Posts

Showing posts from March 10, 2017

VANESSA, DUMISHA HERI WAENDELEA KUSOTA POLISI KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA

Image
Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu operesheni mbalimbali zilizofanyika na jeshi hilo kwa wiki moja leo jijini Dar es Salaam. Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha dawa za kulevya zilizokamatwa katika operesheni leo jijini Dar es Salaam. Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akinyesha gari lililokuwa linatumika kwa ajili ya utapeli na magari yaliyokamatwa kwa tuhuma mbalimbali leo jijini Dar es Salaam. Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha pikipiki zinazopita katika barabara ya mabasi yaendayo haraka leo jijini Dar es Salaam. Kamanda Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi (CP), Simon Sirro akionyesha bunduki iliyoteleekezw

Je una herufi "M" katika kiganja chako? Hii ndio maana yake

Image
Watu wengi wanasema, mistari katika viganja vya kila binadamu vimebeba mambo mengi na maana nyingi kuhusu tabia yako na hatima yako kwa ujumla. Pia inasemekana watu wenye herufi  'M'  katika viganja vyao,ni watu wa aina muhimu sana.Inasemekana watu hawa wana sifa za ajabu.Wana ushirikiano mzuri na wafanyakazi katika aina yeyote ile ya biashara. Kama una mpenzi mwenye alama  'M'  katika kiganja chake,basi yakupasa kujua yupo makini katika uhusiano wenu.Hakuna utani,hakuna uongo na hakuna udanganyifu. Watu wenye herufi  'M'  katika viganja vyao, wana uwezo mkubwa wa kufanya mabadiliko katika maisha yao na daima utumia vizuri fursa wanazozipata katika maisha yao. Imekuwa ikijulikana kwa watu wa zamani, kwamba manabii wote walikuwa na alama hii katika mikono yao. Angalia mkoni wako na endapo ukijikuta una alama ya  'M'  basi tambua kwamba wewe ni mtu maalamu.

HIZI NDIO SENTENSI ZA MBUNGE LEMA KATIKA MKUTANO WAKE WA KWANZA ARUSHA

Image
Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema leo amefanya mkutano wa hadhara ukiwa ni mkutano wake wa kwanza tangu alipotoka mahabusu wiki moja iliyopita. Lema amefanya mkutano huo katika uwanja wa Shule ya Msingi Ngarenaro ili kuweza kuzungumza na wapiga kura wake kuhusu mambo mbalimbali yakiwemo ya maendeleo katika jimbo hilo. Miongoni mwa mengi aliyoyazungumza, Godbless Lema amezungumzia kukamatwa kwake ambapo amesema kuwa amekaa mahabusu kwa miezi minne pasipo kuwa na kosa kabisa. Aidha, ameeleza kuwa mahabusu kuwa watu wengi ambao wapo kule kwa kusingiziwa wengine wamewekwa tu kwa uonevu na hawana kosa, hivyo kama kiongozi ataendelea kuwapigania huku akiwasihi wakazi wa Arusha kuwaombea waliopo mahabusu. Mbali na Lema, mwingine aliyepata nafasi ya kuzungumza na umati huo uliojitokeza leo ni mwanachama mpya wa chama hicho, muigizaji Wema Sepetu. Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa

HUU NDIO UJUMBEE ALIOANDAKA STAA WEMA SEPETU KABLA YA MKUTANO WA MBUNGE LEMA

Image
MSANII wa filamu na malkia wa mtandao nchini Wema Sepetu ‘Madam’,  amejikita zaidi katika siasa baada ya kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hivi karibuni. Wema ameendelea kuzianika mitandaoni  baadhi ya harakati zake za kisiasa ikiwa ni pamoja na kujihusisha na shughuli za kijamii kama vile upandaji wa miti,  uliofanywa na baadhi ya viongozi wa chama hicho na leo kabla ya Lema kuhutubia, ameweka picha na ujumbe mtandaoni unaowahamasisha watu kufika katika mkutano huo. “All Ready Kwa Ajili ya Mkutano wa Mhe. GodBless Lema… See you there…. Giving MY Chadema A New Look… Y’all Know Black And Khaki Be our Colour…. A lil White to add Flavor wont Hurt Nobody…. #CallMeKamanda cc @upendosimwita1 @ _ elm _ @blowassa”, alimaliza Wema. Share this

UN SECRETARY GENERAL STOPS IN DAR ON HIS WAY TO NEW YORK

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Antonio Guterres (kushoto) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam jana. Mhe. Guterres alisimama kwa muda katika uwanja huo akitokea nchini Kenya kwa ajili ya kufanya mazunguzmo na Balozi Mahiga.  Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Mhe Guterres aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi zake za kutafuta amani nchini Burundi kupitia kwa Msuluhishi wa Mgogoro huo Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Benjamin Willium Mkapa. Aidha, Dkt. Mahiga aliwasilisha Salamu Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.  Waziri Mahiga akizungumza jambo huku Mhe. Guterres akimsikiliza kwa makini.  Dkt. Mahiga akiendelea kuzungumza na Mhe. Guterres huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa S

KESI INAYOMKABILI MAXENCE MELO YAAHIRISHWA TENA HADI APRILI 3

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema kesi namba 456 inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo na mwenzake na Mwanahisa Mike Mushi isipoendelea itafutwa. Hayo yalisemwa alhamisi hii na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kukerwa na upande wa Jamhuri ambao ulishindwa kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali badala yake ukaomba kuahirisha kesi. Mwendesha Mashtaka, Inspekta Hamis Said, alidai mbele ya Hakimu Simba kwamba kesi ilitakiwa kuanza kusikilizwa awali lakini wakili anayeiendesha anaumwa. Mwendesha mashtaka aliomba kesi hiyo iahirishwe mpaka tarehe nyingine itakayopangwa. Hata hivyo Hakimu Simba alieleza kukerwa na tabia ya kesi kuahirishwa na kusema wakati mwingine kama kesi hiyo haitaendelea ataifuta. Aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 3, mwaka huu na dhamana ya washtakiwa inaendelea. By: Emmy Mwaipopo

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA.

Image
Picha namba 1-5. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma leo tarehe 9/03/2017. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. PICHA NA IKULU