Posts

Showing posts from January 25, 2016

Uchaguzi Zanzibar Wazidi Kukosolewa..Mwanasiasa Mwingine Mkongwe Atoa ya Moyoni

Image
Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, ameshangazwa na uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kufuta uchaguzi visiwani humo. Amesema jumuiya za kimataifa zilishtushwa na uamuzi huo, amesema kinachotakiwa hivi sasa ni haki itendeke kwa kila kila upande kukaa na kutafuta suluhisho la kudumu. “Tanzania haijazoea migogoro ya siasa jambo ambalo si jema katika sura ya kimataifa,” alisema. Mwanadiplomasia huyo wa kimataifa ametoa kauli hiyo,baada ya Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha, kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi huo Oktoba 28, mwaka jana.  Alisema hatua ya kufutwa uchaguzi  wa Zanzibar ni jambo lililowashangaza  wengi kwa kuwa uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu, huku waangalizi wa ndani na nje wakiusifia katika ripoti zao. “Ni hatua ambayo imewashangaza wengi…imeibua sintofahamu kubwa katika nchi yetu kwa sababu uchaguzi uliopita Tanzania ilipata sifa,baada ya uchaguzi kufanyika kwa amani na utulivu. Lakini kitendo cha kufutw...

Wema Sepetu Could Now Be Having a Baby with BBA Winner Idris Sultan

Image
After some ups and downs with Diamond Platnumz and Ommy Dimpoz and scuffles with Zari Hassan over Diamond, Wema’s heart has finally found a resting place. And the lucky man is none other than Idris Sultan. Idris took to social media to declare his undying love for the former Miss Tanzania and even hinted that they could be expecting a baby: “ Me and You are not the ordinary. I sleep, eat, talk and wake up to only thinking about you. As much as utadhani kuwa you are blessed to have me no no i am blessed to have you. At 1st it was weird me kuangalia ndani ya kabati langu kuona nguo zako na viatu au ukiwa unaongea na mimi unaniambia vitu kama   "Hivi baby unahisi akiwa wa kiume utafanyaje maana naona umekazana na wa kike"   au ukiingia jikoni kwangu and take over my house with good food. The way you look at other women wakinisogelea, how you always know when i need a kiss or a tight hug. The way you force me kuangalia Disney channel, how you wake up e...

DARAJA LA KIGAMBONI KUANZA KAZI RASMI MACHI MOSI.

Image
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (wa nne kushoto), akitoa maelekezo kwa Msimamizi na Meneja Mkuu wa mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka mfuko wa Hifadhi ya jamii (N.S.S.F) Mhandisi John Msemo (wa kwanza kushoto) wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Katibu huyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.    Msimamizi na Meneja Mkuu wa mradi wa ujenzi wa daraja la kigamboni kutoka mfuko wa Hifadhi ya jamii (N.S.S.F) Mhandisi John Msemo, akimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sehemu ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (wa kwanza kulia)  sehemu ya kipande cha km 1.5 kilichopo upande wa Kigamboni kwa ajili ya upanuzi wa daraja hilo.   Mwonekano wa Ofisi za Daraja la Kigamboni zitakazotumiwa na wasimamizi wa daraja hilo linalotarajiwa kuanza kazi rasmi mwezi Machi mwaka huu.   Lango la kuingilia daraja la Kigamboni li...

DK.MAGUFULI AAGIZA MABALOZI WALIOMALIZA MUDA WAO WAREJESHWE NCHINI MARA MOJA

Image
 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu uamuzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli   kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili  2.0 Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa 2.1 Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Mahadhi Juma MAALIM ameteuliwa kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Kuwait, kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki. 2.2 Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kanda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha. Leo hii Mabalozi hao wanatakiwa kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliye chini yao. Mabalozi hao ni: 2.2.1 Bi Batilda Salha BURIAN...

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUWA MAHADHI JUMA MAALIM KUWA BALOZI WA TANZANIA NCHINI KUWAIT

Image
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam. Na Eleuteri Mangi-MAELEZO  Mhe. Rais Dkt. Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki. Vile vile Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha na kuwataka Mabalozi hao kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliyechini yao leo hii. Mabalozi hao ni Bi Batilda Salha Buriani, aliyeko Tokyo, Japan, Dkt. James Alex Msekela, aliyeko Rome, Italia. Kwa mujibu wa Balozi Sefue, Rais pia amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Bwana Peter Allan Kallaghe ambaye anarejea Wizara ya Mambo ya Nje, Afrik...

MATUKIO KUTOKA BUNGENI -MJINI DODOMA JANUARI 25, 2016.

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora , Angela Kairuki akiteta na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaji bungeni mjini Dodoma Januari 25, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majalaliwa  akisalimiana na Mbunge wa  Nkansi Ally Kessy kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Januari 25, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majalaliwa  akisalimiana na Mbunge wa  Mbozi Magharibi,David Silinde kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Januari 25, 2016. Katikati ni Mbunge wa Nkansi, Ally Kessy. Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akisalimiana na Mbunge wa Songwe, Philip Mulugo  kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma  Januari 25, 2016. Katikati ni mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wazee kutoka jimbo la Chemba  Ofisini kwake bungeni mjini Dodoma Januari 25,2016.  Kushoto kwake ni Mbunge wa Chemba Juma Nkamia. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)