulikoni. “Dada mmoja akaniambia kuwa binti aliyekuwa mbele yetu, anatembea na mumewe kwamba siku hiyo aliichukua namba yake kutoka kwenye simu ya mume wake na kuanza kuchat naye akijifanya ndiye yeye. Alizungumza naye mambo mengi na mwishowe akamtaka aje sehemu...

HARUSI YA MENINA ILIYOFUNGWA KWA SIRI KUBWA NIMEKULETEA PICHAZ HAPA TOKA AKIPAMBWA SALOON HADI KITU CHA MKEKANI!! UNAMJUA MUMEWE LAKINI ALIYEBEBA JIKOOOO

Image

CCM YATANGAZA RASMI KIKOSI CHAKE CHA KAMPENI 2015 JIJINI DAR LEO

Image
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi, katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam kuhusiana na uteuzi wa kamati ya Kampeni  kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015,ambayo itaongozwa   na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na  Wajumbe Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa jana Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto. Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja  na Ndugu Jonathan Njau (Singida Mashariki) na Ndugu Emmanuel Papian John (Kiteto). Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Kamati ...

MANCHESTER UNITED WAITANDIKA CLUB BRUGES GOLI 3 KWA 1

Image