ATELLITE YA AUSTRALIA YANASA MABAKI YA NDEGE KWENYE INDIAN OCEAN.
Habari kutoka Aaustralia ni kwamba Satellite ya nchi hiyo imeweza kubaini Kuna mabaki yanayonekana katika Bahari ya Indi yanayokisiwa kuwa ni Mabaki ya ndege na hasa hasa Ndege iliopotea ya Malaysia Airlines Flight 370 .............................. Waziri mkuu wa Australia amesema kuwa mitambo ya satelite ya nchi hiyo imenasa picha za vitu vinavyoonekana kama vifusi ambavyo huenda ni vya ndege ya Malaysia iliyopotea siku 13 zilizopita. Waziri mkuu huyo, Tony Abbott, ameambia bunge mjini Canberra kwamba picha za Satelite zimeonyesha vitu viwili vinavyofanana na vifusi vya ndege hiyo. Taarifa hii imejitokeza karibu wiki mbili baada ya ndege hiyo kutoweka na abiria zaidi ya miambili kutoka mjini Kuala Lumpur Malaysia kuelekea Beijing. Msemaji wa halmashauri ya usalama wa safari za ndege, John Young, baadaye alisema kuwa vifaa hivyo ambavyo kimoja kina ukubwa wa mita 24, vimeonekana umbali wa kilomita 2500 kusini Magharibi mwa pwani ya Austr...