KIPA WA SIMBA AFUNGIWA MIAKA 10, GEITA GOLD NA POLISI ZASHUSHWA DARAJA
Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya Makamu Mwenyekiti wake, Wakil Jerome Msemwa leo imetoa maamuzi ya shauri la upangaji matokeo kwa mechi za Kundi C Ligi Daraja la Kwanza. Akisoma hukumu hiyo baada ya kumaliza kuwahoji viongozi wa klabu na Wenyeviti wa vya vyama vya mikoa husika jana, Wakili Msemwa amesema adhabu hizo zimetolewa kwa kufuata Kanuni za Nidhamu za TFF, na nafasi ya kukata rufaa kwa wahusika juu ya maaamuzi hayo ziko wazi. Klabu za Geita Gold (Geita), JKT Oljoro (Arusha) na Polisi Tabora (Tabora) zimekutwa na hatia ya upangaji wa matokeo na kupewa adhabu ya kushushwa daraja mpaka ligi daraja la pili (SDL) msimu ujao. Upande wa klabu ya JKT Kanembwa FC ya mkoani Kigoma, imeshushwa daraja mpaka kwenye ngazi ya ligi ya mkoa (RCL), baada ya kushika nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi lake, Kundi C. Kamati ya Nidhamu imewafungia maisha kutojihusisha na mpira wa miguu mwamuzi wa mche...